Tatizo la wengi wetu ni bigotry na kukataa responsibility kwa matendo yetu. Tunaona mkono wa mtu mweupe hata pale ambapo sisi wenyewe ndiyo chanzo. Tunamlaumu mtu mweupe kwa kutuingilia mambo yetu na asipoingilia, tunamlaumu kwa kutoingilia. Tunatendeana unyama na ukatili usiofikirika ( DRC, Sudan, Sierra Leone, Ivory Coast, Liberia, Rwanda, Zimbabwe n.k.), anapotukemea mtu mweupe kwa kufanya hayo tunamwambia akae nje kwa sababu hatutakii memba. Tunapochoka kufanyiana ukatili huo au aibu inapotuingia, tunamlaumu mtu mweupe kwa kutotuzuia kuchinjana, kunyofoana viungo, kutoana utumbo nje, kuchomana tukiwa ngdani ya nyumba, kubaka vijukuu vyetu na matendo mengi ambayo tumefanyiana watu weusi kwa watu weusi! Mtu mweusi yeyote akishukiwa kwa kutenda uovu au makosa ya aina yeyote, kuanzia O.J, Michael Jackson, Wesley Snipes, Naomi Campbell hadi Robert Mugabe kimbilio lao la kwanza ni kuwa mnanituhumu kwa sababu mimi ni mtu mweusi. Hawa wote wanatambua weusi wao wakati wakiwa katika matatizo.
Leo wananchi wa Zimbabwe katika nchi inayotawaliwa kibabe na mmoja wetu walidiriki, katika mazingira hayo, kumpigia kura mpinzani wa Mugabe. Badala ya kuheshimu ushujaa na msimamo wao, leo tunawatuhumu kuwa wao hawana akili, ni lazima walishurutishwa na mtu mweupe! Mtu mweupe ambaye amenyang'anywa karibu kila kitu nchini humo bado tunamtafuta chini ya kitanda! Tunasahau kuwa yeyote anayempinga Mugabe anaitwa kibaraka wa watu weupe. Hakuanza na Morgan na bila shaka akitokea mwingine naye ataitwa kibaraka.
Humu ndani watu wamefikia hata kuwaita Mandela ( aliyefungwa miaka 27, aliyesimama kidede kutetea uhuru wa nchi yake hata alipokuwa anaangalia hukumu ya kifo) na Desmond Tutu ( ambaye chini ya utawala dhalimu wa makaburu hakuchelea wala kuogopa kupambana nao) vibaraka kwa sababu wamemkemea muuaji Mugabe! Vijana ambao hawastahili kufunga kmba za viatu za hawa wawili! Tusisahau kuwa Nyerere alimkemea Idi Amin kwa kuwafukuza wahindi. Aliita kitendo hicho ni ubaguzi. Leo angefanya hivyo, bila shaka hawa arm-chair revolutionaries wangemwita kibaraka wa watu weupe! Talk is cheap.
Mimi naamini kuwa mpaka hapo tutakapoweza kujitoa kwenye hii bigotry, tutaendelea kuwa na matatizo. Kumchukia mtu kwa sababu tu ndivyo alivyo si kwa watu weupe na wahindi tu. Unakuwa reflected katika jinsi tunavyoangaliana wenyewe kwa wenyewe( kuanzia mjaluo na mkikuyu, mpemba na muunguja, mhutu na mtusi n.k). Tunapokuwa tayari kutetea maovu ya yeyote ambaye tunafanana naye ki rangi, ni hatua fupi hadi hapo tunapofumbia macho maovu ya yeyote yule aliye kabila letu. Bigotry is a slippery slope. Badala ya kujiuliza kwa nini nchi za Asia pamoja na historia yao ( walikuwa maskini kuliko sisi tulipopata uhuru, walipigana vita za muda mrefu na mataifa ya magharibi n.k) leo wanatuacha mbali? Kuna taifa ambalo lina kila haki ya kumchukia mmarekani kama Vietnam? Mbona leo wanashirikiana nae kibiashara? Sisi tumebaki kulalama ( wengi tunaofanya hivyo tunaishi katika nchi za magharibi) na kudai kutokupendwa wakati wenzetu wanatuacha. Wakati umefika wa kumtambua kila aliyezaliwa na aliye na mapenzi na Afrika, bila kujali rangi yake, jinsia,dini yake au upuuzi mwingine kama huo, kuwa ni mwafrika. na kumtenga yeyote atakayemtendea maovu mtu yeyote anayeishi katika bara hili ( kuanzia anayemua bibi kizee Shinyanga hadi anayeangalia wakati wafuasi wake wanaua na kuwatesa raia zake) bila kujali rangi, kabila, jinsia, dini yake hata kama anayefanya hivyo tunafanana nae kwa njia yeyote! Wakati umefika ambapo yeyote atakayechangia kudumisha hali ya maisha ya watu wa Afrika akemewe na kutengwa bila kujali rangi yake, dini yake, jinsia yake n.k. Huyo si mwenzetu. Hastahili sympathy yetu. Wakati umefika wa kukubali mapungufu yetu bila kutumia kisingizio cha kutokupendwa.
Watu kama Mugabe ni lazima tuwatenge na kuwalani! Huyu anayesema amewanyang'anya ardhi watu weupe ( Ndabaningi Sithole naye mweupe?) ili kuwatendea haki watu weusi na badala yake kuwazawadia waovu wenzake! Huyu anayedai kuwa makampuni ya biashara ni lazima yawape asilimia kubwa ya hisa zao watu weusi! Guess who watakaopewa hizo hisa? Huyu aliyewachinja wandebele. Huyu aliyewabomolea makazi wakazi maskini wa Harare kwa sababu tu ya kuwa upande wa upinzani. Huyu anayedai ni Mungu pekee ndiye ana uwezo wa kumnyang'anya urais. Atakapotugeukia huku mikono yake ikitiririka damu na kudai atambuliwe kama kiongozi halali, inabidi watu wote ambao wana mapenzi ya dhati na watu wa Zimbabwe wamkatalie! Ni lazima aonyeshwe kuwa ni pyrrhic victory aliyoipata!
Amandla......!