Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant

Tatizo la wengi wetu ni bigotry na kukataa responsibility kwa matendo yetu. Tunaona mkono wa mtu mweupe hata pale ambapo sisi wenyewe ndiyo chanzo. Tunamlaumu mtu mweupe kwa kutuingilia mambo yetu na asipoingilia, tunamlaumu kwa kutoingilia. Tunatendeana unyama na ukatili usiofikirika ( DRC, Sudan, Sierra Leone, Ivory Coast, Liberia, Rwanda, Zimbabwe n.k.), anapotukemea mtu mweupe kwa kufanya hayo tunamwambia akae nje kwa sababu hatutakii memba. Tunapochoka kufanyiana ukatili huo au aibu inapotuingia, tunamlaumu mtu mweupe kwa kutotuzuia kuchinjana, kunyofoana viungo, kutoana utumbo nje, kuchomana tukiwa ngdani ya nyumba, kubaka vijukuu vyetu na matendo mengi ambayo tumefanyiana watu weusi kwa watu weusi! Mtu mweusi yeyote akishukiwa kwa kutenda uovu au makosa ya aina yeyote, kuanzia O.J, Michael Jackson, Wesley Snipes, Naomi Campbell hadi Robert Mugabe kimbilio lao la kwanza ni kuwa mnanituhumu kwa sababu mimi ni mtu mweusi. Hawa wote wanatambua weusi wao wakati wakiwa katika matatizo.

Leo wananchi wa Zimbabwe katika nchi inayotawaliwa kibabe na mmoja wetu walidiriki, katika mazingira hayo, kumpigia kura mpinzani wa Mugabe. Badala ya kuheshimu ushujaa na msimamo wao, leo tunawatuhumu kuwa wao hawana akili, ni lazima walishurutishwa na mtu mweupe! Mtu mweupe ambaye amenyang'anywa karibu kila kitu nchini humo bado tunamtafuta chini ya kitanda! Tunasahau kuwa yeyote anayempinga Mugabe anaitwa kibaraka wa watu weupe. Hakuanza na Morgan na bila shaka akitokea mwingine naye ataitwa kibaraka.

Humu ndani watu wamefikia hata kuwaita Mandela ( aliyefungwa miaka 27, aliyesimama kidede kutetea uhuru wa nchi yake hata alipokuwa anaangalia hukumu ya kifo) na Desmond Tutu ( ambaye chini ya utawala dhalimu wa makaburu hakuchelea wala kuogopa kupambana nao) vibaraka kwa sababu wamemkemea muuaji Mugabe! Vijana ambao hawastahili kufunga kmba za viatu za hawa wawili! Tusisahau kuwa Nyerere alimkemea Idi Amin kwa kuwafukuza wahindi. Aliita kitendo hicho ni ubaguzi. Leo angefanya hivyo, bila shaka hawa arm-chair revolutionaries wangemwita kibaraka wa watu weupe! Talk is cheap.

Mimi naamini kuwa mpaka hapo tutakapoweza kujitoa kwenye hii bigotry, tutaendelea kuwa na matatizo. Kumchukia mtu kwa sababu tu ndivyo alivyo si kwa watu weupe na wahindi tu. Unakuwa reflected katika jinsi tunavyoangaliana wenyewe kwa wenyewe( kuanzia mjaluo na mkikuyu, mpemba na muunguja, mhutu na mtusi n.k). Tunapokuwa tayari kutetea maovu ya yeyote ambaye tunafanana naye ki rangi, ni hatua fupi hadi hapo tunapofumbia macho maovu ya yeyote yule aliye kabila letu. Bigotry is a slippery slope. Badala ya kujiuliza kwa nini nchi za Asia pamoja na historia yao ( walikuwa maskini kuliko sisi tulipopata uhuru, walipigana vita za muda mrefu na mataifa ya magharibi n.k) leo wanatuacha mbali? Kuna taifa ambalo lina kila haki ya kumchukia mmarekani kama Vietnam? Mbona leo wanashirikiana nae kibiashara? Sisi tumebaki kulalama ( wengi tunaofanya hivyo tunaishi katika nchi za magharibi) na kudai kutokupendwa wakati wenzetu wanatuacha. Wakati umefika wa kumtambua kila aliyezaliwa na aliye na mapenzi na Afrika, bila kujali rangi yake, jinsia,dini yake au upuuzi mwingine kama huo, kuwa ni mwafrika. na kumtenga yeyote atakayemtendea maovu mtu yeyote anayeishi katika bara hili ( kuanzia anayemua bibi kizee Shinyanga hadi anayeangalia wakati wafuasi wake wanaua na kuwatesa raia zake) bila kujali rangi, kabila, jinsia, dini yake hata kama anayefanya hivyo tunafanana nae kwa njia yeyote! Wakati umefika ambapo yeyote atakayechangia kudumisha hali ya maisha ya watu wa Afrika akemewe na kutengwa bila kujali rangi yake, dini yake, jinsia yake n.k. Huyo si mwenzetu. Hastahili sympathy yetu. Wakati umefika wa kukubali mapungufu yetu bila kutumia kisingizio cha kutokupendwa.

Watu kama Mugabe ni lazima tuwatenge na kuwalani! Huyu anayesema amewanyang'anya ardhi watu weupe ( Ndabaningi Sithole naye mweupe?) ili kuwatendea haki watu weusi na badala yake kuwazawadia waovu wenzake! Huyu anayedai kuwa makampuni ya biashara ni lazima yawape asilimia kubwa ya hisa zao watu weusi! Guess who watakaopewa hizo hisa? Huyu aliyewachinja wandebele. Huyu aliyewabomolea makazi wakazi maskini wa Harare kwa sababu tu ya kuwa upande wa upinzani. Huyu anayedai ni Mungu pekee ndiye ana uwezo wa kumnyang'anya urais. Atakapotugeukia huku mikono yake ikitiririka damu na kudai atambuliwe kama kiongozi halali, inabidi watu wote ambao wana mapenzi ya dhati na watu wa Zimbabwe wamkatalie! Ni lazima aonyeshwe kuwa ni pyrrhic victory aliyoipata!

Amandla......!
 
Fundi I have nothing to add to this brilliant and well thought message. Asante sana. I hope kadri tunavyoendelea na huu mjadala tutajigundua sisi waafrika ni watu wa namna gani.

Nikutakie siku njema,

Masanja
 
Fundi Mchundo,gamba la nyoka,kubwa jinga,Masanja,...

..huwezi kuielewa Zimbabwe bila kufuatilia historia yao toka wakati wanapigania Uhuru. tatizo wengi wetu huu mgogoro tunaufuatilia thr BBC peke yake.
 
Mchongoma,
Umesema kwamba sera za MDC zimezungumzia swala la ardhi kama ni mali ya Wazimbabwe wote.. Hilo ni sawa kabisa, ndivyo hata sera za ZANU PF zipo ktk lugha hiyo hiyo ya kutazama Wazimbabwe wote! na kilichotangulia ilikuwa wazungu ambao ni asilimia juu kidogo ya 10 walikuwa na ardhi asilimia 70 hivyo ilikuwa muhimu kuwepo na uuwiano wa umilikaji wa ardhi hiyo... Hizi ni siasa tu hazina ufumbuzi wa swala zima kama hawatazungumzia wamiliki kwa asili zao.
Sasa kinachogomba hapa ni utekelezaji wa azma hiyo.,, Mugabe kachukua ardhi yote ya wale wazungu (ikawa mali ya Taifa) kisha akawapa offer wazungu ku lease ardhi ambayo wanataka kuitumia.. Mzungu hakukubali..
Tunarudi kwa MDC wao wanadai mwenye haki ya kumiliki ardhi ndiye atapewa!... hapa mzungu ndiye mwenye hati na bila shaka ni MZIMBABWE lakini yule mweusi ambaye pia ni MZIMBABWE itakuwa kafungwa na sheria ya kutokuwa na hati ya kumiliki ardhi. Hivyo ile asilimia 70 bado itakuwa mikononi mwa mzungu Mzimbabwe..

Unajua mkuu hata sisi tuna sheria ambazo zinasema kila mtu ana haki ya kuamini dini anayotaka na hata haki zote hua zinaashiria Watanzania wote. lakini inapofikia mgogoro kati ya tuseme Waislaam n Wakristu ni muhimu kabisa maamuzi ya sera inayohusiana na mgogoro wa Waislaam na Wakristu uwe wazi..Sio tena kuzunguka na kusema sera yetu itafuata sheria fulani ambayo haipo!.. na ukaunde tume ambayo haina sheria tayari mkononi. Hata kama unatetea Lets say Maskini (Poor) haina maana unawapinga ama kuwakataa matajiri (rich) utaifa wao.. ni sera ambazo zimelenga kuleta Uuwiano kati ya jamii haina ubaya ukisema chama change kunawakilisha maskini..na sera zako zikawa wazi kuwatetea maskini.

Swala la ardhi Zimbabwe halina sheria inayokubalika pande mbili zote..
1. Kumilikiwa na wenye kibali ama hati inapendelea WAZUNGU...
2. Kumilikiwa na serikali hali wakipewa weusi - inapendelea WEUSI..

Kwa hiyo jibu la MDC nilitegemea lingekuwa katikati kama nilivyotoa mimi mapendekezo ya kuzigawa zile ardhi ambazo mzungu hazitumii kwa kilimo ila ni ktk ukubwa wa eneo analomiliki.. akifanya kuwinda, kulisha farasi wake huku akiweka senyenge zenye maandishi kama Do not Transpass - Private area - you will be shot! Mtu mmoja ana maili 2 nzima za makazi yake.
Lakini MDC walichokifanya ni kutumia ile sheria ya Ian Smith na kusisitiza kuwa weusi watapewa sehemu nyingine ambazo kwa miaka yote iliyopita ndio chanzo cha vita.
 
Amini usiamini hatuangalii BBC peke yake! Wengine wetu tulikuwa watu wazima wakati Ian Smith anatawala. With all due respect, don't insult our intelligence! Ati hatujui historia yao!!!!
 
Wakuu darasa zito sana hili kuhusu Zimbabwe, na heshima kwa wote mnaochangia wallahi elimu safi na ya bure,

Lakini nina swali moja kwa wale mnao onekana kuielewa hii topic zaidi, hivi huyu mpinzani wa Mugabe, akipewa power je ni vyema arudishe ardhi kwa wazugnu ili kuleta amani huko au? maana wengine bado hatuelewi vizuri hapo?

Ahsante Kwa msaaada!
 
Mnajua kuna kitu kimoja ambacho wengi wana'assume' tu. Kuwa hao walionyang'anywa hayo mashamba wako tayari kurudi. Wengi wao wameishaanza maisha mapya Australia, Mozambique na kwingine walikoenda. Kwa wengine itachukuwa muda mrefu sana kurudisha tena imani kwa serikali yeyote ya watu weusi. Wengine toka awali ni wabaguzi na baada ya huu ambao wanaona ni uthibitisho wa unyama wa ngozi nyeupe hawata rudi. Uganda chini ya M7 waliwakaribisha wahindi walionyang'anywa biashara zao kurejea na ni wachache tu waliorejea. Kwa hali hiyo sitoshangaa kama baadhi ya hayo waliokuwa na mashamba, hata wakirudishiwa, wakikataa kuyachukua. Cha msingi ni kurudisha imani kwa raia wote wa Zimbabwe bila kuangalia rangi, jinsia,dini n.k. kuwa haki itatendeka. Wale walionyang'anywa mashamba yao walipwe fidia kwa hasara yao. Wale waliopewa mashamba kwa sababu tu ya ukaribu wao na Mugabe waambiwe walipe thamani ya hayo mashamba. Mashamba yapewe wale wote wenye nia ya kuyaendesha na kuonyesha uwezo wao. Kama ni wakulima wadogo wapewe kiasi watakachoweza kumudu. Wale wenye uwezo wa kilimo cha biashara waruhusiwe kufanya hivyo bila kuangalia rangi au historia yao. Nasema hivi kwa sababu itakuwa tempting sana kulipiza kisasi kwa wafuasi wa Mugabe. Kama mtu anaendeleza shamba lake na anaweza kulilipia, aruhusiwe kuendelea nalo. Serikali ifanye jitihada kuwekeza kwenye elimu na sekta nyingine ili wale ambao hawatapata ardhi waweze kupata ajira.

Lakini ikumbukwe mimi ni Fundi Mchundo mtanzania, si mzimbabwe, mkulima, mwanasiasa, mchumi kwa hiyo inawezekana kabisa yote ninayoyasema humu ni utumbo!
 
Na inawezekana yote unayosema ni ukweli, lakini binafsi ninachukua hii sentesi ya mwisho maana ukweli ni kwamba wengi hapa tunajua machache sana kuhusu Zimbabwe na kinachoendelea sasa,

ingawa pia tunaamini tunajua sana, lakini ukweli hatuelewi mengi, tunayojua ni machache sana ambayo tunayapata kutoka kwenye source zenye sababu mbali mbali kuhusiana na huo mgogoro.

Ahsante Kwa Darasa Wakuu!
 
Lakini ikumbukwe mimi ni Fundi Mchundo mtanzania, si mzimbabwe, mkulima, mwanasiasa, mchumi kwa hiyo inawezekana kabisa yote ninayoyasema humu ni utumbo!

Unajua kabisa kwamba una shusha nondo za nguvu all along kwenye hii mada wa Zimbabwe.

Huku ni kujikweza kwa kujishusha!

(I'm just busting your balls Fundi, just kidding)
 
Zimbabwe's opposition leader Morgan Tsvangirai said in interviews published on Sunday he would push for negotiations with President Robert Mugabe on a new constitution and fresh elections. He also kept open the possibility that Mugabe could remain as a ceremonial head of state.

Speaking ahead of the expected announcement that Mugabe had won re-election in Friday's run-off vote in which he was the only candidate, Tsvangirai said his Movement for Democratic Change (MDC) party would use its parliamentary majority, which it won in elections in March, to force negotiations over a transitional arrangement.

"We must bring the old man to the negotiating table as soon as possible," he was quoted as saying by the Mail on Sunday from Harare. "We have the power to control parliament, and that is recognised even by Mugabe's Zanu-PF ... We must force a transitional agreement for a set time-frame and work towards a new constitution for Zimbabwe.

"I am confident we can achieve that if international pressure keeps up."
In a separate interview to the Sunday Telegraph, Tsvangirai said under such a scenario Mugabe could possibly remain as a figurehead president.
"I don't think it's inconceivable for such an arrangement to include him, depending, of course, on the details of what is being proposed and what are the arrangements."

International condemnation has continued of Friday's vote, which was boycotted by the MDC, with the United States pledging to tighten sanctions against Mugabe's "illegitimate" government. Tsvangirai won the first round of the election, but pulled out of the contest last weekend after nearly 90 MDC supporters were killed in attacks he blames on pro-Mugabe militias.

Source: News24.com
 
Mchongoma,
Umesema kwamba sera za MDC zimezungumzia swala la ardhi kama ni mali ya Wazimbabwe wote.. Hilo ni sawa kabisa, ndivyo hata sera za ZANU PF zipo ktk lugha hiyo hiyo ya kutazama Wazimbabwe wote! na kilichotangulia ilikuwa wazungu ambao ni asilimia juu kidogo ya 10 walikuwa na ardhi asilimia 70 hivyo ilikuwa muhimu kuwepo na uuwiano wa umilikaji wa ardhi hiyo... Hizi ni siasa tu hazina ufumbuzi wa swala zima kama hawatazungumzia wamiliki kwa asili zao.
Sasa kinachogomba hapa ni utekelezaji wa azma hiyo.,, Mugabe kachukua ardhi yote ya wale wazungu (ikawa mali ya Taifa) kisha akawapa offer wazungu ku lease ardhi ambayo wanataka kuitumia.. Mzungu hakukubali..
Tunarudi kwa MDC wao wanadai mwenye haki ya kumiliki ardhi ndiye atapewa!... hapa mzungu ndiye mwenye hati na bila shaka ni MZIMBABWE lakini yule mweusi ambaye pia ni MZIMBABWE itakuwa kafungwa na sheria ya kutokuwa na hati ya kumiliki ardhi. Hivyo ile asilimia 70 bado itakuwa mikononi mwa mzungu Mzimbabwe..

Unajua mkuu hata sisi tuna sheria ambazo zinasema kila mtu ana haki ya kuamini dini anayotaka na hata haki zote hua zinaashiria Watanzania wote. lakini inapofikia mgogoro kati ya tuseme Waislaam n Wakristu ni muhimu kabisa maamuzi ya sera inayohusiana na mgogoro wa Waislaam na Wakristu uwe wazi..Sio tena kuzunguka na kusema sera yetu itafuata sheria fulani ambayo haipo!.. na ukaunde tume ambayo haina sheria tayari mkononi. Hata kama unatetea Lets say Maskini (Poor) haina maana unawapinga ama kuwakataa matajiri (rich) utaifa wao.. ni sera ambazo zimelenga kuleta Uuwiano kati ya jamii haina ubaya ukisema chama change kunawakilisha maskini..na sera zako zikawa wazi kuwatetea maskini.

Swala la ardhi Zimbabwe halina sheria inayokubalika pande mbili zote..
1. Kumilikiwa na wenye kibali ama hati inapendelea WAZUNGU...
2. Kumilikiwa na serikali hali wakipewa weusi - inapendelea WEUSI..

Kwa hiyo jibu la MDC nilitegemea lingekuwa katikati kama nilivyotoa mimi mapendekezo ya kuzigawa zile ardhi ambazo mzungu hazitumii kwa kilimo ila ni ktk ukubwa wa eneo analomiliki.. akifanya kuwinda, kulisha farasi wake huku akiweka senyenge zenye maandishi kama Do not Transpass - Private area - you will be shot! Mtu mmoja ana maili 2 nzima za makazi yake.
Lakini MDC walichokifanya ni kutumia ile sheria ya Ian Smith na kusisitiza kuwa weusi watapewa sehemu nyingine ambazo kwa miaka yote iliyopita ndio chanzo cha vita.

Mkandara unatia chumvi kuhusu MDC, hata siku moja MDC hawajasema ile ardhi itarudishwa kwa wazungu. Ile ardhi ambayo iliynyang'anywa kutoka kwa wazungu ilipewa kwa mawaziri na wanajeshi wakubwa na rafiki za mugabe. MDC wanasema wakiiichukua nchi wataitaifisha ardhi kuwa state owned halafu itakuwa redistributed kwa haki kwa watu wote.[farms were then given to his Cabinet ministers, military leaders and other elite. Hundreds of thousands of farm laborers lost their jobs.
Hadi kesho MDC wanasema wazungu kushika ardhi kubwa kiasi kile ilikuwa ni makosa.
 
Mkuu IO,

Heshima mbele, unayaonenaje haya maneno mapya ya huyo mkuu wa MDC kuwa baada ya kugomea uchaguzi sasa anataka mazungumzo na Mugabe,

na hata kwamba Mugabe aendelee na urais? Naomba darasa mkuu mimi hii topic inanipita pembeni sana?
 
Je..kati Ya Mzungu Na Mweusi Nani Kauwa Watu Wengi Zaidi?
Je Nani Mwene Nyuklia?
Je..hao Waafrika Waliowaua Wenzao Nani Aliwapa Silaha Za Kufanya Hivyo?
Je...nani Aligundua Silaha Za Maangamizi?

Mkuu Mushi,

Nafikiri jibu la swali "waafrika waliowaua wenzao nani aliwapa silaha za kufanya hivyo?" linapatikana kutoka kwa Nyani Ngabu: WAAFRIKA NDIVYO TULIVYO. Ni kweli mzungu ndiye aliyetupa hizi silaha zote zenye maangamizi. Lakini, sisi ni binadamu na tuna akili. Tuna uwezo wa kupambanua mazuri na mabaya, tunajua kuwa kuuana si jambo jema. Sasa pale tunapoamua kuchukua ndoano kutoka kwa hawa wazungu na kukubali kupokea silaha ili tumalizane, hapo kwa kweli hatuna wa kumlaumu ila sisi wenyewe. Tujiulize kwa nini wazungu hawamalizani wenyewe kwa wenyewe? Nafikiri mkuu sisi tuna akili na busara ya kujua jema na baya na tuache kasumba ya kutokuwa responsible na kuwapasia lawama watu wengine.

Tukirudi kwa Mugabe Na Morgan T., maoni yangu ni kuwa whether mmoja wao ni kibaraka na mwingine ni mwanamapinduzi that is not the point. The point is, there are millions of Zimbabweans who are suffering, thousands are dead. Zimbabwe ilipopata uhuru ilikuwa ni moja ya mataifa machache ya Afrika yaliyokuwa yameendelea kuliko mengine. Sasa kwa miaka 28 kama RGM ameshindwa kumaintain au kufanya mambo yawe bora, then it time for him to go. Yeye akiwa katika hatamu nchi nzima ilikuwa katika uangalizi wake na ameshindwa kuendeleza nchi au amezorotesha kilichokuwepo.

Ili kuwapa wananchi wa Zimbabwe haki, Mugabe ni lazima aondoke. Kama mtang'ang'ania kuwa Tsavingirai ni kibaraka, well, yeye basi huenda ni baniani mbaya (kiatu chake ni dawa kwa wazimbabwe).

Suala hili linaniumiza kichwa na kunipa legitimate concerns. Kama kina JK, Mbeki, dos Santos na wengineo hawamkemei Mugabe (the same applies to Museveni), kwangu mimi natafsiri kuwa wanaendorse huo ubabe na udhalimu. Kama wanaendorse hilo, ina maana tusishangae hata wao wakija kubadilika siku moja na kuwa wadhalimu (kitu ambacho sitarajii lakini ya binadamu mengi).

Mugabe alikuwa mpigania uhuru, alifanya mengi kusaidia nchi yake ipate uhuru lakini hiyo si sababu ya kumfanya asiwe held accountable for his actions. Hata Winnie Mandela alikuwa accountable na ANC kwa mauaji yaliyofanyika wakati wa kupigania uhuru. By no means Mugabe is not Hitler, however, just like Hitler, the propaganda was said to be for "the best interest of the masses"
 
Mugabe is just another dictator,he must be defeated...why defend this stupid ambaye ameleta disaster kwenye nchi yake,28 yrs in power? what is he looking for kwani hakuna wengine,no excuse and he should go...i'll be more than happy to see this guy in the Hague akinyea debe for the rest of his life,sijui mnalitetea la nini wakati half of his countrymen end up refugees kutokana na policy zake mbovu.

hivi omar bongo wa gabon yupo madarakani miaka mingapi vile?
mbona hatusikii kelele nyingi kuhusu huyu mkuu? naamini jibu
wengi mnalo.
 
Hata Mugabe alipoua watu 20,000 miaka ya 80, kina Nyerere walimpetesha. Kwa nini?
 
Mkuu Mushi,
Ili kuwapa wananchi wa Zimbabwe haki, Mugabe ni lazima aondoke. Kama mtang'ang'ania kuwa Tsavingirai ni kibaraka, well, yeye basi huenda ni baniani mbaya (kiatu chake ni dawa kwa wazimbabwe).

Suala hili linaniumiza kichwa na kunipa legitimate concerns. Kama kina JK, Mbeki, dos Santos na wengineo hawamkemei Mugabe (the same applies to Museveni), kwangu mimi natafsiri kuwa wanaendorse huo ubabe na udhalimu. Kama wanaendorse hilo, ina maana tusishangae hata wao wakija kubadilika siku moja na kuwa wadhalimu (kitu ambacho sitarajii lakini ya binadamu mengi).

Mugabe alikuwa mpigania uhuru, alifanya mengi kusaidia nchi yake ipate uhuru lakini hiyo si sababu ya kumfanya asiwe held accountable for his actions. Hata Winnie Mandela alikuwa accountable na ANC kwa mauaji yaliyofanyika wakati wa kupigania uhuru. By no means Mugabe is not Hitler, however, just like Hitler, the propaganda was said to be for "the best interest of the masses"

what ur saying above would make sense kama the following prezidos could get the same treatment: hosni mubarak, nguema, omar bongo, paul biya. the people of egypt, cameroon, equatorial guinea, gabon wote wanataka hiyo haki unayoisema hapo juu au wao sio watu na zimbabweans tu ndo watu? all these presidents have been leaders of their countries for more than 25 yrs (and some of em are life presidents..!), kill their citizens and don't allow the opposition a fair game in the so-called democracy. so lets stop that double standard and be real other than kufuata mkondo wa wazungu. itz funny that us afrikans tutampenda kiongozi wa nchi when the western media inapomsifia but wakianza kumchukia basi na sisi tunafuata mkumbo wa kuanza kumchukia.
 
Jamani uovu wa Mugabe usigeuke kuwa siasa za magharibi na mashariki tena.
Huko tulishatoka basi.
Hata wakati ule wa usosharisti najua wazi madikteta wengi ambao baadaye tuligundua janja yao walikuja na story hizi hizi za Marekani na UK.
Ninaamini si Marekani wala Uingereza anayeua wananchi wa Zimbabwe bali ni Mugabe mwenyewe na ushahidi upo.
Kama ni ardhi ya Zimbabwe si walimuachia ardhi? kwani walikwenda nayo hao wazungu wanaolalamikiwa? tena mnakumbuka kwamba waliondolewa kwa fujo na hata wengine kuuwawa na hao wanaojiita maveterani. Watu ambao sisi tulifunga mkanda kwa ajili yao.
South afrika mbona hata baada ya mzungu kusalimu amri bado wanapeta?
Shida za Mugabe ni zake mwenyewe! na one day history will tell the truth.
 
Back
Top Bottom