Sio kweli kwamba Mugabe anataka kushindana na Wazungu, au anaamini hali ya Zimbabe inatokana na nguvu za nje. Hana hiyo dhati.
Anachofanya Mugabe ni sawa na Osama bin Laden anaposema ujasusi ni juhudi za kutetea Uislamu unaotishiwa na Wamagharibi ikiongozwa na US. Hiyo inamsaidia kupata sapoti ya wapenda Uislamu, na wachukia ukoloni mamboleo wa US na siasa zao za kibeberu (imperialism). Kama unachukia ubeberu, na ukoloni mamboleo na pia ni mpenda Uislamu unaweza kujikuta unajiunga na kambi yake ya mafunzo, kumbe ukweli ni kwamba mzizi wa fitina haswa ni bifu yake na watu wa kwao huko Uarabuni ambao walikataa mawazo yake fulani fulani miaka kibao iliyopita.
Anachofanya Mugabe kunyooshea kidole Magharibi ni pretext kama hiyo hiyo ya kumsaidia kupata hurumu ya wote tusiopenda Ukoloni mambo leo na ubeberu wa Wamagharibi. Ni usanii wa kisiasa.
Mimi nawapa changamoto wale wote mnaobisha kuwa Waafrika Ndivyo Tulivyo kunionyesha mifano ya Sivyo Tulivyo na nitatoa ya kwangu ya Ndivyo Tulivyo ili kulinganisha lipi ni zaidi. Nawahakikishia mkinionyesha mifano kumi ya Sivyo Tulivyo mimi nitawaonyesha mifano 10,000 ya Ndivyo Tulivyo. Haya kazi kwenu......let's go for it.
Hiki ni kichekesho. Ina maana Mugabe anafurahia kuongoza nchi iliyo na matatizo ya kiuchumi? Inamaana akina Mbeki, Mkapa na wengine ni wajinga kumkingia kifua Mugabe kwa vile tu analia waingereza-waingereza-waingereza? Naona mkuu stori za vyombo vya magharibi zimekushiba sana.
Hiki ni kichekesho. Ina maana Mugabe anafurahia kuongoza nchi iliyo na matatizo ya kiuchumi? Inamaana akina Mbeki, Mkapa na wengine ni wajinga kumkingia kifua Mugabe kwa vile tu analia waingereza-waingereza-waingereza? Naona mkuu stori za vyombo vya magharibi zimekushiba sana.
Na hiki nacho ni kichekesho.
Mugabe angekuwa hapendi kuona moto wa kiuchumi unaowakuta Wananchi wake angeendeleza uhuni uliopelekea Zimbabwe kuwa mafukara wa kuchapwa viboko wasio na mfano?
Mbeki -anaeiambia Africa kwamba AIDS hailetwi na HIV ila ni Wazungu wanatuongopea- na Mkapa - ambae wakati anajaza fomu za kuandikisha kampuni alipokutana na swali "mahala pa biashara," akajaza "Ikulu," hao watu unaweza kuwatumia kama mifano ya watu waliotulia vichwani hao?
Nikiogopa kukemea uhuni wa utawala wa Zimbabwe eti kwa vile Mbeki na Mugabe wataniita kibaraka wa Magharibi nitakuwa nimekubali waninyweshe maji yao ya sharbati. Mugabe ni fidhuli.
Kwani wewe mpaka leo hujajua kwamba Mbeki na Mkapa ni wajinga sana kuendelea kufumbia macho matatizo yaliyo wazi kwa sababu za uswahiba? Ndio wenzake ANC wamemtimua na anahesabu siku tu akapumzike.
Ngabu,
Mimi nakubaliana nawe kuwa waafrika ndivyo tulivyo. Watu kama Mugabe ndio wanathibitisha kabisa hili.
Sio kweli kuwa wamefumbia macho, in contrast ni kuwa wameyahangaikia sana lakini kwa vile MDC instruction zao zinatokea UK n.k., inakuwa vigumu kufikia compromise ya kiafrika ambayo inajumlisha kusameheana. Waingereza wanachotaka ni kichwa tu cha Mugabe kama ilivyokuwa kwa Sadaam na Millosevic.
........freedom Is Coming Tomorrow....!
Lets Open Our Brothers & Sisters Konshas About Freedom.....from Oppression, Corruption, Invasion, Inferiority Complex.....!
Waafrika ndio tulivyo ina maana gani?
KJ,
hapa msee umeteleza, yaani unataka ku-side na watu waajabu kabisa!! ktk watu woote wewe umeona Mkapa na Mbeki!!? Mbeki bado ana-hangover ya lile saga lake la ARV's, sijui anataka ku-prove point gani!! huyu Mkapa anajua kabisa, kwamba kama Jongwe akichukuliwa hatua basi kutakuwa na precedence ya kudili na watu mafisadi kama yeye!!
mwisho wa siku...!!! kazi kwako kubwajinga, uzalendo unamipaka kaka, oooohooo. Hii issue ni simpo, soln(s) zipo wazi, hakuna miujiza, Mugabe gotta go!!! hivi kwenye first round si alishapewa "pink slip," sasa nini tena??
Wewe kama hujui hadi hivi sasa maana ya Waafrika Ndivyo Tulivyo basi ndio unazidi kunithiubitishia kuwa kweli ni Ndivyo Tulivyo!!
Kama unakubalian na misemo ya kumwonyesha kuwa mwafrika ni duni kiutendaji, kiuamuzi n.k., na kuwa habadiliki basi ujue kuwa wewe uko katika hali mbaya sana kifikra, na utaendelea kutawaliwa mpaka utakapodondoka.
...halafu kusema vyombo vya Magharibi this or that, haisadii kupata ufumbuzi wa tatizo la Zimbabwe!! hakuna mchawi hapa zaidi ya Mugabe mwenyewe.....puliz!