'Who created God' is an Illogical Question!

'Who created God' is an Illogical Question!

gasgas
Noted. Kwa sasa ngoja tusubiri jamaa aje na proof ya msahafu wake uitwao truth table. Akishindwa kuthibitisha kile ambacho ni authority yake asiendelee kuuliza kuhusu Mungu!

Hawezi kuja na proof hiyo unayotaka aje nayo, atageuza maneno na kuanza kutuchezea mchezo wa lugha ili atoke kilingeni, na hatimaye atakimbilia kuuliza maswali. Anapenda kuuliza, lakini hataki kuelewa, na mbaya zaidi anapoulizwa badala ya kujibu atakuja na uchambuzi wa maneno, muundo wa sentensi, n.k.

Huyu ni muumini wa dini ya Wakana Mungu ambaye bila shaka anatumika kupotosha wengine wenye uelewa mdogo. Kuna kusudi analotumikia si bure.
 
Ngoja aje na evidence ya Truth Table kwanza la sivyo sina cha kujadili naye huyu ndugu kama hawezi ku prove basis yake ya argumentation 🙂

Never! Hawezi kuja nayo hii, atafanya juu chini kubadilisha hoja. Ndivyo alivyo, na watu wa aina hii itakuwa shida sana kujifunza vitu vipya maana imani yake inakataa japo yeye atakuja na theory za hataki imani ila kuelewa!
 
Bado unahubiri.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitiaha.
Kiranga wewe una balaa sana.
Ila unaleta chachu ya watu kijifunza zaidi. Na kuisoma dini yao vyema na sio kuamini tu kwasababu walizaliwa na kujikuta wapo chini ya wazazi wenye kuamini imani fulani.

Dhana yako ya Mungu hayupo ni chachu tosha.
Lakini mimi kwa mara nyingine tena, niseme tu kwamba:-
Mungu yupo.
Kwanini Mungu yupo, kwasababu kuna Ulimwengu ambao yeye ndiye aliyeuumba.

Hakuna yeyote mwenye uelewa wa ulimwengu, mwenye maelezo ya ndani kabisa juu ya features zote za ulimwengu isipokuwa YEYE Mungu.

Kiranga, unamjua mwenye Quran?
Mwenye Quran ni yule aliyeuumba Ulimwengu.

Ngoja niachie hapo kwanza.
 
Hujui hata kusoma.

Wapi nimesema tulishia kwa mimi kukuuliza maswali hayo?

Ndiyo maana hatuelewani. Hujui kusoma.
Mimi kusoma najua na ndiyo maana hata wewe unaniuliza maswali humu,ila wewe una tatizo la kuelewa unachokisoma.

Nimekuuliza swali tuliishia wapi,sasa kwa sababu una tatizo la kutokuelewa unachokisoma ukaanza kuniuliza maswali badala ya kusema tulipoishia.

Nimekuuliza uthibitisho wa imani ya kuwa mungu yupo ni hadi atakapoonekana mungu kama ambavyo wewe hadi ulione jua ndiyo iwe uthibitisho wa imani yako kuwa jua litachomoza kesho?
 
Mungu mwenyewe yuko subjected to logic hivyo ana uwezo wote. Kama Mungu yupo above logic je anaweza kuumba kiumbe chenye uwezo kumzidi yeye?
 
Don't flatter yourself.Huna ubongo wa kuweza kunitoa povu.

"Unaniambiaga" is not a Swahili word.

Mjini umekuja na mwenge nini?

Learn to spell Swahili first before you step to me.
Sawa mkuu nimekuelewa.

Haya naomba unifafanulie alichokieleza maxime.
 
Nataka kusema kama nilivyosema/ulivyosoma, kama hujaelewa changanua kitu gani ili nipate kufanunua ila kiufupi huwezi kuwa na uwezo wa kutatua jambo fulani ambalo Lina madhara kwa watu/jamii ukaiacha wakiangamia halafu ukasema au kudai unawapenda!!! Can you? Why The so called God allowed the devil to exist & misleading us? Lengo lake ni nini mkuu? Kaumba viumbe wake dhaifu halafu yeye huyo huyo atawatia kwenye moto wa milele!!! Kwann hakutuumba wakamilifu tangu mwanzo? Ili tumtumikie.
Kwahiyo unataka kusema Mungu hatupendi sie viumbe wake aliyetuumba? au sijaelewa
 
Bado unahubiri.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitiaha.
Unasema huwezi kuthibitisha kitu ambacho bado hakijatokea na ndiyo huwezi kuthibitisha kuwa jua litachomoza hadi litakapo chomoza,sasa hebu thibitisha kitu unachokiamini ambacho tofauti na hivyo.
 
Hapana,

Nimekuletea kitu ukakikataa.

Nikasema sawa. Ili wote tuwe pamoja hatufarakani, ili nisikuletee uthibitisho halafu wewe uukatae, basi nieleze viwango vyako unavyovitaka na mimi nijipime kabla ya kukujibu nizingatie viwango.

Uthibitisho wenye ithibati maana yake ni nini? Kwangu naona kama unarudia neno moja lile lile tu kama mtu anayesema "uthibitisho wenye uthibitisho". Etymology ya uthibitisho na ithibati ni moja.

Sasa unaposema ithibati yenye uthibitisho au uthibitisho wenye ithibati au uthibitisho wenye uthibitisho, maana yako hasa ni nini?

Na unaweza kutoa uthibitisho kama huu kuonesha Mungu yupo?

Umeongelea "usiokuwa na ukinzani", nimekuambia kwamba Mungu wako ana contradiction (ukinzani).

Hujaweza kuondoa contradictions hizo.

Sasa leo wewe ambaye hujaweza kuondoa ukinzani katika dhana ya kuwepo kwa Mungu wako ndiye uje kuniambia mimi nitoe uthibitisho )ambao hata husemi viwangi vyake) ambao hauna ukinzani?

Utanitakaje nifanye kitu ambacho mimi nilianza kukutaka wewe ukifanye halafu ukashindwa?

Tena hata bila ya kuniambia misingi ya unachotaka nifanye ni ipi?

Kweli unataka mjadala au unaleta inda ya kinda tu hapa?
Hujaleta uthibitisho Wenye ithibati,ya kuridhisha,kwa kuthibitisha,mabaya.
Utajuwaje haya ni mabaya,na iwe ni mabaya kwa wote walioko katika hadhira.Huwenda wewe kwa mtizamo wako ukaona ni mabaya,lakini upande wa pili wa hadhira,uone sio mabaya.
Kwa mfano wapo wanaona nyoka si kitoea kizuri kuliwa,lakini wapo wanaokula nyoka,na wanaona ni kitoeo kizuri tu.Kwa upande wasiokula nyoka watasema kwa nini nyoka akaumbwa na hana manufaa yoyote,lakini upande wa walaji wa nyoka wanaona ana manufaa na kitoeo kizuri sana.
Kwa hiyo huwezi kuwa na uthibitisho wenye ithibati,kwa jambo unaloliona wewe,kimtizamo wako bila kuwa na uthibitisho wenye ithibati,je upande wa pili wa hadhira,wanahisi kama ninavyohisi?
 
.
Hivi kuna mtu hapa duniani anayeona kwamba lile tetemeko la Kagera lililoua watu 17 na kujeruhi mamia ni jambo jema. That is a natural evil that casts a serious doubt on divine omnipotence...Jibu hoja bila kuikwepa
 
Itakuwa wewe umekuta mjadala katikati,bila kujuwa umeanzia wapi.Mjadala ni kuhusu Mungu,kuleta mabaya,ili kitu tukijuwe ni kibaya,kuna uthibitisho upi ni kibaya,kilicholetwa na Mungu.
Kwa upande wako jibu la Mabaya yanaonekana kwa wote,yanasababishwa na sisi wanadamu wenyewe.Hilo tetemeko,lisingekuwako ila ni binadamu wenyewe,baada ya kutumia silaha kali za maangamizi,fikiria majaribio ya kurusha silaha kali zilizofanywa na Korea,kwa upande wa Korea wameona ni kitu kizuri,lakini kwetu ni huzuni kubwa,tumepoteza wapendo wetu(usitukumbushe,bado tuna huzuni kubwa).
Maradhi mbalimbali yanaowasumbua binadamu,wataalamu wanatuambia asili yake ni vitu vilivyotengenezwa na binadamu kwa mfano Cancer,Ukimwi,Ebola,Ndui nk.
Ukija upande wa kuzaliwa vilema,wataalamu wa tiba wote wanasema mtoto akizaliwa na kasoro yoyote ni kosa la kibinadamu,ima mama mjamzito amechelewa kwenda clinic au ametumia madawa bila ushauri wa wataalamu wa uzazi.
 
Hakuna haja ya malumbano.Jawabu la hoja yako ni rahisi sana..Mimi na wewe tuna tofauti ya imani kuhusu Mungu.Wewe ni atheist mimi ni theist.

Atheism ni hali ya kutokuwa na imani na uwepo wa Mungu.Theism ni hali ya kuwa na imani ya uwepo wa Mungu.Kuna wanao amini Mungu mmoja kama waislam.Kuna wanaoamini Mungu watatu kama wakristu na kuna wanao amini Mungu jike na dume yaani miungu wawili.

Tafiti zinaonyesha atheists(wapagani) wanaweza kufika takribani asilimia nane .mpaka 12 ya watu wote duniani.Mahali kama China Atheists wanaweza kufika mpaka 60% ya wachina wote.

Nimalize kwa kusema kuwa Mungu ni imani.Mungu hazibitishwi.Kama unaona hakuna ushahidi wa uwepo wa Mungu basi wewe ni "Atheists" na mpo wengi tu duaniani.
Sina tatizo na imani.

Naelewa imani ni nini. Natetea haki ya kila mtu kuwa na uhuru wa kuamini anavyotaka kama ilivyoandikwa katika "The Universal Declaration of Human Rights" see Universal Declaration of Human Rights - Wikipedia

Sina tatizo na imani.

Ila naelewa kwamba mtu akija na kuniambia imani yake ndiyo ya kweli, nina haki ya kumuuliza maswali anithibitishie.
 
Kiranga wewe una balaa sana.
Ila unaleta chachu ya watu kijifunza zaidi. Na kuisoma dini yao vyema na sio kuamini tu kwasababu walizaliwa na kujikuta wapo chini ya wazazi wenye kuamini imani fulani.

Dhana yako ya Mungu hayupo ni chachu tosha.
Lakini mimi kwa mara nyingine tena, niseme tu kwamba:-
Mungu yupo.
Kwanini Mungu yupo, kwasababu kuna Ulimwengu ambao yeye ndiye aliyeuumba.

Hakuna yeyote mwenye uelewa wa ulimwengu, mwenye maelezo ya ndani kabisa juu ya features zote za ulimwengu isipokuwa YEYE Mungu.

Kiranga, unamjua mwenye Quran?
Mwenye Quran ni yule aliyeuumba Ulimwengu.

Ngoja niachie hapo kwanza.

Asante kwa kuiona challenge ninayoileta bila kuichukia wala kuibeza.

Nilivyokuwa mdogo, kama nikiwa na miaka 10 hivi, nilikuwa nasikiliza kanda ya mabishano ya kidini kati ya Waislamu na Wakristo. Ikafikia kipindi Sheikh wa Kisslamu akawa challenged.

Sikumbuki vizuri details, lakini kuna maneno alisema yule Sheikh nayakumbuka mpaka leo.

Kabla ya kujibu alisema "Muislamu haogopi chellenge.Muislamu haogopi challenge".

Nashukuru kwamba wewe huogopi challenge. Kuna Muislamu nilim challenge hapa mpaka akashindwa kuikubali Quran, ikawa kimsingi anamkana Allah huku anajinadi uislamu. Nikamshangaa sana.

Kwa kuwa umefurahia uwezo wangu wa kuwafanya watu wafikiri zaidi, nitakupa msemo mmoja watu wanaopenda logic wanautumia na kukuomba unipe maana yake, au kama hujui, uitafute na kunieleza maana yake ni nini.

Ukinieleza nitakuambia kwa nini nimekupa msemo huu.

Unafahamu "non sequitur" ni kitu gani?

Naomba unieleze kwa maneno yako maana ya "non sequitur".
 
Mimi kusoma najua na ndiyo maana hata wewe unaniuliza maswali humu,ila wewe una tatizo la kuelewa unachokisoma.

Nimekuuliza swali tuliishia wapi,sasa kwa sababu una tatizo la kutokuelewa unachokisoma ukaanza kuniuliza maswali badala ya kusema tulipoishia.

Nimekuuliza uthibitisho wa imani ya kuwa mungu yupo ni hadi atakapoonekana mungu kama ambavyo wewe hadi ulione jua ndiyo iwe uthibitisho wa imani yako kuwa jua litachomoza kesho?
Ndiyo.

Wewe unaweza kuthibitisha kitu ambacho hakijatokea?

Mwanga wa jua unaouna wakati wowote ule unapoona mwanga wa jua hapa duniani umesafiri kwa dakika nane na sekunde 20.

Hilo lina maana kwamba ikiwa saa moja na dakika nane na sekunde ishirini, hulioni jua kama lilivyo saa moja na dakika nane na sekunde ishirini, unaliona jua kama lilivyokuwa saa moja kamili.

Hilo lina maana jua likizimika saa moja kamili, kwetu hatutajua lolote lile kuhusu kuzimika huku mpaka saa moja na dakika nane na sekunde ishirini.

Sasa kama hatujui na hatuwezi kujua jua lilivyo sasa hivi tu, tutajuaje jua litakavyokuwa kesho?

Zaidi ya yote, utathibitishaje kwamba jua halitazimwa na kitu usichokijua leo na lisichomoze kesho?
 
Hujaleta uthibitisho Wenye ithibati,ya kuridhisha,kwa kuthibitisha,mabaya.
Utajuwaje haya ni mabaya,na iwe ni mabaya kwa wote walioko katika hadhira.Huwenda wewe kwa mtizamo wako ukaona ni mabaya,lakini upande wa pili wa hadhira,uone sio mabaya.
Kwa mfano wapo wanaona nyoka si kitoea kizuri kuliwa,lakini wapo wanaokula nyoka,na wanaona ni kitoeo kizuri tu.Kwa upande wasiokula nyoka watasema kwa nini nyoka akaumbwa na hana manufaa yoyote,lakini upande wa walaji wa nyoka wanaona ana manufaa na kitoeo kizuri sana.
Kwa hiyo huwezi kuwa na uthibitisho wenye ithibati,kwa jambo unaloliona wewe,kimtizamo wako bila kuwa na uthibitisho wenye ithibati,je upande wa pili wa hadhira,wanahisi kama ninavyohisi?
"Uthibitisho wenye ithibati" maana yake nini?

Mbona unarudia neno moja kwa mtindo tofauti tu?

Hujajibu swali langu, unaamini Quran? Unamuamini Allah?
 
Ndiyo.

Wewe unaweza kuthibitisha kitu ambacho hakijatokea?

Mwanga wa jua unaouna wakati wowote ule unapoona mwanga wa jua hapa duniani umesafiri kwa dakika nane na sekunde 20.

Hilo lina maana kwamba ikiwa saa moja na dakika nane na sekunde ishirini, hulioni jua kama lilivyo saa moja na dakika nane na sekunde ishirini, unaliona jua kama lilivyokuwa saa moja kamili.

Hilo lina maana jua likizimika saa moja kamili, kwetu hatutajua lolote lile kuhusu kuzimika huku mpaka saa moja na dakika nane na sekunde ishirini.

Sasa kama hatujui na hatuwezi kujua jua lilivyo sasa hivi tu, tutajuaje jua litakavyokuwa kesho?

Zaidi ya yote, utathibitishaje kwamba jua halitazimwa na kitu usichokijua leo na lisichomoze kesho?
Kwahiyo kitendo cha wewe kuisubiri kesho ifike ndiyo kuthibitisha kwenyewe huko au ni hali ya kusubiri kuona kama unachokiamini kitakuwa ni kweli au sio kweli?
 
"Uthibitisho wenye ithibati" maana yake nini?

Mbona unarudia neno moja kwa mtindo tofauti tu?

Hujajibu swali langu, unaamini Quran? Unamuamini Allah?
Ikiwa hujui uthibitisho Wenye ithibati,ilikuwaje useme Mungu hayupo.
Mimi Naamini Allah na Qur'an.
 
Back
Top Bottom