Habari zisizo rasmi ni kwamba tovuti ya Ikulu haitakarabatiwa, badala yake, itazinduliwa (sijui lini) tovuti ya JK. Lakini tatizo ni kwamba, kutokana na kuwapo kwa matatizo mengi yanayosababishwa na ufisadi (kuanzia Richmond hadi EPA hadi Chenge na kwingineko), sidhani kama JK atakuwa na ubavu wa kuizindua tovuti yake hiyo.
Yeye ameanisha malengo yake, sera zake, itikadi yake na ya chama chake. Sasa, kila kinachotokea kwenye serikali yake kinakwenda kinyume na itikadi, sera, maoni, visheni, na kadhalika. Ana raha gani kiasi hicho mpaka atangaze mipango yake wakati tayari jahazi linazama, sasa ni suala la kuondoa maji ili lisizame haraka, kwani kasi ya maji kuingia kwenye jahazi imekuwa kubwa. Kila anapofanikiwa kuchota maji yanayoingia kwa kasi kubwa kwenye jahazi lake, na kuziba matundu yanayoingiza maji hayo, akigeuka anakutana na matundu mengine makubwa zaidi, ambayo yanaingiza maji kwa kasi kubwa zaidi. Sasa watu wanabaki kumshangaa... ni nahodha gani huyo ambaye anashindwa kukiongoza chombo chake, kwani inaonekana mabaharia wake wote hawana uwezo wa kumsaidia kukiongoza, kwani wao hawajafuzu ubaharia.
Hiyo meli ya JK sijui itafika lini? Ndege ya nahodha msaidizi wake, EL, tayari ilianguka na kuungua.
Mwenye ramani ya wapi itakapoishia hii meli atuambie. Tuna hamu ya kujua kama itazama au itaingia bandarini salama.
./Mwana wa Haki