Mkuu hivi unajua Ikulu watumiaji wa Internet ni wangapi? na wana ofisi ngapi?
Nafikiri kwa Tanzania kama either wanamlipa ISP kwa mwaka mzima. Hicho kiasi nafikiri ni sawa kabisa.
Jamani hizo hela si za kwendea internet cafe...au nimeelewa vibaya!!
Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na ukweli kuwa Ikulu hawana hata website kwa kipindi chote hiki ila ni kuwa gharama za Internet zilizoombwa ni kiasi cha shilingi 38,400,000.
Hizi fedha zipo kwenye kifungu 2002 mawasiliano serikalini, kwenye kasma namba 260104 ya kitabu cha bajeti ofisi ya rais ikulu,
wameandika hivi ,nanukuu..Kasma hii hutumika kulipia gharama za mawasiliano ya mtandao kwa njia ya internet .katika mwaka wa fedha 2008-2009 zinaombwa shilingi 38,400,000.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa kama kutuma tuu internet wanahitaji kiasi chote hicho kwa mwaka ni gharama halisi ama ni mchezo wa Salva et all?
Kwa ujumla gharama za mawasiliano ,habari na utoaji huduma zimeobwa kiasi cha shilingi 60,475,000. na hizi ni kwa ajili ya vitu kama gharama za simu 2,400,000,gharama za posta 500,000, Internet 38,400,000,uchapishaji 4,200,000, huduma za utangazaji 12,675,000 na tepu,rekodi na diski 800,000.
Hya angalieni wenyewe jinsi internet inavyokula pesa zetu je wakiweka na website si ndio tutakwisha kabisa?
Hivi mwaka jana walitengewa fedha za Intaneti? na vipi mwaka juzi...?
Hii ni hela ndogo sana kwa internet connection kwa nchi ya Africa Mashariki zinazotumia satellite... acheni ulimbukeni...
Hiyo sio fedha ya webhosting... surely webhosting is cheaper than internet connection...
sasa tumekosa ya kuongea... du!
kasheshe... mwaka jana Ikulu walitengewa fedha za Intaneti.. na mwaka juzi pia.. hizo firewall, na vyombo, nk halafu kuna bajeti ya mawasiliano.. n.k hivi huoni tatizo? Kabla hawajapewa hatu hutu tusenti milioni 38 si wasema hizo nyingine walizopewa walizitumiaje?
Naona Kila Kitu Kinakuwa Siasa Siku Hizi Hata Hii Nayo Imeshakuwa Siasa Kwa Sababu Tu Ccm Ndio Ipo Ikulu , Lakini Wanaoleta Siasa Wanatakiwa Wajue Pale Wafanyakazi Wote Wale Hawako Pale Kwa Sababu Ya Kadi Au Uwanachama Wao Wa Chama Fulani Wale Ni Raia Huru Kitu Chochote Wanachofanya , Kupanga Au Kupangua Wanafanya Kwa Masilahi Ya Sehemu Yao Husika Na Taifa Kwa Ujumla .
Hata Hizo Hela Walizoomba Wameomba Kutokana Na Mahitaji Yao Hapo Walipo Wao Nina Uhakika Watakuwa Wameonana Na Wataalamu Wao Wa Ict Katika Kupanga Mambo Hayo Pamoja Na Wataalamu Wengine Kabla Ya Kuja Na Kitu Kama Hicho
Tuache Zarau Na Kushoboka Hii Sio Siasa Ni Kitu Halisi