Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Fundi Mchundo,

..huyo Mandela alikuwa wapi siku zote anakuja kusema leo? alikuwa wapi wakati wa-Congo milioni 3 wanakufa? ni hilo disco analopigiwa huko London ndiyo limemfanya aseme?

..nimeuliza kule inakuwaje Mugabe ambaye aliweza kuendesha uchumi ukakua hata kwa double digits leo hii agueze nchi kuwa mufilisi?

..pia inakuwaje nchi ambayo inakabiliwa na janga la njaa ikawekewa vikwazo na vyombo vya fedha, na zaidi ikalazimishwa kulipa madeni yake on time?

..kuna ripoti zinazomnukuu Mtanzania Peter Ngumbula, aliyekuwa head wa African desk IMF, akilalamika kwamba Zimbabwe imenyimwa fedha za budjet support kwasababu za kisiasa.

..sikumsikia Mandela, Askofu Desmond Tutu, Askofu Sentamu,...wakilaani ukatili huo wa vyombo vya fedha vya kimataifa. ndiyo maana wengine tunaona hawa wamekuwa kama vibaraka.

..kwa yeyote yule ambaye amejisumbua kufuatilia historia ya Zimbabwe, lazima ataelekeza lawama kwa wote[Mugabe,Tsivangarai,Tony Blair,ZANU,MDC,Labor Party] wanaohusika na mgogoro huu kwa kutufikisha hapa tulipofika.

..ni uhuni kwa chama cha Upinzani kupiga kampeni kwa wafadhili ili serikali iliyoko madarakani ikatiwe misaada, kwa nia ya kuifanya ichukiwe na wapiga kura, ili kukiwezesha chama cha upinzani kuingia madarakani. hicho ndicho walichofanya MDC for more than 10 yrs.

..NAOMBA NIMALIZE KWA KUSEMA KWAMBA HALI YA KISIASA IMECHAFUKA MNO ZIMBABWE KWA SASA HIVI. ZANU NA MDC WANAHUSIKA MOJA KWA MOJA KWA SIASA CHAFU ZA KUWAGAWA WANANCHI.

..KWA MAONI YANGU NI BORA JESHI LITWAE MADARAKA ZIMBABWE. SHUGHULI ZA SIASA ZISIMAMISHWE, NA BADALA YAKE SERIKALI YA MPITO IJIELEKEZE KTK KUTATUA MATATIZO YA KIUCHUMI YA ZIMBABWE.

Mandela alikuwa wapi wakati wa Sierra Leone wanauawa? Mandela alikuwa wapi wakati wa Ivory Coast wanachinjana, Mandela alikuwa wapi wakati waSomali wanachinjana, Mandela alikuwa wapi wakati wa Liberia wananyongana? Mandela ni retired president. Kuna watu wameuliza kwa nini hakutolea tamko South Afrika? Madiba anachelea sana kum'criticise' rais wake na tamko lolote kutoka nyumbani kwake itaonekana hivyo. Tofauti na Tutu. Tutu anajisemea bila kujali yuko wapi. Yeye atasema tu linalomuuma. Hawa wawili hata wangenyambaza, hauwezi kuwaita vibaraka. Kama alivyosema Madiba kwenye hilo Disco, mzigo ni mzito kwa mtu mwenye umri wa miaka 90!

Ameiba. Amewanyang'anya waliokuwa wanachangia uchumi na kuwapa mashoga zake ambao hawana nia yeyote na maendeleo ya nchi yao. Wezi wenzake. Hata sisi mara baada ya uhuru uchumi wetu ulikuwa unakuwa sana. Mpaka tulipoamua kushikawenyewe utamu. Bila maandalizi. Uka nosedive. Lakini pengine yote haya kwako ni simulizi tu. Kuwa si ajabu kiongozi kuharibu uchumi wa nchi yake katika muda mfupi kwa maamuzi na matendo mabovu.

Vikwazo ambavyo mnang'ang'ania kutumia kama kisingizio ni kwake yeye binafsi na viongozi 140 wa serikali yake. Baada ya uchaguzi huu haramu ndiyo Marekani inafikiria kufanya vikwazo hivyo vijumuishe familia za wahusika.Hakuna trade embargo dhidi ya Zimbabwe iliyowekwa na serikali yeyote. Kama una ushahidi to the contrary, uweke humu badala ya kutumia talking points za Mugabe. Hii ni www kwa hiyo haitakuwa vigumu kupata tamko la kiongozi yeyote wa nchi za magharibi akitamka kuwekewa vikwazo vya uchumi Zimbabwe.

Hata ungekuwa wewe ungetoa hela kusupport nchi yenye inflation rate iliyo katika maelfu? Nchi ambayo badala ya kunua chakula kwa watu wake inakimbilia silaha? Nchi ambayo ime'unilaterally seize assets za raia zake na za mashirika ya kigeni? IMF misaada yake inatanguliwa na conditions. Moja ya conditions ni ku'control inflation. Nyingine ni structural adjustments. Huyo mtanzania amesema kuwa Zimbabwe ilikubali hizi conditions na muhimu zaidi, je, walishaanza kuzitimiza? Ukumbuke si lazima kukubali hizi conditions. Malaysia walikataa, wakanyimwa msaada, na bado wanapeta. Unasahau kuwa Mwalimu alitamka yeye hawezi kuzitimiza na ni moja ya sababu zilizomfanya amwachie Mwinyi? Kama ni kweli huyo bwana katamka hayo, ni yeye anayeingiza siasa. Sitoshangaa maana pengine anajipalilia kuukwaa ugavana siku za mbeleni.

Ukatili upi wa vyombo vya fedha? Mbona hata sisi tulinyimwa mpaka tulipokubaliana na masharti yao? Ulitaka Madiba, Tutu na Sentamu waseme nini? Kuwa wapeni tu kama tulivyozoea kulazimisha financial institutions zetu kutoa mikopo hata pale ambapo dhahiri wanaona kuna matatizo.

Mwenye responsibility kubwa ni yule anayetawala nchi husika. Hauwezi kusema Morgan na Mugabe wote culpability yao ni sawa.

Aha! Na si uhuni kuwafanyia wananchi wako yale anayoyafanya mugabe. Au MDC wangeomba silaha ili waingie mwituni kama walivyofanya wengi katika bara ndiyo ungewaona si wahuni? MDC mpaka leo wanadai kuwa mataifa ya nje yauwekee presha utawala wa Zimbabwe. Presha si lazima iwe sanctions.

Na bila aibu, unahitimisha kwa kupendekeza jeshi ndiyo lipewe mamlaka Zimbabwe? jeshi hilo hilo lililotangaza toka awali kuwa haliko tayari kumpigia saluti kiongozi mwingine yeyote asiye Mugabe! jeshi hilo hilo linalotumika kikamilifu katika uhalifu unaofanyika Zimbabwe? Hawa waliozawadiwa mashamba ndiyo leo unataka watatue matatizo ya uchumi Zimbabwe. Are you for real?

Amandla......
 
..wako viongozi wengi ambao ni stooge,tena wengi wao wako madarakani. wanatofautiana mabwana wanaojipendekeza kwao tu.

..ungekuwa wewe ungekimbilia wapi?

Wanasahau sisi tuliisha warudisha wakenya waliokimbilia kwetu kuomba hifadhi ya kisisiasa. Hao waKenya walinyongwa!
 
..wako viongozi wengi ambao ni stooge,tena wengi wao wako madarakani. wanatofautiana mabwana wanaojipendekeza kwao tu.

..ungekuwa wewe ungekimbilia wapi?

nadhani ingekuwa bora kama swali lingekuwa " ungepata nafasi ungemshauri akimbilie ubalozi gani?".

huyu mheshimiwa alikimbilia ubalozini na kama sikosei siku iliyofuata alitoka kwenda kufanya press conference. kwa mantiki hiyo sinahakika kama uhai wake ulitishiwa kiasi kwamba ikabidi akimbilie ubalozi ulio karibu.

katika mazingira ya kisiasa naamini huko harare zipo nchi kadhaa za kiafrika ambazo hazijachukua upande. angekimbilia huko. kama huko nako anawasiwasi basi angalau angekimbilia ubalozi wa tanzania na kudai kwamba kaenda huko sababu ni tz ni mwenyekiti wa au.
 
Kama kawaida yetu, tulifumbia macho!

Pamoja na kuwakumbatia makikteta wa Havana na kwingineko, hili linasema nini kuhusu commitment ya Nyerere kwenye haki za binadamu na stature yake duniani kama mtu mwenye misingi?

Mimi nadhani inatoboa tundu kubwa kwenye joho tulilomvika pamoja na dunia nzima kuwa ni "Mbuyu Wa Afrika" wa usawa, haki na dhamira.
 
nionavyo mimi wengi tunakubaliana kwamba jongwe amefanya mabaya kwa wananchi wake. naona tunatofautiana katika tafsiri yetu ya matukio yanayoendelea hususan mchango wa vyombo vya habari vya mataifa makubwa, mchango wa nchi kama uingereza na marekani na pia tunavyomuona bwana morgan.

hata hivyo matokeo ya tofauti hizi za mitazamo binafsi nimefaidika na michango mbali mbali. asantei wote
 
Tanzania na Afrika walisimama wapi kuhusu hili, miaka hiyo?

Kuhani,

Usishangae kuona hata dakika hii kuna watu wanadiriki kutetea matendo ya Mugabe na kutaka kuwabebesha mzigo mizimu ya Ian Douglas Smith.
 
Kosa la MDC (kama ilivyo kwa CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi, UPD, DP, na vyama vingenevyo vya upinzani hapa kweu) ni kukubali kufanya uchaguzi chini ya katiba iliyotungwa na chama kongwe kilichoko madarakani. Katiba hiyo ndiyo iliyompa madaraka Mugabe kuteua Tume ya Uchaguzi, Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Majeshi, na Majaji wa Mahakama ambao wote hawa wamechangia kuhakikisha kuwa Mugabe anarudi madarakani hata kama hatakiwi na wananchi wake, yaani wanalinda udikteta badala ya kulea demokrasi. Mabadiliko ya katiba ni ya muhimu sana kama tunataka kuhakikisha kuwa demokarasi halisi inapata nguvu nchini kwetu, ama sivyo tutaendelea kulia kilio cha samaki siku zote kama ilivyo kwa MDC.

Sasa ngoma inayowapata MDC ni kuwa, kesho Mugabe ataapisha wabunge wote, wakati chama chake kina wabunge wachache. Sasa kama wabunge wa MDC watakubali kuapishwa na Mugabe then, watakuwa wamemtambua! na wakikataa kuapishwa naye, then hawataruhusiwa kufanya shughuli za bunge na watakuwa wamejifukuza ubunge!

Mbaya zaidi ni kuwa, pamoja na Chama cha Mugabe kupata viti vichache sana Bungeni kwenye uchaguzi na yeye mwenyewe kuupata kura chache kulinganisha na idadi halisi ya waliopiga kura hata baada ya uchaguzi wa marudio, bado Mugabe atateua wabunge wengine 30 kutoka kwenye chama chake na kukifanya kiwe na majority!!

KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA: Hilo ndilo jawabu la matatizo yote haya.
 
Mandela alikuwa wapi wakati wa Sierra Leone wanauawa? Mandela alikuwa wapi wakati wa Ivory Coast wanachinjana, Mandela alikuwa wapi wakati waSomali wanachinjana, Mandela alikuwa wapi wakati wa Liberia wananyongana? Mandela ni retired president. Kuna watu wameuliza kwa nini hakutolea tamko South Afrika? Madiba anachelea sana kum'criticise' rais wake na tamko lolote kutoka nyumbani kwake itaonekana hivyo. Tofauti na Tutu. Tutu anajisemea bila kujali yuko wapi. Yeye atasema tu linalomuuma. Hawa wawili hata wangenyambaza, hauwezi kuwaita vibaraka. Kama alivyosema Madiba kwenye hilo Disco, mzigo ni mzito kwa mtu mwenye umri wa miaka 90!

Ameiba. Amewanyang'anya waliokuwa wanachangia uchumi na kuwapa mashoga zake ambao hawana nia yeyote na maendeleo ya nchi yao. Wezi wenzake. Hata sisi mara baada ya uhuru uchumi wetu ulikuwa unakuwa sana. Mpaka tulipoamua kushikawenyewe utamu. Bila maandalizi. Uka nosedive. Lakini pengine yote haya kwako ni simulizi tu. Kuwa si ajabu kiongozi kuharibu uchumi wa nchi yake katika muda mfupi kwa maamuzi na matendo mabovu.

Vikwazo ambavyo mnang'ang'ania kutumia kama kisingizio ni kwake yeye binafsi na viongozi 140 wa serikali yake. Baada ya uchaguzi huu haramu ndiyo Marekani inafikiria kufanya vikwazo hivyo vijumuishe familia za wahusika.Hakuna trade embargo dhidi ya Zimbabwe iliyowekwa na serikali yeyote. Kama una ushahidi to the contrary, uweke humu badala ya kutumia talking points za Mugabe. Hii ni www kwa hiyo haitakuwa vigumu kupata tamko la kiongozi yeyote wa nchi za magharibi akitamka kuwekewa vikwazo vya uchumi Zimbabwe.

Hata ungekuwa wewe ungetoa hela kusupport nchi yenye inflation rate iliyo katika maelfu? Nchi ambayo badala ya kunua chakula kwa watu wake inakimbilia silaha? Nchi ambayo ime'unilaterally seize assets za raia zake na za mashirika ya kigeni? IMF misaada yake inatanguliwa na conditions. Moja ya conditions ni ku'control inflation. Nyingine ni structural adjustments. Huyo mtanzania amesema kuwa Zimbabwe ilikubali hizi conditions na muhimu zaidi, je, walishaanza kuzitimiza? Ukumbuke si lazima kukubali hizi conditions. Malaysia walikataa, wakanyimwa msaada, na bado wanapeta. Unasahau kuwa Mwalimu alitamka yeye hawezi kuzitimiza na ni moja ya sababu zilizomfanya amwachie Mwinyi? Kama ni kweli huyo bwana katamka hayo, ni yeye anayeingiza siasa. Sitoshangaa maana pengine anajipalilia kuukwaa ugavana siku za mbeleni.

Ukatili upi wa vyombo vya fedha? Mbona hata sisi tulinyimwa mpaka tulipokubaliana na masharti yao? Ulitaka Madiba, Tutu na Sentamu waseme nini? Kuwa wapeni tu kama tulivyozoea kulazimisha financial institutions zetu kutoa mikopo hata pale ambapo dhahiri wanaona kuna matatizo.

Mwenye responsibility kubwa ni yule anayetawala nchi husika. Hauwezi kusema Morgan na Mugabe wote culpability yao ni sawa.

Aha! Na si uhuni kuwafanyia wananchi wako yale anayoyafanya mugabe. Au MDC wangeomba silaha ili waingie mwituni kama walivyofanya wengi katika bara ndiyo ungewaona si wahuni? MDC mpaka leo wanadai kuwa mataifa ya nje yauwekee presha utawala wa Zimbabwe. Presha si lazima iwe sanctions.

Na bila aibu, unahitimisha kwa kupendekeza jeshi ndiyo lipewe mamlaka Zimbabwe? jeshi hilo hilo lililotangaza toka awali kuwa haliko tayari kumpigia saluti kiongozi mwingine yeyote asiye Mugabe! jeshi hilo hilo linalotumika kikamilifu katika uhalifu unaofanyika Zimbabwe? Hawa waliozawadiwa mashamba ndiyo leo unataka watatue matatizo ya uchumi Zimbabwe. Are you for real?

Amandla......

Haya siku zote ndo mawazo ya sisi waafrika, lazima tuitafute Marekani au Uingereza kwa matatizo yetu.Tunafanya upumbavu then tunaushabikia na kuuhalalisha tukidhani tunaikomoa Marekani au Uingereza, kumbe tunajiumiza sisi wenyewe. Waafrika tunashindwa kuondokana na umasikini na kutatua matatizo yetu kwa kuwa tumeshindwa kukubali kuwa sisi ndo tatizo.
 
Fundi Mchundo,

..katika dunia ya leo IMF na WB wakikuwekea vikwazo basi huwezi kupata fedha toka chombo chochote kile cha fedha cha nchi za magharibi.

..ninavyoelewa mimi Peter Ngumbulu kama head wa IMF Africa Desk alisema hayo aliyosema kwasababu aliamini Zimbabwe imetimiza masharti ya kupata fedha za IMF.

..hakuna haja ya kusubiri tamko la viongozi wa nchi za magharibi kuwa Zimbabwe imewekewa vikwazo. situation on the ground inaelekeza kwamba Zimbabwe inakabiliwa na ukata uliosabibishwa na vikwazo.

..wakati ule Tanzania tunapanga foleni kwani Mwalimu na mawaziri wake walikuwa wamewekewa vikwazo vya kusafiri? je kuna kiongozi wa nchi za magharibi alitutangazia vikwazo?

..Mugabe hakukurupuka[unilaterally] tu na kutaifisha mashamba. hatua ya kwanza aliyofanya ni kutekeleza makubaliano ya Lancaster kusubiri kwa miaka 20 kabla hajachukua hatua zozote ku-distribute ardhi.

..Mugabe aliitisha mkutano wa wadau wote kuhusu suala la ardhi Zimbabwe. Mkutano huo ulivunjika kwasababu Waingereza na Wamarekani walipinga wazo la kugawa ardhi Zimbabwe.

..Baada ya hapo Mugabe aliitisha referendum ya kubadili katiba ili kumpa nguvu za kisheria kugawanya ardhi. Waingereza wakawatumia MDC kukampeni na mapendekezo ya katiba yakashindikana.

..lakini mapendekezo hayo hayo ya katiba yalikuwa na vipengele ambavyo vingempunguzia Raisi/Mugabe madaraka, na zaidi kufanya chaguzi kuwa huru zaidi. MDC wangekuwa siyo vibaraka wasingeyapinga mapendekezo yale ya katiba.

..sintoendelea zaidi lakini pia kuna barua ya Waziri Claire Short wa Uingereza chini ya Waziri Mkuu Tony Blair[labour party] ambayo unaweza kuitafsiri kama uamuzi wa Uingereza kutoyatambua makubaliano ya Lancaster.

Mag3,

..Mugabe alikuwa number 3 katika uongozi wa ZANU, baada ya Chitepo na Takawira[??].

..Takawira alifia kizuizini kabla Chitepo hajauawa. sasa yalipotokea mauaji yale moja kwa moja Mugabe akawa mrithi wa uongozi.

..inasemekana Chitepo aliuawa na kundi la Josiah Tongogara na wenzake.

..nadhani Kaunda alikuwa akiwawekea longolongo Wazimbabwe kuhusu kuendesha vita dhidi ya Ian Smith. badala yake ZANU wakahamia Msumbiji na kuweza ku-recruit wapiganaji na kuteka maeneo makubwa ndani ya Rhodesia.

..Mugabe alikuja kuungwa mkono na Samora na Nyerere wakati Nkomo aliungwa mkono na Kaunda. actually nafikiri kuna mahali Nkomo ameandika akimlaumu Nyerere kwa kumpendelea Mugabe.

..zaidi wapigania wa ZAPU/Nkomo waliwahi kutungua ndege ya kiraia, na Nkomo alitoa statements za kikatili kiasi kwamba jumuiya ya kimataifa isingemkubali kama kiongozi wa Zimbabwe.

..kabla ya mauaji ya Wandebele yaliyofanywa na 5th brigade kulitokea mapigano kati ya ZANU na ZAPU ktk maeneo ya midlands na mandebele. pia kulifanyika hujuma dhidi ya jeshi la anga la zimbabwe huru. wakati huo huo maofisa wengi wa jeshi wa kizungu walitimkia afrika kusini. mwisho makasha ya silaha yalipatikana ktk mashamba ya viongozi wa ZAPU.

..kulikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba yaliyotokea Msumbiji[Renamo], yanaweza kuikuta Zimbabwe.

..pamoja na yote hayo Mugabe aliomba radhi kwa mauaji ya ndebele. upatanishi ulishafanyika na ZANU na ZAPU-PF wakaunda chama kimoja ZANU-PF. Joshua Nkomo aliteuliwa kuwa Makamu wa Raisi wa Zimbabwe na ZANU-PF. Viongozi wa jeshi la ZAPU walipewa heshima zao na kuzikwa ktk heroes acres kama wenzao wa ZANU.

..inashangaza kwamba MDC wameamua kufungua jeraha la mauaji yale kwa manufaa ya kisiasa. serikali ya Ian Smith iliua raia wengi tu, tena kwa kutumia silaha za kemikali. serikali ya Zimbabwe ilimsamehe bila masharti yoyote. kama MDC walikuwa wana uchungu sana na maisha ya Wazimbabwe basi wangepaswa kumsakama Ian Smith kabla hata ya Mugabe.
 
Ndugu Zangu Ni Vyema Tukaendelea Na Mjadala Huu Kama Tupendavyo...lakini Ni Muhimu Ni Wa Update Kuwa Vita Hakuna Tena.

Kilichobaki Sasa Ni Kazi Ya Kulielewesha Congress La Usa Likatae Mipango Ya Mwisho..ama Option Ya Mwisho Ya Kuwawekea Vikwazo Wananchi Wa Zimbabwe Na Huku Wakijidai Kuwa Eti Ni Mugabe Wamemwekea Vikazwo!

Sasa Kama Ni Kweli Vikwazo Vitamwathiri Mugabe Na Si Wazimbabwe Wanyonge Na Masikini Wanaokufa Kwa Njaa...then Kwanini Vikwazo Hivyo Havikuwazuia Wachina Kutoa Silaha?

Waende Huko Basi....!
 
Si kuna wale wanaosapoti KICHAKA?

SASA FYI..NO WAR!

OPTION 2...KUMPA SILAHA KIBARAKA...HII INATAYARISHWA.
HOW?

VIKWAZO AND MORE VIKWAZO ILI WATU WAFE NJAA NA WAO KUITUMIA NAFASI HIYO KUANZISHA GUERILLA WAR KWA KUTUMIA VIBARAKA.

Hivi kwanini KIKWETE HAKUMUULIZA KICHAKA KUWA NI KIVIPI KUWE NA VIKWAZO NA AT THE SAME TIME UCHINA WAFIKISHE SILAHA HUKO?

Thabo Mbeki kwa kutumia RESOLVE YA WAZALENDO...ATAKABIDHIWA MAJUKUMU.

KIKWETE KAA NYUMBANI NA HATUTAKI MISAFARI YAKO TENA HADI UKAMATE KWANZA MAFISADI!

Kwa taarifa yenu NYIE MAMLUKI....

HIVI MULITAKA VIPI MANDELA AJE KWENYE MAZISHI YA MWALIMU NA WAKATI WANATAKA KUIPELEKA NCHI YETU KWENYE VITA NA SA?

Mi nakwambia mngeenda vitani basi MWAFRIKA KUSINI ANGEKUNYOOSHENI NYIE NA KICHAKA WENU!

DAMN IT!
 
..ninavyoelewa mimi Peter Ngumbulu kama head wa IMF Africa Desk alisema hayo aliyosema kwasababu aliamini Zimbabwe imetimiza masharti ya kupata fedha za IMF.

..hakuna haja ya kusubiri tamko la viongozi wa nchi za magharibi kuwa Zimbabwe imewekewa vikwazo. situation on the ground inaelekeza kwamba Zimbabwe inakabiliwa na ukata uliosabibishwa na vikwazo.

..wakati ule Tanzania tunapanga foleni kwani Mwalimu na mawaziri wake walikuwa wamewekewa vikwazo vya kusafiri? je kuna kiongozi wa nchi za magharibi alitutangazia vikwazo

Kweli, apendae, chongo huita kengeza!

Sasa kama hao viongozi (sio lazima rais au waziri mkuu. Msemaji wa serikali yeyote!) hawajatamka kweli hivyo ni vikwazo?

Kama kweli kuzuiwa kutembelea nchi za magharibi na ku'freeze' assets za viongozi hawa ndiko kulikoyumbisha uchumi wa Zimbabwe, basi extent ya wizi wao unatisha! Hatukuwekewa vikwazo bali financial institutions na nchi nyingi za magharibi zilikataa kutusaidia kiuchumi hadi hapo tutakapobadilisha sera zetu za uchumi.

Waingereza wakawatumia MDC kukampeni na mapendekezo ya katiba yakashindikana.

..lakini mapendekezo hayo hayo ya katiba yalikuwa na vipengele ambavyo vingempunguzia Raisi/Mugabe madaraka, na zaidi kufanya chaguzi kuwa huru zaidi. MDC wangekuwa siyo vibaraka wasingeyapinga mapendekezo yale ya katiba.

Uongo mwingine! Alitaka kujiongezea nguvu na ndiyo maana WANANCHI wakamstukia. Si MDC waliokataa hizo so-called reforms bali ni wananchi! Hao waingereza kwani waligawa vitenge mpaka vijijini?
 
Nyie Mnaotetea Kaburu Nauliza!
Vikwazo Mnavyotaka Kichaka Aweke Kwa Zimbabwe Vinamwathiri Mugabe Ama Myonge Mzimbabwe?
Jibu Tafadhali.
Aluta Continua!
 
Na wale niliowaambia kuwa vikwazo vya kiuchumi NI TATIZO LA KISAIKOLOJIA WAKABISHA...THEN NA RECOMMEND HAKUNA KUMPA KIONGOZI NCHI KAMA HAJUI WHATS PSYCHOLOGY!

Njaa ni tatizo la kisaikolojia kwani HUATHIRI MBONGO ZETU AS IN UWEZO WA KUFIKIRIA NA HATA KUAMUA!

Kwa kifupi mnageuka MAZEZETA!

NA KUWAPEKEA WANANCHI WA ZIMBABWE NJAA...NI KUWAPELEKEA UZEZETA ILI WAMWEKE KIBARAKA WA MKABURU!

HAO MASAPOTA WA TSIVANGARAI WANAPEWA CHAKULA NA HUKU WANANCHI WAKIFA NJAA NA NYIE MNASEMA NI WATU HAO?

SASA MAZEZETA YANAJUWA HAKI ZAO NYIE MAMLUKI WA SHETANI?

HUWEZI KUFANYA MAAMUZI YA MAANA KAMA TUMBONI HAKUNA KITU!

AFRIKA YENYE NJAA...NI AFRIKA YA MAZEZETA,VICHAKA,VIKWETE NA WENGINEO!

NA KAMWE SI AFRIKA YA MZALENDO!

AFRIKA YA MZALENDO NI AFRIKA HURU!

TUNAANZA NA TANZANIA!

WENZETU WA ZENJI WAKIGOMA...TUNAANZA NA TANGANYIKA!

AFRIKA WILL BE FREE!
 
Mag3,

..Mugabe alikuwa number 3 katika uongozi wa ZANU, baada ya Chitepo na Takawira[??].

kama MDC walikuwa wana uchungu sana na maisha ya Wazimbabwe basi wangepaswa kumsakama Ian Smith kabla hata ya Mugabe.

JokaKuu,

Mwaka 1963 ZAPU ilipogawanyika, ZANU ilianzishwa na Reverend Ndabaningi Sithole, Edgar Tekere, Edson Zvobgo, Enos Nkala and lawyer Herbert Chitepo. Zanu ilikuwa na mahusiano ya karibu na PAC (Pan African Congress) ya Afrika Kusini wakati ZAPU ilihusiana mno na ANC (African National Congress). Mpaka hapo Mugabe akawa bado yuko ZAPU pamoja na Nkomo. Kwa kutokuridhika na nafasi yake ndani ya ZAPU alihama akajiunga na ZANU. Baada ya kifo cha Chitepo na mgogoro kutokea, makundi ya kikabila yakajitokeza moja ZANU (Ndonga) likiongozwa na Sithole na ZANU (Shona) likiongozwa na Mugabe. Huyo ndiye Robert Mugabe.

Naomba pia tusichanganye mambo hapa. Ian Smith (marehemu) hatuwezi kumrudisha ajibu mashitaka. Mugabe on the other hand yupo na anatumia kila uwezo alio nao kung'ang'ania madaraka na zaidi ya yote matendo yake kwa raia wa Zimbabwe hayawezi tena kufumbiwa macho. Hapa siyo swala la kuwatetea wazungu, NO - ni swali maisha ya wana Zimbabwe. Mugabe anazidi kutufanya Waafrika tudharauliwe.
 
Inawezekana nilikurupuka kumuita JokaKuu muongo kwenye suala la constitutional reforms za mwaka 2000. Ndani yake kulikuwa na vipengere (two term limits kwa rais) ambavyo sasa hivi vingemng'oa Mugabe.
Ninaiweka hapa ili wenyewe mjiamulie kama kweli ilikuwa inaongeza uhuru au kumuongezea madaraka Mugabe. Hii hapa:
http://en.wikisource.org/wiki/Proposed_Constitution_of_Zimbabwe

Tenure of office of President

1. In this section-

"term of office" includes part of a term of office.

2. The term of office of the President is a period of five years and no one may hold office as President for more than two terms.

Au hii ilikuwa ni asali iliyoficha sumu?

Amandla....
 
JokaKuu,

Ni lini mara yako ya mwisho kufika Zimbabwe? Nina imani kuwa inawezekana tulikuwa pamoja pale Harare nyakati zile za miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini.

Mugabe ni kama mamba; anajua sana kulia machozi ya mamba, na vile vile anajua sana kutumia mdomo wake kujipatia mahitaji yake kama afanyavyo mamba.

Mugabe aliingia madarakani kuiongoza ZANU kwa kupigiwa debe kali sana na Edgar Tekere; je unajua leo amemtupa wapi mzee huyu?

Kama kweli wapigania uhuru wa ZAPU walipewa hadhi ya kuzikwa heroes acres, je unajua James Chikerema aliyefariki mwaka 2006 amezikwa wapi?
 
kichuguu,

..ni kweli Edgar Tekere alimbeba sana Mugabe ndani ya ZANU. lakini inawezekana kwamba Mugabe alikuwa very calculating. katika simulizi zote inaelekea Tekere alikuwa radical and hot headed wakati Mugabe alikuwa moderate.

..Edgar Tekere ndiye anakuwa credited kwa kumkaribisha Bob Marley kwenye uhuru wa Zimbabwe.

..tatizo la Tekere ni ile kesi yake ya mauaji. ile hukumu ya "not guilty" nadhani ndiyo malipo ya fadhila zake kwa Mugabe.

..sijafuatilia kuhusu Chikerema, lakini najua kwamba suala la kuzikwa heroes acres limekuwa na utata sana. kwa hilo siwezi kumtetea Mugabe moja kwa moja.

Fundi Mchundo,

..i am learning a great deal from you.

..i read some where kwamba constitutional referendum kulikuwa kuna vipengele vya Proportional Representation, na nafasi ya Waziri Mkuu.

..vilevile kamati walipendekeza waziri mkuu anayeteuliwa na bunge, lakini Mugabe akacheza majanja na ku-doctor report isomeke waziri mkuu anayeteuliwa na raisi.

..kile kitendo cha MDC kuipinga referendum ndiyo kikampa Mugabe hoja kwamba MDC is against land redistribution.

..wako wanaoichukulia kampeni ya MDC kupinga constitution mpya kama strategic mistake.
 
Inawezekana nilikurupuka kumuita JokaKuu muongo kwenye suala la constitutional reforms za mwaka 2000. Ndani yake kulikuwa na vipengere (two term limits kwa rais) ambavyo sasa hivi vingemng'oa Mugabe.
Ninaiweka hapa ili wenyewe mjiamulie kama kweli ilikuwa inaongeza uhuru au kumuongezea madaraka Mugabe. Hii hapa:
http://en.wikisource.org/wiki/Proposed_Constitution_of_Zimbabwe

Au hii ilikuwa ni asali iliyoficha sumu?

Amandla....

Katiba hii ilikuwa nzuri; kushindwa kupitishwa kwa katiba hii kulitokana kwa kiasi kikubwa na matendo ya Mugabe mwenyewe na kwa kiasi fulani upande wa upinzani pia.

(a) Tume ya katiba iliteuliwa kipendeleoa, wote walikuwa watu wa Mugabe.

(b) Utawala wake ulikuwa unalaumiwa sana kutokana na maisha magumu. Ucahguzi wa mwaka huo ulikuwa mgumu sana kwa Mugabe. Ndipo akaamua kuanza na hili la katiba ili kukabiliana na uchaguzi. Tatizo kubwa lilikouwepo ni kuwa Katiba hii ilikuwa inapitishwa Mwezi wa pili tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwezi wa tatu. Ni dhahiri kuwa mapendekezo yote ya muundo wa serikali katika katiba hii yasingetekelezwa kabla ya uchaguzi mkuu. Upinzani walitaka kutumia referendum hii kama vote of no confidence kwa serikali.

(c) makosa ya upitishwaji wa katiba yalitokana na pande zote. Upande wa Mugabe na upande wa upinzani ambao waliamini wakati huo kuwa wangeshinda uchaguzi ule na kuunda katiba mpya. Kwa bahati mbaya walikatwa mkenge na Mugabe kiasi kuwa hadi leo hawajaweza kuwa na katiba ya uwazi tena.
 
Back
Top Bottom