Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

MtuMungu,
Haya yanayotokea Zimbabwe unashangaa kitu gani hali yameshatoikea Tanzania..Mara umesha sahau ya Pemba na ule uchaguzi mdogo vijana wa Chadema walikipata cha mtema kuni!...au kwa sababu hawa ni CCM wajomba zetu, mama zetu na baba zetu?

Pengine yaliyokwisha tokea sii kwa kwa kiwango cha Zimbabwe lakini hakuna geni kabisa kwa nchi zetu -Yanatokea ktk nchi karibu zote za Kiafrika.. Mkuu -Ndivyo tulivyo, ajabu tunashangaa leo ya Zimbabwe hali sisi wenyewe tayari tumeisha weka maji kichwani...ZANU PF haina tofauti kabisa na CCM ktk swala la kura na nadhani katika malengo ya chama cha CCM ushindi wa kura ndio umepewa kipaumbele katika katiba yao.. Ushindi ni lazima..

Mimi nafikir mada hii ilikuwa inazungumzia zaidi kuhusika kwa wazungu na propaganda zao dhidi ya Mugabe na kwamba wanajaribu kila njia kuepusha ukweli kuwa wao ndio kichombezo kikubwa cha maafa yote..
Fundi mchundo,
Mkuu ile habari ulosema hapo nyuma nadhani hukuelewa kwamba mfanyabiashara unayemzungumzia ni Mimi mwenyewe! Mimi ndiye nilikwqenda bank kujaribu kunua kitu Zimbabwe na kikampuni changu uchwara. Nilikataliwa na maelezo ya mhudumu wa bank alisema Zimbabwe ipo ktk sanction sasa wewe unachotaka kusema bila kuonyesha jinsi wewe ulivyojaribu na kufanikiwa ni maneno ya mgahawani...
Werwe kama upo nje iwe Marekani ama Uingereza naokuomba nenda bank yako na wambie unataka kufanya kununua kitu Zimbabwe ambacho unahitaji kutuma hizo fedha kwa kampuni X... kihsa sikia majibu yao.
Halafu swala la Pamba ni jamaa yangu kabisa anayeshughulika na ununuzi wa Pamba Zimbabwe hivyo huwezi kunambia kitu ambacho binafsi nakifahamu vizuri..
Mugabe ni kiongozi mbaya kama alivyokuwa Saadam hHussein na alitakiwa kuondolewa lakini inapotumika swala la WMD kuwa ndio sababu ya uabya wake hapo ndipo napopinga mimi na kusema hawa wazungu washenzi tu. Mugabe ana ubaya wake lakini mengi wanayoyafanya hayamuumizi Mugabe isipokuwa wananchi wa Zimbabwe kama walivyoumia Wa Iran enzi zile walipowekewa vikwazo.. Kama wanavyoumia Wa Cuba kwa sababu tu wao ni Wajamaa!... Cuba hata sikui moja haijawahi kuitishia Marekani kiuchumi wala kisiasa na kusema kweli sioni kabisa sababu ya kuwawekea vikwazo...wanaoumia ni wananchi sio Castrol na utawala wake...
Hii ndio point yangu na hakuna mahala nimempongeza Mugabe kwa ubabe wake wala sinyta mpongeza Morgan kwa kutumiwa na hawa wazungu...
Mwisho, maamuzi yangu yote yametazama Zimbabwe ya kesho baada ya Mugabe na hakika kama Morgan atakuja kuchukua nchio basi tumejivunmia Somalia nyingine!...
Mtakuja nambia.....nakomea hapo ktk mjadala huu..
 
Haya yanayotokea Zimbabwe unashangaa kitu gani hali yameshatoikea Tanzania.. Pengine sio kwa kiwango hicho lakini yanatokea ktk nchi karibu zote za Kiafrika.. mkuu Ndivyo tulivyo na ajabu tunashangaa leo ya Zimbabwe hali sisi wenyewe tayari tumeisha weka maji kichwani...ZANU PF haina tofauti kabisa na CCM ktk swala la kura na nadhani katika malengo ya chama cha CCM ushindi wa kura ndio umepewa kipaumbele katika katiba yao.. Ushindi ni lazima..

Mkuu Bob,

Weka darasa sijui ni kwa nini hawa the Nkurumah hawaelewi kuwa usafi unatakiwa kuanzia nyumbani kwako, ama sivyo utaenda kuambukiza uchafu wako huko kwenye nchi za watu! Hivi hawa watu tuwaambie lugha gani ili waelewe kuwa usafi unatakiwa kuanzia hapa bongo?
 
Hivi una maana gani unaposema Marekani inamilikiwa na mchina na mjapani ?

Benki zote!
Na sasa biashara zote za uzalishaji!
Na pia hivi vita vya IRAQI MMAREKANI ANAKOPA MABILIONI KWA MCHINA!
MAREKANI ANADAIWA NA MCHINA PESA AMBAZO MCHINA AKIZIDAI KWA NGUVU KAMA MMAREKANI AKIJIDAI KICHWA NGUMU THEN HAKUTAKALIKA!
MMAREKANI HATHUBUTU HATA SIKU MOJA KUPAMBANA NA MCHINA!
WE UNAFIKIRI MUGABE NI MJINGA ALIPOMKIMBILIA HU JINTAO?
ALI COUNTER BALANCE NA NDIO MAANA ANA CONFIDENCE!
TUMESHAPAMBANA NA AFRIKA HAWATAKI HIVYO VITA!
HIVYO BUSH ANATAPATAPA KWANI NI MKATABA WALIOSAINIANA NA BLAIR NA SASA HAWEZI KUUTIMIZA!
OPTION YAO YA MWISHO NI KUMPA TSIVANGIRAI SILAHA.
 
Benki zote!
Na sasa biashara zote za uzalishaji!
Na pia hivi vita vya IRAQI MMAREKANI ANAKOPA MABILIONI KWA MCHINA!
MAREKANI ANADAIWA NA MCHINA PESA AMBAZO MCHINA AKIZIDAI KWA NGUVU KAMA MMAREKANI AKIJIDAI KICHWA NGUMU THEN HAKUTAKALIKA!
MMAREKANI HATHUBUTU HATA SIKU MOJA KUPAMBANA NA MCHINA!
WE UNAFIKIRI MUGABE NI MJINGA ALIPOMKIMBILIA HU JINTAO?
ALI COUNTER BALANCE NA NDIO MAANA ANA CONFIDENCE!
TUMESHAPAMBANA NA AFRIKA HAWATAKI HIVYO VITA!
HIVYO BUSH ANATAPATAPA KWANI NI MKATABA WALIOSAINIANA NA BLAIR NA SASA HAWEZI KUUTIMIZA!
OPTION YAO YA MWISHO NI KUMPA TSIVANGIRAI SILAHA.

Unajua nilikuwa nikujibu ila nimegundua itakuwa wastage of time , Mushi nasikitika kusema ya kuwa uwezo bado ni mdogo sana katika masuala ya siasa na ulimwengu kwa ujumla . Mambo mengi unayoyazungumza ni ya vijiweni ....

Mada zako nyingi zimejaa pupa na wala azionyeshi reasoning ya aina yoyote.
 
Mkuu ile habari ulosema hapo nyuma nadhani hukuelewa kwamba mfanyabiashara unayemzungumzia ni Mimi mwenyewe! Mimi ndiye nilikwqenda bank kujaribu kunua kitu Zimbabwe na kikampuni changu uchwara. Nilikataliwa na maelezo ya mhudumu wa bank alisema Zimbabwe ipo ktk sanction sasa wewe unachotaka kusema bila kuonyesha jinsi wewe ulivyojaribu na kufanikiwa ni maneno ya mgahawani...

Mkandara!
Nimekuelewa sana lakini bado naona mimi na wewe tunaongea lugha tofauti. Tamko la mhudumu wa benki au rafiki yako, with all due respects, sio official statement ya serikali. Ungeniambia ulifuatilia kwenye idara ya biashara ya serikali ukaambiwa hivyo ningekuelewa. Unasema maneno yangu ni ya mghahawani wakati nimekuweka website ya SERIKALI ya Marekani ikielezea ni sanction za aina gani zinazozungumziwa! Wewe mwenzangu unanijia na personal experience (ambayo siwezi kuthibitisha) na taarifa kutoka shirika la habari likitoa anecdotal kuhusu kukuta bidhaa kutoka Marekani katika mduka Cuba ( nyingine zikiwa fakes) ! sasa anayeleta hadithi za kinyozi nani?

Hofu yako ya kuwa akiondoka Mugabe patatokea chaos ina merit. Lakini iko based kwenye statements za Mugabe na maswahiba wake. Hata wakina Marcos waliamini hivyo lakini hao askari wao wa kawaida walipokuwa faced na choice ya all out war against their own people they blinked! Mugabe atavuna alichopanda. Iwe leo au kesho. Lakini asiruhusiwe azame na Zimbabwe kama anavyotaka. He is evil. Watu kama yeye hawastahili sympathy. No way! Hatuwezi kumkumbatia kwa ati Zimbabwe itageuka Somalia. Kwa mtazamo huo basi Charles Taylor angekuwa bado rais Liberia.
 
Wakuu,

Katika hoja zetu zoote hatujamjadili raisi Thabo Mbeki.

Kuna taarifa kwamba ile meli ya kutoka China ilipotia nanga pale Durban, Mbeki alitoa agizo kwamba vile vifaa vya kijeshi vipakuliwe na shughuli hio ikafanyika bila kupingwa.

Kuna mwenye data zingine.
 
Maneno ya Niemöller kwa wale wanaosema charity begins at home:

When the Nazis came for the communists,
I remained silent;
I was not a communist.

When they locked up the social democrats,
I remained silent;
I was not a social democrat.

When they came for the trade unionists,
I did not speak out;
I was not a trade unionist.

When they came for the Jews,
I remained silent;
I wasn't a Jew.

When they came for me,
there was no one left to speak out.
 
Wakuu,

Katika hoja zetu zoote hatujamjadili raisi Thabo Mbeki.

Kuna taarifa kwamba ile meli ya kutoka China ilipotia nanga pale Durban, Mbeki alitoa agizo kwamba vile vifaa vya kijeshi vipakuliwe na shughuli hio ikafanyika bila kupingwa.

Kuna mwenye data zingine.

Thabo is a joke.
Wafanyakazi wa bandari waligoma kuipakuwa meli ikaenda kushusha mzigo Angola!
 
Hii taarifa ni kutoka katika moja ya invetigative journals.

durban_3_318657a.jpg
Meli ya mizigo bandarini Durban.

Summary of documents showing an arms shipment from China to Harare

The file below contains 4 scanned documents in PDF form, presenting information on a recent chinese weapons shipment to Zimbabwe. The documents are dated between January 21st and 10th of March 2008.
Document 1 holds an arrival notification for the Ministry of Defence in Zimbabwe related to 77 tons of Arms shipped in 3080 cases from a shipper Poly Technologies (INC). Document 2 presents the commercial invoice from Poly Technologies related to that shipment, detailing a purchase of 3,004,755 rounds of different ammunition, from 7.62 shells to mortar bombs. Document 3 holds the Packing List for this shipment. Document 4, while being in very bad quality holds another confirmation of the shipment in form of the Bill Of Lading.

View attachment zimbabwe_arms.pdf

Ndio kama hivyo, ikiwa imeshushwa Angola itakuwa kwa mbinu gani?
 
Jana Mandela, ametoa maneno mazito sana kumsema Mugabe kwa mara ya kwanza, lakini ninashangaa kuwa kwa nini ameenda kuyasemea majuu badala ya Afrika, tena akiwa amezungukwa na wazungu why? Wakuu naomba kueleweshwa?

Mkuu Thabo Mbeki, nasikia Muagbe anamuita ni play boy, na kwamba anamdharau sana kuwa ni kibaraka wa wazungu na ameshamwabia hivyo mara nyingi usoni kwake, na pia nasikia na sisi bongo anatuona ni a big joke hasa baada ya Joji Kichaka kuja kwetu, nasikia anatudharau sana,

Hapa ndio tunamkumbuka Mwalimu, yule mzee alikuwa na something sijui ni kile kifimbo au tunguli, maana angekwenda kwa huyu Mugabe na angemshikisha adabu, muulize Buyoya wa Burundi!
 
Vikwazo ni TACTICS ZA KUI ISOLATE SERIKALI NA WATU WAKE! KAMA SI SANCTIONS...BASI MUGABE ANGEWEZA KUSHINDA USHINDI WA TSUNAMI! KUNA NJIA YA KUUSHUGHULIKIA MGOGORO HUU LAKINI OPTION SI KUFANYA WANACHOTAKA BUSH NA BLAIR. BUSH NA BLAIR WALISHAKUBALIANA KITAMBO TU ON IRAQ AND ZIMBABWE AS IN SADDAM AND MUGABE. WASIWAPANGIE WAAFRIKA CHA KUFANYA KWANI MATOKEO YAKE HAYATAMNUFAISHA MWAFRIKA BALI MKOLONI.

Ndugu yangu Mushi, hivi uchaguzi wa Zimbabwe ulipangwa na UK na US? Kama uchaguzi ulikuwa kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe na wapiga kura walikuwa ni Wazimbabwe wenyewe ni kwa nini walaumiwe UK na US? Kama kweli Mugabe alikuwa na nia ya dhati kuwa na uchaguzi huru na wa haki, ni kwa nini aue watu waliopiga kura kumkataa?

Watu wa Zimbabwe wanaijua hali ya Zimbabwe kuliko wapiga debe wa Mugabe wasio Wazimbabwe na ndio maana walipiga kura ya kumkataa Mugabe na kumkataa na kumtaka Morgan awe rais wao. Wazimbabwe sio wajinga kumpigia kura Morgan eti kwa sababu tu amewekwa na UK na US. Kama Morgan angekuwa na madaraka serikalini tungefikiri kuwa labda aliwahonga Wazimbabwe na ndio maana alipigiwa kura ya kukubaliwa, lakini hivyo sivyo. Mimi ninaamini kuwa Wazimbabwe walimpigia kura Morgani kwa sababu waliona kuwa ni kiongozi bora kuliko Mugabe na si kwa sababu ya madai kuwa ni kibaraka wa UK na US.
 
Jana Mandela, ametoa maneno mazito sana kumsema Mugabe kwa mara ya kwanza, lakini ninashangaa kuwa kwa nini ameenda kuyasemea majuu badala ya Afrika, tena akiwa amezungukwa na wazungu why? Wakuu naomba kueleweshwa?

Mkuu Thabo Mbeki, nasikia Muagbe anamuita ni play boy, na kwamba anamdharau sana kuwa ni kibaraka wa wazungu na ameshamwabia hivyo mara nyingi usoni kwake, na pia nasikia na sisi bongo anatuona ni a big joke hasa baada ya Joji Kichaka kuja kwetu, nasikia anatudharau sana,

Hapa ndio tunamkumbuka Mwalimu, yule mzee alikuwa na something sijui ni kile kifimbo au tunguli, maana angekwenda kwa huyu Mugabe na angemshikisha adabu, muulize Buyoya wa Burundi!

Mkuu wazungu wanapenda jambo hili.

Wametumia opportunity hii katika kujaribu kumkandamiza zaidi Mugabe.

Mandela nafikiri jana hakuwa na taarifa yoyote ya kwamba atazungumzia suala la Zimbabwe.

Ni katikati ya hotuba yake iliohusu mambo mengine kabisa ndio akapenyezewa kikaratasi ambacho kilikuwa na maneno machache sana kwamba the situation in Zimbabwe shows a "tragic failure of leadership".

Alipomaliza kusoma hicho kikaratasi, basi akaendela na mambo mengine.

Kwa hio uelewe tu kwamba aliandikiwa un-official kikaratasi na yeye kama mgeni wa waingereza akakisoma.
 
Unajua nilikuwa nikujibu ila nimegundua itakuwa wastage of time , Mushi nasikitika kusema ya kuwa uwezo bado ni mdogo sana katika masuala ya siasa na ulimwengu kwa ujumla . Mambo mengi unayoyazungumza ni ya vijiweni ....

Mada zako nyingi zimejaa pupa na wala azionyeshi reasoning ya aina yoyote.

Kuhusu mabenki ya marekani kumilikiwa na JAPAN NA CHINESE?
Uwezo mdogo?
MAJOR YANGU BUSINESS NA NIKO FIT KWENYE WORLD HISTORY!

MAHESABU KESHATOA FORMULA YA WAZALENDO.

KUNGURU MWEUPE KESHAKUPA SOMO...NA WEMBE MKALI ANAYACHANJA MAKALIO YENU NYIE VIBARAKA!

UNASOUND KAMA HUNA AKILI NA HUKU UKIBASE KWENYE PERSONAL ATTACKS FOR INTIMIDATION PURPOSES!

SIJAJA HAPA JF KUTAFUTA SIFA AMA UMWAMBA!

ILA RESOLVE YANGU WHEN I HAPPEN TO BELIEVE IN A CAUSE...NEVER EVER WAVER!

WALISHANIANZISHIA HADI THREADS NA WEWE UNATAKA NINI?
 
Fundi Mchundo,
Imebidi nirudi tena kukufahamisha kile nilichokuwa nikisema toka mwanzo... Kuwa sanctions zote ni siasa za Biashara!.. toka mwanzo nimelisema hili sijui unatazama wapi mkuu... hukutaka kunielewa bali kila wakati huongeza maswali tu kwa kila nilichoandika badala ya kutazama the big picture.
Ni hivi pamoja na kwamba vikwazo vinajieleza wazi katika nchi tofauti ukweli wa hali halisi sivyo kama ilivyoandikwa...Hizi ni siasa za nchi za magharibi siku zote..
Nikatoa mfano wa Cuba, Iran na kadhalika.. hata Mugabe kuwepo New York na majuzi Italia bado hukujibu kitu ila kutafuta njia ya kutokea.. Sheria zinasema tofauti na vile vinavyoendelea humo. Vitu vinaingia pamoja na vikwazo vyote as a fact Canada wapo wafanya biashara wamewekesha Cuba na dunia haitambui kisheria ushirikiano kama huo ambao upo..best destination ya Wa -Canada ktk tourism ni Cuba.. na kwa mwaka mmoja tu Cuba inapata zaidi ya watalii 500,000 toka North America peke yake... hawa wote wanaingia Marekani na kutoka bila kufuata hizo sheria za sanction unazozizungumzia. Cigar za Cuba hadi kesho zinaingia Marekani kinyume cha sheria hizo unazozungumzia...Hii ndio hali halisi mkuu, sio kilichoandikwa.

Kitu kingine labda nikwambie tena kuwa kama wewe ni Muislaam na jina lako lina majina yote matatu ya Kiarabu basi mkuu huwezi kutuma fedha hata iwe Africa kirahisi fedha hizo zinarudishwa! Je, ipo sheria ya namna hiyo!.. Mimi nafikiria tunachozungumza hapa ni kile kinachotendeka na sio sheria! Mugabe anayoyafanya sidhani kama yamo ktk katiba ya Zimbabwe ama yanatambuliwa kisheria!..tunachozungumzia ni ubabe wa Mugabe na huo wa wazungu hasa Waingereza..na binafsi nafikiria hofu yao kubwa ni MCHINA ambaye anaingia Afrika kwa kasi ya ajabu.
Mugabe kasimamiwa na wahuni ambao hawajali sheria inasema nini! wao upinzani hukumu yake ni kifo tu yaani unauza nchi.. Huu ni uharamia kama alioufanya Saadam Hussein wakati wale Ma Qurdish walipotumiwa na Marekani...Na siku Saadam alipokianzisha kwa hao Qurdish - Wamarekani waliingia mitini, waliwaacha Qurdish ktk mataa wakauawa kama ndama. hiki ndicho nachozungumzia kuwa wazungu wanafiki, washenzi na siku zote watu kama Morgan ambao wanataka kubebwa na mzungu ni hatari sana...

Leo hii Iraq nchi nzima wanalipa kosa la uongozi wa Saadam as a fact sababu kubwa ni Marekani na uongoi wa Bush hata kama tunaweza kusema Saadam was brutal and he had to go!.Hii ndio hofu yangu kubwa na nawaomba tujihadhali nayo zaidi ktk kila tunapojaribu kulitazama swala la Zimbabwe!
Sheria zilizoandikwa kuhusiana na Zimbabwe ni kama ulivyozieleza na kama unakumbuka niliwahi kuyasema haya toka mwaka 2004 ktk ubishi kama huu...Na nyie kwa kutofikiria mnakubali kabisa kwamba Wa - Zimbabwe hawajui kulima isipokuwa mzungu..Na inazidi kunishangaza unapotumia vigezo zvizito kama Utaalam wa ujenzi wa nyumba ktk kilimo ambacho ni jadi ya Mbantu. yaani wazungu ndio wametufundisha kweli kulima ati wao ni architectures wa ukulima!..kiasi kwamba Wazimbabwe washindwe kujua la kufanya hata chakula chao wenyewe washindwe kulima!..
Pengine msichoweza kufahamu ni impact ya kufungiwa kiuchumi, wazungu ni zuga wakubwa sana inapofikia maslahi ya nchi zao ama haki ya mwafrika..

Well, nitarudia kusema kwamba siwezi kuendelea kubishana..kwani nakumbuka wakati wa kuivamia Iraq nilisema wazi ktk kijiwe hiki (Bcstimes) kuwa Marekani wamevamia nchi hiyo kwa sababu ya Mafuta (OIL)mkanibishia sana na kusema yote mabaya ya Saadam including WMD kama ndio sababu kubwa..lakini mkashindwa kuelewa kwamba sikubisha kabisa mabaya ya Saadam isipokuwa kuwashutumu Westerners ktk hatma ya Iraq ni ukweli usiofichika!..
Leo tena najikuta ktk mjadala kama ule ule ambao baada ya miaka mtakuja kaa kimyaaaa msikubali makosa yenu ya kutoona mbali.
 
Kuhusu mabenki ya marekani kumilikiwa na JAPAN NA CHINESE?
Uwezo mdogo?
MAJOR YANGU BUSINESS NA NIKO FIT KWENYE WORLD HISTORY!

MAHESABU KESHATOA FORMULA YA WAZALENDO.

KUNGURU MWEUPE KESHAKUPA SOMO...NA WEMBE MKALI ANAYACHANJA MAKALIO YENU NYIE VIBARAKA!

UNASOUND KAMA HUNA AKILI NA HUKU UKIBASE KWENYE PERSONAL ATTACKS FOR INTIMIDATION PURPOSES!

SIJAJA HAPA JF KUTAFUTA SIFA AMA UMWAMBA!

ILA RESOLVE YANGU WHEN I HAPPEN TO BELIEVE IN A CAUSE...NEVER EVER WAVER!

WALISHANIANZISHIA HADI THREADS NA WEWE UNATAKA NINI?



Kwa hiyo wewe unaona kuanzishiwa thread ni sifa au ? Vitu unavyozungumza havina vichwa wala miguu . Hata argument zako ni za kitoto , mimi naona unaharibu mtiririko tuu wa mada hapa . Unasema major yako ni ya biashara , Hivi unajua kitu chochote kuhusu free market ?

Mtu unaandikaje kitu halafu unajijibu mwenyewe ...
 
Mimi naamini kuwa viongozi wengi wa Afrika ni vibaraka wa wazungu...wakishapata kiti wanatafuta kila njia ili wapewe blessing toka kwa hawa wazungu...Na hiki ndiko kilichotokea kwa Mugabe, he was their poodle wakamsifia hadi na kumpa chibuku wenyewe wanaita knighthood.

Hawa weupe ikafika wakati wakamwona kuwa Mugabe amekuwa liability kwao, basi wakamtema...na hili ndio tatizo letu waafrika, kukaa kuwanyenyekea hawa wazungu...namsifu sana mzee wetu JKN kwa vile alikuwa ana guts.

Sasa tusiwalaumu hawa weupe, kwa vile kila mwafrika anajua kuwa hawa ni maharamia, mimi naona tujilaumu sisi ambao hatuna uamuzi wowote ule mpaka tuamrishwe na hawa cowboys.....hamuoni kuwa ni ajabu? Zimbwabwe iko katika hali mbaya kisiasa na uchumi kwa muda mrefu halafu ghafla sasa poodles wachache wa kiafrika wanajitokeza na kuanza ati kukemea na kuzungumzia?...walikuwa wapi wakati wa machafuko huko Rwanda?Darfour? au Somalia?...au kwa vile huko weupe hawana maslahi?

Ni kweli Mugabe ameharibu uchumi wa Zimbwabwe na kama kumkemea Mugabe ilibidi ianze siku nyingi....lakini ukiangalia na upande mwingine, ni vizuri hawa poodles wanakemea ya Mugabe ili nao wakija kufanya makosa waje wakemewe.

Kitu moja muhimu ieleweke kuwa bara letu ni keki ya wanaojiita first world...wanakaa wanaamua tu we Mchina nenda Darfour, we Mfaransa nenda Congo...walifanya hivyo wakati wa ukoloni na wanaendelea na wataendelea kufanya hivyo na viongozi wetu wanajua hivyo...lakini kwa sababu ya ubinafsi wao, wako radhi kutekeleza.

Ndio maana mara nyingine nakubaliana na Nyani Ngabu kuwa WAAFRIKA NDIYO TULIVYO.......zamani tulilamikia ukoloni....ikaja tukalalamika ati hatuna usomi...je sasa tulalamike nini?..kama ukoloni umekwisha kama wasomi tunao wenye madigrii mengi tu.....Kwa hiyo lini tutafika na kuacha kulalamika na kujivunia cha kwetu?
 
Mwanatanu,
Mifano ni mingi sana yaani hata haina idadi... tazama kina Mobutu wa Zaire...walisifiwa sana, Lumumba akapewa matusi yote hata kabla hajatawala..Wazungu walipomchoka Mobutu ndipo kila mwafrika alipomwona ubaya wake.. Baada ya mzungu kusema! na wakaingizwa mjini bila kufahamu kwamba hatua watakazo chukua dhidi ya Mobutu zitakuja kuwaangamiza zaidi..

Ndio maana nawauliza Waingereza ilikuwaje kwa miaka 17 Mugabe alikuwa kiongozi shujaa na kapewa sifa zote! Tazama kina Mubarak huyu katawala toka Zimbabwe haijapata Uhuru wake hadi leo anapeta pamoja na kwamba kairudisha Egypt nyuma kishenzi nchi imegeuka kuwa na Utawala wa Kijeshi na Kidikteta wanakufa watu kila siku hakuna anayesema kitu sii Muingereza wala America, wapinzani wote wa Mubarak wanaitwa Terrorist pamoja na kwamba wamejiandikisha kisheria kama vyama vya Upinzani.
Kila kona ya Afrika mchezo ni huo huo na hakuna hata siku moja tumejifunza kutokana na yale yaliyotangulia.... Bila shaka nakubaliana na Nyani Ngabu -NDIVYO TULIVYO!
 
Yournameismine,



Umeona lakini lugha anayotumia huyo mtu unayemtetea , anaposema makalio yetu *************** unaona ni sawa tuu au ndio kukata ishu huko ?
 
Back
Top Bottom