jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,379
- 25,475
jmushi Kwa Kweli Maswali Yako Yanajieleza Kabisa, Ndio Maana Nilikuwa Nashindwa Pa Kuanzia Kukupa Majibu Yanayojitosheleza, Lakini Hata Hivyo Nitajaribu:
Je Tumsikilize Mkoloni Kwa Kuwa Aliondoka Bila Kupenda? Jibu Kwa Swali Hili Inategemea Kipi Anachotuambia, Kwani Dunia Ni Uwanja Wa Fujo Na Kila Mtu Anatafuta Kipande Chake Cha Keki Kwa Gharama Ya Mtu Mwingine, Hivyo Tujiulize Na Kutafakari Ikiwa Ni Pamoja Na Kuchukua Tahadhari Zote, Kwa Lolote Lile Mkoloni Analojaribu Kutuambia, Hii Ni Pamoja Na Wakoloni Weusi.
Je Ana Nia Nzuri? Jibu La Haraka Kwa Swali Hilo Ni Kuwa Hakuna Mkoloni Mwenye Nia Nzuri Na Koloni Lake, Kwani Uhusiano Wao Umejengwa Juu Ya Mtawala (mtafuta Maslahi) Na Mtawaliwa ( Anayepambana Kulinda Hadhi Na Utu Wake Inapobidi).
Je Walituacha Na Elimu? Jibu Ni Ndio Walituacha Na Elimu, Lakini Kwa Kiwango Gani Na Elimu Hiyo Kwa Ajili Ya Nani, Hili Ni Suala Linalohitaji Mjadala Mwingine; Kwani Ukweli Unajidhihili Kuwa Elimu Iliyotolewa Ni Kwa Ajili Ya Mkoloni Na Kwa Ajili Ya Maslahi Yake, Na Sio Kumkomboa Mwafrika Au Kumsaidia Mwafrika. Haka Kama Elimu Hiyo Ilisaidia Waafrika Ilikuwa Ni Kwa Bahati Tu Na Halikuwa Lengo La Mkoloni.
Vipi Kuhusu Chakula? Mkazo Ulitiliwa Zaidi Kwenye Mazao Ya Biashara Na Suala La Chakula Lilikuwa Sio Kipaumbele Cha Mkoloni.
Je Wanawapenda Waafrika? Sina Hakika, Mkoloni Alikuja Kutafuta Na Suala Kupenda Waafrika Sio Kipaumbele Chake. Tuangalie Jinsi Walivyomuondoa Lumumba Na Kumuweka Mobutu, Angalia Walivyomuondoa Nkrumah Na Kumweka Afifa, Na Sasa Angalia Wanavyotaka Kumuondoa Mugabe Na Kumweka Tsivangilai. Africa Wake Up!!!!
Mpango Wa Kumtoa Mugabe Ni Wa Blair Na Bush...then Nia Yao Nini?
Kuna Anayejua Kuwa Bush Ana Uhusiano Wa Damu Na Familia Ya Kifalme Ya Uingereza?
Kwanini Cia Walimwua Lumumba Na Nkrumah!?
Je..ni Haki Wakimwua Mugabe?
Je..tuwasaidie Kufanya Hivyo?