Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,803
- 11,257
Mkandara.
Kuwa ni mswahili hilo halina shaka. Umekiri kuwa Mugabe ni muuaji na ni kiongozi mbovu. Waliokuwa wakigombea urais huko Zimbabwe ni wawili, Robert na Morgan. Mada hii inadai kuwa watu wa magharibi wanafanya propaganda kumfanya Robert aonekane mbaya bila shaka ili Morgan, unayemuona kuwa ni puppet wao, ashinde. Hili unaona halikubaliki ndio maana tumekesha hapa tukipingana hoja. Mimi nasema Robert kutokana na uovu wake lazima atoke ( by implication si propaganda za watu wa magharibi zinazompakazia bali yeye ni mtu muovu) na ampishe mwingine, hata kama ni Morgan. Wewe unasema Morgan ni kibaraka kwa hiyo kwa vyo vyote vile asipewe urais. Kwa mantik yako mwenyewe ni kuwa kama ni choice kati ya Robert, muuaji na Morgan kibaraka, heri Robert aendelee. Katika hali ya Zimbabwe ilivyo sasa, huku ni kumshabikia Robert. Alternative uliyoitoa ni mwanamke ambaye hata jina humkumbuki! Huyu ambaye hata hajawahi kusimama hadharani kugombea urais. Hata Makoni humzungumzii. Kwa vile unadai mimi napindisha maneno yako, swali rahisi. Kati ya Robert Mugabe na Morgan Tsvangirai, ambao ndio walikuwa wagombea pekee wa urais katika raundi ya pili ya uchaguzi, ni nani unadhani anafaa kuwa rais wa Zimbabwe? mimi nasema Morgan Tsvangirai, kwa sababu kuna kila dalili alishinda ngwe ya kwanza na hata damu mikononi mwake. Mwenzangu unasemaje? Robert au Morgan?