Unapimaje u-shaghalabagala wa kitu? Unapimaje kitu kama kiko kwenye order au la?
Kwa kuangalia logical consistency. Kama kitu hakina logical consistency, hakina order. Contradiction ni namna moja ya kukosa logical consistency na order. Mungu wenu mnasema ni Mungu wa order halafu hapo hapo hana logical consistency. Hiyo ni contradiction nyingine.
Kuna tatizo gani kusema kiranga yupo na hayupo at same time in the same sense?
Hapo utaonekana hujui the laws of physics na labda una matatizo ya akili. Kiranga hawezi kuwa yupo na hayupo at the same time in the same sense. Ukiamini hilo siwezi kushangaa unaamini Mungu ambaye hayupo yupo.
Kama hakuna Mungu hakuna maana. Maana unaitoa wapi?
Logical consistency haimuhitaji Mungu. Maana inaweza kutoka katika logical consistency. Mungu wenu kakosa logical consistency, hivyo kakosa maana
Kwani kuna tatizo gani kuishi katika dunia ya namna hiyo?
Tatizo ni kwamba hata kuuliza swali hilo umetumia logical order ya alphabet. Ulimwengu ambao hauna logical consistency hata wewe usingekuwepo kuuliza swali hili.
Jua lisingechomza in order, hakuna chochote ambacho kingeweza kufanyika in order.
Kwa hiyo tatizo ni ukweli kwamba usingeweza kuishi at all. The fact kwamba unaishi inaonesha unaishi katika ulimwengu wenye logical consistency
Kama hakuna Mungu hakuna order ni chaos kama ulivyoandika. Bahati mbaya kwako ni kuwa Mungu yupo na siku ya siku utakutana naye na huna la kufanya kuhusu hilo!
Hapana. Mungu wenu ambaye kwa upande mmoja mnasema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote na upande wa pili kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ndiye hana order. Hana logical consistency. Ana contradiction.
Upande mmoja tunaona anatupa proposition (p) ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote huku upande mwingine anatupa proposition negation of p (-p) kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Unaweza kuondoa contradiction hii?