Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Masanja,

Mkuu hapa tena umezungusha.. huu mbuyu hatuwezi kuumaliza..
nachosema mimi ni kuhusiana na Wazungu jinsi wanavyotumia siasa za Uchumi..
Ni hawa wazungu waliotujenga imani kubwa ya kile kilichotokea Sudan for their interest in OIL..lakini tazama basi walipopewa contract Sudan imesahauliwa kabisa!... Congo mauaji kila siku haizungumziwi kwa sababu ahdi leo machimbo ya nchi hiyo wanaingia kama kwao na askari wa kukodishwa toka Ulaya wamewekwa.. Sisi waafrika hatulitazami hilo na hakuna mada humu ndani inazungumzia Congo, Sudan, Somalia wala Chad leo hii. WHY? kwa sababu mzungu hajasema kitu tena, huyu ndiye kiongozi wa hizi propaganda ambaye nyinyi mnashindwa kumtazama machoni..Kesho Mugabe alikubali deal na mzungu akarudisha ardhi nina hakika nyie nyie mtakuwa wa kwanza kumfagilia kutokana na maneno ya mzungu na pengine hata kusahau mabaya ya Mugabe kama mnavyosahau ya Sudan na Congo.
Umezunguzia Bashir na utawala wake ebu nionyeshe mada ama hoja hata moja uloweza kumzungumzia hata siku moja!..kwa nini hujafanya hivyo?... kwa sababu mzungu hajasema tena wala kuifanya issue. Leo unakuja hapa na kuonyesha kuwajali Wasudan kwa maneno yale yale yaliyosemwa na mzungu kama vile tunasoma biblia hapa.
Mkuu twende na hoja iliyopo hapa na useme ukweli wako kuwa mzungu anahusika ktk matatizo ya Zimbabwe, nje ya hapo unazuga tu... yaani aibu hata kusema mzungu anahusika na matatizo ya Zimbabwe mdomo umeshika ganzi jamani!
duh ama kweli safari ni ndefu..
 
Wale wanaomtetea KICHAKA NA BLAIR NINA MASWALI KADHAA TU!
MKINIJIBU HAYA...THEN TUTAENDELEA NA MJADALA...
1)JE NI WATU WANGAPI ZIMBABWE WANAOISHI VIBANDANI NA HAWANA ARDHI?
2)JE INGEKUWA NI MWEUSI KAPORWA ARDHI WANGEKASIRIKA?
3)JE HUKO SUDAN WAMEPORWA NINI?

MUGABE HAJAUA MZUNGU...JE KUNA WAAFRIKA WANAKUFA? AMA KUUWAWA?
KUNA MTU ANA TAKWIMU YA WAAFRIKA WANAOKUFA KILA SIKU AMA AMA WASIO NA ARDHI YA KULIMA ILI KUPATA CHAKULA?
JE MWAFRIKA ANASTAHILI KUMILIKI ARDHI YAKE?
AMA NI MZUNGU TU?
 
Fundi Mchundo,Masanja,Koba,Kuhani Mkuu,Kitila Mkumbo,Mkandara,....

..naomba kuwauliza maswali yafuatayo wachangiaji wa mjadala huu.

..ni sera zipi za Mugabe ambazo zinasababisha inflation iwe kubwa kiasi kile?

..najua kwamba wana-print pesa kama wajinga, lakini why do they have to do it in the first place?

..vilevile ninavyoelewa mimi, in Mugabe's watch uchumi wa Zimbabwe ulipata kukua hata by double digits. what was he doing right? what is he doing wrong now?

..zaidi kuna yeyote anayefahamu sera za Morgan Tsivangarai ambazo zitaondoa hii inflation?

..pia Tsivangarai ana sera au mipango gani ya kupambana na njaa ya muda mrefu Zimbabwe?

..je Tsivangarai atarudisha ardhi kwa wazungu? kama atarudisha si kutakuwa na vita? na asiporudisha njaa itakwisha kweli? inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.
 
Sasa hivi naanza kuelewa kwanini JK anaogopa kutengua mikataba ya madini na ubinafsishaji uliotufikisha hapa tulipo. Naamini sio kwa sababu haimuumizi, isipokuwa njaa za watu wetu, uroho wa madaraka na umaskini wa akili ni silaha tosha ambayo JK anaweza kusulubiwa peke yake kwa maamuzi anayoweza kufanya kwa niaba ya taifa.

Amini nawaambia, matatizo yetu ndani ya Bongo yakiwekwa kwenye luninga za BBC na kuelezea uovu wa CCM dhidi ya wananchi maskini, bila shaka Zimbabwe bado itakuwa mbingu kama tunafananisha na mashaka ya watanzania ambayo si wengi tunayafahamu ingawa tunajiita watanzania.

Amini nawaambia, Mugabe ni sehemu ndogo sana ya tatizo la Zimbabwe, kubwa ni vikwazo vya uchumi ambavyo hata Saddam pamoja na mafuta yake hakuweza kuvihimili; na hakuna nchi ambayo hata kama wangekuwa na demokrasia kiasi gani na sera nzuri kupindukia, kwenye vikwazo uchumi, nchi hiyo itafukarishwa na njaa itakayotengezwa na vikwazo hivyo, inaweza kabisa kutengeneza wavunja sheria ambao wakiguswa na vyombo vya usalama wanageuka wapinzani.

Picha hii tunayoiona Zimbabwe ni ishara tosha ya nini kinaweza kumkumba JK pindi atachukua hatua madhubuti kuhakikisha watanzania wanapata chao cha halali. Swali je tutakubaliana kusimama naye na kumuunga mkono, au tutaitikia kibwagizo cha wenye maslahi yao kuwa JK anakiuka haki za binadamu, mpinga demokrasia na chanzo cha mateso ya watanzania, mateso ambayo hao hao watakaompinga kesho hawayaoni kwa sasa kwa sababu ya kufaidika na mikataba ya kishenzi?

Swali la kutafakari, leo hii bajeti yetu inategemea wafadhili kwa asilimia 42, hatuna vikwazo vya biashara, embu tujiangalie tulipo. Halafu jiulize, kama Tanzania ingekuwa Zimbabwe, kwa miaka hii minane hakuna vijisenti vya mfadhili vinavyodondoka kwenye bajeti huku uchumi ukichagizwa na vikwazo vya kiuchumi, je ni sera zipi za uchumi na busara gani ya kisiasa zaidi ya kuwa mtumwa zingeweza kuisadia nchi kupambana na madhara ambayo wenzetu wamekutwa nayo?
 
Sasa hivi naanza kuelewa kwanini JK anaogopa kutengua mikataba ya madini na ubinafsishaji uliotufikisha hapa tulipo. Naamini sio kwa sababu haimuumizi, isipokuwa njaa za watu wetu, uroho wa madaraka na umaskini wa akili ni silaha tosha ambayo JK anaweza kusulubiwa peke yake kwa maamuzi anayoweza kufanya kwa niaba ya taifa.

Amini nawaambia, matatizo yetu ndani ya Bongo yakiwekwa kwenye luninga za BBC na kuelezea uovu wa CCM dhidi ya wananchi maskini, bila shaka Zimbabwe bado itakuwa mbingu kama tunafananisha na mashaka ya watanzania ambayo si wengi tunayafahamu ingawa tunajiita watanzania.

Amini nawaambia, Mugabe ni sehemu ndogo sana ya tatizo la Zimbabwe, kubwa ni vikwazo vya uchumi ambavyo hata Saddam pamoja na mafuta yake hakuweza kuvihimili; na hakuna nchi ambayo hata kama wangekuwa na demokrasia kiasi gani na sera nzuri kupindukia, kwenye vikwazo uchumi, nchi hiyo itafukarishwa na njaa itakayotengezwa na vikwazo hivyo, inaweza kabisa kutengeneza wavunja sheria ambao wakiguswa na vyombo vya usalama wanageuka wapinzani.

Picha hii tunayoiona Zimbabwe ni ishara tosha ya nini kinaweza kumkumba JK pindi atachukua hatua madhubuti kuhakikisha watanzania wanapata chao cha halali. Swali je tutakubaliana kusimama naye na kumuunga mkono, au tutaitikia kibwagizo cha wenye maslahi yao kuwa JK anakiuka haki za binadamu, mpinga demokrasia na chanzo cha mateso ya watanzania, mateso ambayo hao hao watakaompinga kesho hawayaoni kwa sasa kwa sababu ya kufaidika na mikataba ya kishenzi?

Swali la kutafakari, leo hii bajeti yetu inategemea wafadhili kwa asilimia 42, hatuna vikwazo vya biashara, embu tujiangalie tulipo. Halafu jiulize, kama Tanzania ingekuwa Zimbabwe, kwa miaka hii minane hakuna vijisenti vya mfadhili vinavyodondoka kwenye bajeti huku uchumi ukichagizwa na vikwazo vya kiuchumi, je ni sera zipi za uchumi na busara gani ya kisiasa zaidi ya kuwa mtumwa zingeweza kuisadia nchi kupambana na madhara ambayo wenzetu wamekutwa nayo?

Kama hawajui Psychology SHAURI YAO!
Njaa ni TATIZO LA KISAIKOLOJIA!
 
... inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.

...heri wewe uliyeliona hilo!...

😀

maana hata kama 'wazungu' wamembana Mugabe asiuze mazao ulaya, basi hata soko la ndani, au southern Africa pia hakuna wa kununua?
 
Nani atanunua mazao yao wakati ni weusi?
Nani atawapa mikopo wakati ni WAAFRIKA?
Zimbabwe iliwalisha wazungu...Je WAAFRIKA WALISHWE NA NANI?
 
...heri wewe uliyeliona hilo!...

😀

maana hata kama 'wazungu' wamembana Mugabe asiuze mazao ulaya, basi hata soko la ndani, au southern Africa pia hakuna wa kununua?

Unajua maana ya vikwazo vya UCHUMI?
almasi ni YA AFRIKA!
LAKINI KAMPUNI YA SA INAMILIKI DIAMOND ZILIZOCHIMBWA KULIKO ZILE ZILIZOKO ARDHINI...KWASABABU SASA TUNAJUA MADINI YANA MWISHO..THEN..YAKIISHA NANI ATAKUWA ANA CALL SHOTS?
 
Kuna Anayejua Story Ya Zambia,copper,kilimo,nyerere Na Kaunda?
Nani Anapanga Bei Za Vyakula Na Madini?
 
Fundi Mchundo,Masanja,Koba,Kuhani Mkuu,Kitila Mkumbo,Mkandara,....

..naomba kuwauliza maswali yafuatayo wachangiaji wa mjadala huu.

..ni sera zipi za Mugabe ambazo zinasababisha inflation iwe kubwa kiasi kile?

..najua kwamba wana-print pesa kama wajinga, lakini why do they have to do it in the first place?

..vilevile ninavyoelewa mimi, in Mugabe's watch uchumi wa Zimbabwe ulipata kukua hata by double digits. what was he doing right? what is he doing wrong now?

..zaidi kuna yeyote anayefahamu sera za Morgan Tsivangarai ambazo zitaondoa hii inflation?

..pia Tsivangarai ana sera au mipango gani ya kupambana na njaa ya muda mrefu Zimbabwe?

..je Tsivangarai atarudisha ardhi kwa wazungu? kama atarudisha si kutakuwa na vita? na asiporudisha njaa itakwisha kweli? inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.


Mkuu haya maswali wengi tuna mitizamo tofauti. Lakini what I know.

1. Hilo la inflation mimi siyo mchumi. Nawaachia wenzangu wasomi!

2. Baada ya kutaifisha mashamba hali ilibadilika maana washirika wake wa magharibi walikuwa hawaingizi tena pesa, yeye alichokifanya si kukaa chini kuangalia ni namna gani wanaweza kupambana na hizo sera za ukosefu wa pesa za magharibi bila kuathirika sana, bali wale wachache waliomzunguka wakaanza kama vile kukomoa wakahodhi uchumi wote...(remember mke wake-Grace.alivyoulizwa kwa nini anafanya shopping Italy-akasema kwamba Zimbabwe hakuna designer anayeweza kupima miguu yake sawa sawa....)

3. Mwaka 2000 Morgan alipomshika Mugabe pabaya, the only card aliyokuwa nayo ilikuwa ni mashamba na aliplay na sentiments za wapiga kura kwamba mkinichagua nitawagawia ardhi. It was a populist move for him to remain in power. Well alishinda na mashamba waliopewa ni wanene, kama majaji, wanajeshi nk ambao hata kulima hawajui. (personally nina rafiki yangu ambaye aliamua kurudisha kama ekari mia mbili alizopewa na serikali).

4. Yes, whites are equally culpable for the happenings in Zim, but Mugabe alifikiria kwamba unaweza kuplay na economics kwa kutumia siasa na ukafanikiwa, and that was damn wrong! Uchumi wa kiafrika bado ni tegemezi. hatuwezi kujiengua kwenye makucha ya wazungu kabla hatujawa na foothold. So we have to know how to play the game!

5. Ndo maana mpaka leo China na ubabe wake woooote, hawezi kuwaudhi hawa westerners, He knows the consequences. China ina market lakini inahitaji pesa za macapitalist na matycoons wengine. Afrika tumeshindwa hilo!

Joka kuu acha siasa mufilisi kwamba Morgan atarudisha mashamba kwa wazungu... has he said so? I repeat politics of fear kama za CCM kwamba ukivote upinzani umevote vita ya burundi au Congo, au ile ya Zanzibar kwamba ukivote MAALIM umevote ujio mpya wa Sultan wa Oman..haisadii. We are tired of those politics bwana!
 
Jokakuu,
Shukran pamoja na kwamba issue hii ilitakiwa mada inayohusu Utawala wa Mugabe nitajaribu kuelezea ufahamu wangu kuhusiana na maswali yako..

Mimi mkuu niliwahi kukaa sana Zimbabwe na nafahamu mengi kuhusiana na nchi ile mbali na maandishi tunayoyasoma as a fact nilikuwa naenda huko mara mbili kwa mwezi kwa miaka minne mfulululizo.Nilichokiona Zimbabwe toka wapate Uhuru ni ujenzi wa chama ZANU kama vile CCM kwa muda wote uchumi wa Zimbabwe ulikuwa juu lakini fedha yao ikidondoka mwaka hadi mwaka kwa points chache.. Kufikia mwaka 1984 tayari dollar ya Zimbabwe ambayo ilikuwa senti 98 kwa dollar ya Kimarekani ilishafika 2 Zimbabwe kwa ya Kimarekani.
Uchumi wa nchi hautokani na fedha unazo print labda ktk kuokoa hali mbaya sana ya kiuchumi ambayo ishara zote za kuporomoka uchumi huo bado hazijajitokeza wazi. Mugabe alikuwa Mbabe toka mwanzo, kabla hata ya kuungana na kina Nkomo (ZAPU) nadhani unakumbua. walikufa Wandebele Kibao na kibaya zaidi hawa Wandebele wamezaa sana na wazungu kuna point five kibao Bulawayo. Uhasama wao ulikuwa mkubwa kuliko huu tunaouona leo, yaani walichinjwa kishenzi hadi ilipofikia Mwalimu kuingilia kati na bahati nzuri walifikia Muafaka wakaunda chama kimoja, kama tulivyofanya sisi..Hao Washona jamani wasikieni hivyo hivyo, wanacheka na wewe lakini anaweza kula nyama yako siku zikimpanda!

Tatizo kubwa la Uchumi Zimbabwe ni Uongozi mbaya wa Mugabe hasa baaya ya kuchukua ardhi. Walikuwa wakishuka miaka yote taratibu lakini baada ya hapo tu, nchi ilikwenda mrama na nimesema huko nyuma kwamba Mwalimu aliwahi kumkanya Mugabe asifanye hivyo hata siku moja akimkumbushia hali halisi ya Uchumi wa Tanzania ktk miaka ya mwisho ya Utawala wake.
Mugabe hakusikia baada ya Muingereza kuvunja ahadi ya ugawanaji wa ardhi na hii ilitokana na shinikizo wa Wapigania Uhuru ambao walikuwa hawana ardhi sio tu ya kilimo bali hata ile isokuwa na mashamba. Kwa mtazamo wa haraka na bila kufikiria utaona kuwa Wazimbabwe walikuwa na kila haki ya kudai ardhi yao ambayo ndio sababu kubwa ya vita ya miaka yote iliyopita..wamepoteza ndugu wengine vilema kwa sababu ya ardhi, na uchumi wa mtu ama nchi hutegemea ardhi, hivyo wakidhani kwamba wanaweza kujiendesha wenyewe wakajipanga bungeni na kupitisha sheria ya ardhi..
Toka hapo, uchumi wa nchi hiyo ulianza kuporomoka vibaya sana, na ukweli niu kwamba kila kitu kinachozalishwa nchi hiyo kilikuwa mali ya mzungu ambaye kanyang'anywa ardhi (makazi) na kuitwa mgeni hali ahadi ya awali ni kwamba wote ni Wazimbabwe. Well hii ndio hatari ya kutegemea wageni kushika vianzio vyote vya Uchumi wa nchi na pengine naweza sema ni makosa makubwa tunayoyafanya sisi Tanzania leo hii. Kesho tutakuwa hatuna jinsi isipokuwa kutegemea mzungu ktk kukuza uchumi wa nchi yetu badala ya sisi kutupa magongo ya kutegemea na tushirikiane na mzungu kama ni biashara kati yetu Tanzania na nchi za nje. Tha's why leo hii Tanzania mapato ya Taifa ni makubwa sana ukilinganisha na mchango wa pato hilo ktk mfuko wa Taifa..
Baada ya hapo Zimbabwe wamewekewa vikwazo hasa na nchi za Marekani, Canada na UK ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa mali zao na fedha yao ktk market hakuwa na nguvu tena kwa sababu hakuna mtu anayetaka kununua kitu Zimbabwe..
Haya ni matokeo ambayo aidha Mugabe aliya over look ama hakujiandaa nayo na ndio maana nashindwa kuelewa Mugabe ambaye alikuwa akisifiwa na wazungu miaka ya 80 na 90 leo kawa shetani kwa mzungu hali sera zake kiuchumi hazijabadilika, labda hilo la ardhi tu. Nyama zao za ng'ombe zilipigwa marufuku karibu dunia nzima, na binafsi siamini kuwa Wazimbabwe hawana ujuzi wa kilimo wakati ndio wao waliokuwa wakilima mashamba hayo miaka yote. After all ni Wabantu wenye kila sifa ya Ukulima..kwa hiyo swla la mbolea na mbegu limekuwa hoja kubwa sana nchini humo na kama unavyojua kilimo cha siku hizi hasa nchi zinazotumia mbegu za maabala ndio hapo!..
Mugabe hafai na kashindwa hata kufikiria wananchi wake, miaka yote kashindwa kusoma alama akitumia ile aya ya kutogeuka jiwe.. Binafsi kama unakumbuka niliwahi kusema WHY hajaribu kufikia deal na wazungu hawezi kushindana nao.. ardhi igawanywe kati yao badala ya kuchukua yote. Kata kipande kisichotumiwa na wanzungu wape hao waswahili lakini pia ni muhimu kukumbuka kwamba mswahili kuwa jirani na mzungu ni issue nyingine!.. tunajifahamu wenyewe, yet ni lazima ipo njia ya kufikia muafaka fulani wa ardhi badala ya kunyang'anya kila kitu mzungu atakushusha kama alivyowafanya kina Michael Jackson, Wesley Snipes na wengine kibao... Dunia hii huwezi kumtegemea mzungu kisha ukafikiria kuna siku unaweza kuwa fit kumgeuka atakumaliza kama Saadam Hussein. Na wanammaliza kweli hana choice Mugabe isipokuwa kung'atuka lakini Morgan sio solution ktk kutazama mustakabali wa nchi hiyo!

Sasa nikirudi kwa Morgan, huyu mkuu hana hoja ni opportunist anayetumiwa na wazungu, hii haina ubishi na ndio maana walishindana na chama cha ISO ambao walijiunga pamoja kumtoa Mugabe. lakini jamaa hawa wa ISO walipogundua njama za Morgan na chama chake wakaziweka wazi, ndipo Morgan na MDC walipovunja umoja wao..Hii inatisha sana na kama utatazama ubabe wa Mugabe na watu wake kurudisha ardhi chini ya Morgan ni hatari sana.. na yote matusi anayotumia Mugabe sio kwamba anafanya dhihaka.. watafanya kweli na Zimbabwe itageuka kuwa Somalia nyingine!..
Kifupi binafsi sioni nje ya swala hili zaidi ya kumlaumu mzungu, Mugabe na Morgan..wananchi wa Zimbabwe na kiburi chao cha kutofikiria leo hii ni vita kati ya kizazi kipya ambao hawakupitia mapigano ya Uhuru na kizazi kile kilichopigana vita.. Amani hakuna na nchi inazidi kudidimia..labda Mugabe amchukue mtu mwingie nafasi yake, yet kama ardhi hairudi ina maana uchumi wa Zimbabwe utaendelea kushuka.. It's either you give in or else!...
 
Mkuu hapa tuko pamoja. Ndo hapo tunapoona kwamba the current system we have is not working, lakini wale wanaojaribu kuibadilisha ndo tunawacrucify kama vibaraka.. Jamani ni nchi gani mpinzani atashindana na incumbent asionekane msaliti na kibaraka wa wazungu? Thats exactly what our leaders want us to believe. Sasa tusilaumu tuu, lets give alternative basi! Nani atatukomboa? au kila mtu mwenye mapenzi mema na Africa lazima aje kwenye platform ya ant western? ndo atakubalika?

Hapana, Nimekataa na nimechoka kudanganywa!


Ndugu Masanja,

Waafrika ndivyo tulivyo - kutafuta scapegoat. The most glaring example na ambayo iko fresh na wengi tulifwatilia kwa karibu sana ni hapo jirani tu - Kenya.

Mpiganiaji Raila Amolo Odinga ama Tinga aliitwa kibaraka wa Wazungu na wenye madaraka wali"allege" kuwa kumpa madaraka ni kama kuuza uhuru wa nchi hiyo. Hata huyo Kibaki aliwahi kuitwa kibaraka na Moi and the list goes on and on. What a shame.
 
Mag3,

Kama kweli hao watu walikuwa vibaraka haitakiwi kusema hata kama ushahidi upo!..
kwanza kabisa aliyesema Kuwa Morgan na MDC ni kibaraka ni watu aliokuwa ameungana nao, watu wake mwenyewe, na Mugabe used it kisiasa. Lakini ukweli unabakia pale pale kuwa jamaa alicheza na Muingereza.. Je, wewe kama raia acha unazi unalichukulia vipi?
 
Joka Kuu said:
..pia Tsivangarai ana sera au mipango gani ya kupambana na njaa ya muda mrefu Zimbabwe?

..je Tsivangarai atarudisha ardhi kwa wazungu? kama atarudisha si kutakuwa na vita? na asiporudisha njaa itakwisha kweli? inaelekea hao waliopewa mashamba hawajui kulima.

Masanja said:
Joka kuu acha siasa mufilisi kwamba Morgan atarudisha mashamba kwa wazungu... has he said so?

Masanja,

..nimeuliza maswali kuhusu sera za Tsivangarai kuhusu ardhi. vilevile nimeuliza mikakati na mipango aliyonayo kupambana na janga la njaa.

..sasa kama Tsivangarai ataendelea kuiacha ardhi ktk mikono ya wazalendo wasioweza kulima, hili tatizo la njaa litaisha vipi Zimbabwe?

..inaelekea mna taarifa fulani fulani toka kwa Tsivangarai kuhusu umiliki wa ardhi, vipi kuhusu matumizi ya ardhi hiyo?

..Tsivangarai ana mikakati gani ya kuondoa njaa Zimbabwe bila kuingilia umilikaji wa ardhi?

Masanja said:
Yes, whites are equally culpable for the happenings in Zim, but Mugabe alifikiria kwamba unaweza kuplay na economics kwa kutumia siasa na ukafanikiwa, and that was damn wrong! Uchumi wa kiafrika bado ni tegemezi.

..whites are culpable of what, and to what extent?

..muda wote nilifikiri matatizo ya Zimbabwe yamesababishwa/yanasababishwa na utawala mbaya wa Mugabe.

..pamoja na maelezo yako mazuri, bado nina maswali mengi kichwani. la msingi ni hili: Morgan anakuja kufanya mabadiliko gani haswa?


Mkandara,

..nashukuru kwa maelezo yako marefu. tatizo wewe mkuu unaandika kwa kirefu mno, hivyo najaribu kuwa makini kabla sijauliza maswali ya ziada.
 
...kidole bado kinamuelekea MUGABE...!

Tatizo kubwa la Uchumi Zimbabwe ni Uongozi mbaya wa Mugabe hasa baaya ya kuchukua ardhi...Mwalimu aliwahi kumkanya Mugabe asifanye hivyo hata siku moja akimkumbushia hali halisi ya Uchumi wa Tanzania ktk miaka ya mwisho ya Utawala wake.

...Mugabe hakusikia baada ya Muingereza kuvunja ahadi ya ugawanaji wa ardhi na hii ilitokana na shinikizo wa Wapigania Uhuru ambao walikuwa hawana ardhi sio tu ya kilimo bali hata ile isokuwa na mashamba

....wakidhani kwamba wanaweza kujiendesha wenyewe wakajipanga bungeni na kupitisha sheria ya ardhi..Toka hapo, uchumi wa nchi hiyo ulianza kuporomoka vibaya sana, na ukweli niu kwamba kila kitu kinachozalishwa nchi hiyo kilikuwa mali ya mzungu ambaye kanyang'anywa ardhi (makazi) na kuitwa mgeni hali ahadi ya awali ni kwamba wote ni Wazimbabwe.

...Baada ya hapo Zimbabwe wamewekewa vikwazo hasa na nchi za Marekani, Canada na UK ambao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa mali zao na fedha yao ktk market hakuwa na nguvu tena kwa sababu hakuna mtu anayetaka kununua kitu Zimbabwe..

...Haya ni matokeo ambayo aidha Mugabe aliya over look ama hakujiandaa nayo na ndio maana nashindwa kuelewa Mugabe ambaye alikuwa akisifiwa na wazungu miaka ya 80 na 90 leo kawa shetani kwa mzungu hali sera zake kiuchumi hazijabadilika, labda hilo la ardhi tu. Nyama zao za ng'ombe zilipigwa marufuku karibu dunia nzima, na binafsi siamini kuwa Wazimbabwe hawana ujuzi wa kilimo wakati ndio wao waliokuwa wakilima mashamba hayo miaka yote.

...na kashindwa hata kufikiria wananchi wake, miaka yote kashindwa kusoma alama akitumia ile aya ya kutogeuka jiwe.. Binafsi kama unakumbuka niliwahi kusema WHY hajaribu kufikia deal na wazungu hawezi kushindana nao.. ardhi igawanywe kati yao badala ya kuchukua yote. Kata kipande kisichotumiwa na wanzungu wape hao waswahili lakini pia ni muhimu kukumbuka kwamba mswahili kuwa jirani na mzungu ni issue nyingine!..

...Dunia hii huwezi kumtegemea mzungu kisha ukafikiria kuna siku unaweza kuwa fit kumgeuka atakumaliza kama Saadam Hussein. Na wanammaliza kweli hana choice Mugabe isipokuwa kung'atuka lakini Morgan sio solution ktk kutazama mustakabali wa nchi hiyo!

..labda Mugabe amchukue mtu mwingie nafasi yake, yet kama ardhi hairudi ina maana uchumi wa Zimbabwe utaendelea kushuka.. It's either you give in or else!...

...Mkuu Mkandara sina la kuongeza, darasa lipo well and clear, na kwa sababu huyu Mugabe haambiliki, ndio maana hata hakusoma alama za nyakati kuwa afadhali angeng'atuka na kumuachia kijana mfano Simba Mukoni agombee kwa ticket ya ZANU-PF. Kwa kudhani ni yeye pekee anastahiki kuongoza nchi mpaka kifo 'kitapomtenganisha'...

...hata kama Tsvangarai hafai, Mugabe namuona ni Tyrant kwa vitendo na kauli zake.

I wish Mugabe angeukumbukia usemi; 'Dont argue with a spouse who packs your parachute!'

am out!
 
Nani anayefikiri kuwa Mkololoni aliondoka ZIMBABWE KWA KUPENDA?
JE...SERA ZA MZUNGU KABLA YA KUTOLEWA RHODESIA KWA DAMU ZIMEBADILIKA?
JE..TUMSIKILIZE NANI?
KUNA KITU MUGABE AMEONA?
JE WAZUNGU BADO WANAPENDA ZIMABABWE IWE HURU?
 
Kuna mtu anayejua kuwa bila ZAIRE cellular phone zisingekuwepo?
Kuna mtu anayejua kuwa makampuni makubwa ya wazungu yametajirishwa na MASIKINI MWEUSI?
 
Back
Top Bottom