Mwanasiasa
Unaposema siyo sahihi lazima utueleze ref. kama katiba au kifungu gani cha sheri. Ukiniambia hicho kitendo hakitendi haki hapo nitakuelewa. Ninavyojua mimi chama tawala kiko juu ya serikali na tunavyopiga kura tunachagua CHAMA siyo mtu na yule mtu anafuata sera za CHAMA siyo sera zake kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi. Ndiyo maana JK aliwaambia wafanyakazi wote wa serikali wanatakiwa wafuate muongozo wa CCM kitu ambacho kinaonekana siyo cha haki lakini kutokana na katiba he was right. Rais na serikali wanatekeleza sera za chama tawala. Rais hana sera zake mwenyewe kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi. Sidhani kama kuna ubaya website ya Ikulu kutoa info cha chama tawala. Hata nyie CHADEMA mkiingia Ikulu siyo vibaya mkaweka info za chama chenu kwenye website ya Ikulu mpaka hapo katiba itakabodalishiwa na kufanya serikali iwe inaundwa na vyama. Nilisoma habari za Mtikila nadhani jana nikaona ana make sense kuhusu suala la Zenji, mtikila amekataa serikali ya mseto kwa kuwa uundaji wa serikali ya mseto ni kitu ambacho kinatakiwa kiwe kwenye katiba kitu ambacho ni kweli kabisa. Kwa hiyo amesema tatizo liko kwenye katiba siyo sehemu nyingine. Lazima tukubali kwamba Sheria/katiba na Haki ni vitu tofauti.