Yanga yagongwa faini ya Tsh. Milioni 5 kwa kuingiza Timu kwa mlango wa nyuma

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania imevitoza faini Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya makosa kadhaa katika mchezo dhidi yao uliyochezwa Novemba 5 2023 na Yanga kushinda 5-1.

Kamati hiyo imeipiga Yanga faini ya Tsh. milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango sio rasmi kuelekea mchezo huo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba SC imetozwa faini ya Tsh. milioni 1 kwa kosa la Wachezaji wake kuchelewa kutoka vyumbani na kupelekea mchezo huo kuchelewa kuanza kwa takribani dakika 4 kutoka vyumba vya kubadilishia nguo na kupelekea kuharibu program za mrushaji matangazo (Azam TV).

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania imefikia hatua ya kuwafungia miezi 6 kuingia viwanjani Mashabiki wanne wanaodaiwa kuwa wa Simba SC kutokana na kumshambulia Shabiki wa Yanga wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Ihefu FC uliyochezwa Benjamin Mkapa na Simba kushinda 2-1.

Mashabiki hao waliofungiwa ni Hassan Khatibu, Hamza Dafa, Patrick Shelukindo na Shaban Anga wamefungiwa kuingia michezo yote ya TFF, Bodi imewataka Mashabiki kujiepusha vurugu wawapo uwanjani.

20231117_164703.jpg
20231117_164707.jpg
20231117_164709.jpg
20231117_164711.jpg
20231117_164828.jpg
 
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania imevitoza faini Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya makosa kadhaa katika mchezo dhidi yao uliyochezwa Novemba 5 2023 na Yanga kushinda 5-1.

Kamati hiyo imeipiga Yanga faini ya Tsh. milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango sio rasmi kuelekea mchezo huo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
6616[/ATTACH]View attachment 2816617
Sawa
 
Wasomi wetu uchwara ndio mjifunze sasa hawa akina mudi utajiri wao sio wa hardwork wala swaga za pasion ni wanamachimbo yao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom