Ukichukua video ya ajali Dubai unaweza kutozwa faini ya Tsh. Milioni 100 au zaidi au kifungo cha miezi 6 au vyote kwa pamoja

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Kuchukua video ama picha ya matukio ya ajali si jambo la kiungwana, lakini pia linakiuka haki ya faragha yao kulindwa na kuvunja sheria ya taarifa binafsi na faragha. Picha au video zinazochukuliwa zinaweza kuwa za kudhalilisha na kushusha utu wa watu waliohusika kwenye ajali hiyo.

Kwa upande wa Dubai ni kosa kuchukua video za matukio ya ajali, na kwa kukiuga agizo hilo unaweza kutozwa fine kama Tsh. Milioni 100 mpaka milioni 300 au kifungo cha miezi sita jela, au vyote kwa pamoja.

Makosa mengine ambayo yanaweza kukuingiza matatani na kukufanya ulipe faini kubwa ni pamoja na kudhihaki au kutukana watu au hata mwanafamilia, na kosa linakuwa kubwa zaidi hasa aliyedhihakiwa mwanawake, ambapo unaweza kulipa fine ya mpaka Tsh. Milioni 500 na wakati mwingine kwenda jela.

Kulisha wanyama wanaozura ovyo mtaani kama paka na mbwa ni kosa pia na unaweza kulipa faini au kukaa jela kwa siku kadhaa, lakini pia hauruhusiwi kuanika nguo kibarazani, na kukiuka agizo hilo unaweza kutozwa faini ya kama laki 3 ya Kitanzania.

Kwa Tanzania Sheria ya Kanuni za adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 chini ya kifungu cha 162(1) (a) (b) kinakataza pia kuchukua au kusambaza picha, video, au taswira za miili ya marehemu, watu waliokufa, waathiriwa wa uhalifu, au matukio ya kutisha ila kwa madhumuni maalum kama vile uchunguzi wa jinai au picha kwaajili ya shughuli za mazishi.
 
Naunga mkono hoja hii, sio uungwana kupiga picha au video eneo la ajali, maana ni upumbavu wa hali ya juu, toa msaada sio kupiga picha
 
mkuu sio sheria tu, huko dubai hizo sheria zinatekelezwa kikweli, Hiyo miezi sita unakwenda ndani kweli kimasihara tu hakuna kutoboa.
 
Back
Top Bottom