Website ya IKULU na miradi ya COMPUTER ya Serikali

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,869
20,050
Nimegundua kuwa website ya Ikulu (ambayo iko hosted na NTT pale Centennial Colorado) ina page maalumu ya CCM. Je katika nchi ya vyama vingi hiyo kweli ni halali?
 
Mzee ebu tupe link maana ninavyojua mimi website ya ikulu ipo underconstraction.

http://www.statehouse.go.tz/

kama unazungunzia website ya serikali ya jamhuru ya muungano kuna page ambayo inatoa info za vyama vyote vya siasa vilivyosajilia na sidhani kama kuna ubaya wa kuelezea kwa undani habari za chama tawala ili watu wajue serikali inaendeshwa na chama cha namna gani. Kumbuka CCM ndiyo iliyopewa madaraka ya kuunda serikali kwa mujibu wa katiba, kama serikali ingekuwa inaundwa na vyama vyote vya siasa habo ingekuwa issue nyingine.
 
umekosea

website ya ukulu has been on leave for almost MWAKA MZIMA

na huyu JK ndio techie savy president tulienaye

hii ni skendo amablo itabidi tuanzishe separate topic kwani tatizoni kubwa kuliko unavyoliona na lilianzia kwenye website ya BUNGE
 
sam said:
Mzee ebu tupe link maana ninavyojua mimi website ya ikulu ipo underconstraction.

http://www.statehouse.go.tz/

kama unazungunzia website ya serikali ya jamhuru ya muungano kuna page ambayo inatoa info za vyama vyote vya siasa vilivyosajilia na sidhani kama kuna ubaya wa kuelezea kwa undani habari za chama tawala ili watu wajue serikali inaendeshwa na chama cha namna gani. Kumbuka CCM ndiyo iliyopewa madaraka ya kuunda serikali kwa mujibu wa katiba, kama serikali ingekuwa inaundwa na vyama vyote vya siasa habo ingekuwa issue nyingine.

Nafikiri imefungwa muda mfupi tu uliopita labda baada ya mimi kuuliza kuhus CCM kwenye website hiyo. Nilikuwa hapo leo hii jioni (Nov 13) hii nikiangalia namba za simu za Ikulu; ndiyo maana niligundua kuwa iko hosted kupitia network ya NTT huko Colorado. Katika website hii kulikuwa na taarifa mbalimbali za ikulu ambazo sikuzisoma kwa undani. Baadahi ya pages zilikuwa tupu, under construction lakini page nyini zilikuwa active klukiwa na ile iliyosema The Ruling Party. Tatizo langu lilikuwa hapo kwenye ruling party kuunganisha na serikali. Kwa historia ye maiisha chini chama kimopa au chama kushita hatamu tulikuwa hatuoni tofauti kati ya chama na serikali lakini katika maisha chini ya vyama vingi hilo ni kosa kuchanganya mambo ya serikali na yale ya chama. In fact ilitakiwa viongozi wote wa kiserikali wasitumie reseources za serikali kufanyia mambo ya chama ikiwa ni pamoja na magari ya serikali. Ndiyo maana chama kinapata ruzuku ya serkiali ili kuweza kujiendesha. Chama tawala kinakuwa kinatumia mali ya walipa kodi kuliko haki yao kwa kupata ruzuku kwa proportion kubwa halafu tena kwa kupitia mlango wa nyuma kwa kubebwa na serikali!
 
bora hiyo web ya ikulu iwepo tumshauri world travellr wetu moja kwa moja...jana ameingia ktuka asia akpokewa na viongozi ndugu ,jamaa na wananchi likiwemo tinginya rembo moja lililotinga na vogue new model;pale terminal one [namba zipo],likaambulia zawadi kutoka kwa mzee.

ije hiyo web tupanue demokrasia...hata na wanyonge tutasikika.
 
ata kama ikiwepo kwani hiyo web si itakuwa na na moderators amabao wata edit mambo kabla hajaona
 
Sam: Nafikiri sio sahihi website ya ikulu kubeba loaded information kuhusu chama kimoja tu, hata kama ni chama tawala. Chama cha siasa kinapaswa kueleza policy zake kwenye website yake ambayo CCM wanayo. You are just trying to just the obvisouly unjustifiable!
 
Mwanasiasa
Unaposema siyo sahihi lazima utueleze ref. kama katiba au kifungu gani cha sheri. Ukiniambia hicho kitendo hakitendi haki hapo nitakuelewa. Ninavyojua mimi chama tawala kiko juu ya serikali na tunavyopiga kura tunachagua CHAMA siyo mtu na yule mtu anafuata sera za CHAMA siyo sera zake kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi. Ndiyo maana JK aliwaambia wafanyakazi wote wa serikali wanatakiwa wafuate muongozo wa CCM kitu ambacho kinaonekana siyo cha haki lakini kutokana na katiba he was right. Rais na serikali wanatekeleza sera za chama tawala. Rais hana sera zake mwenyewe kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi. Sidhani kama kuna ubaya website ya Ikulu kutoa info cha chama tawala. Hata nyie CHADEMA mkiingia Ikulu siyo vibaya mkaweka info za chama chenu kwenye website ya Ikulu mpaka hapo katiba itakabodalishiwa na kufanya serikali iwe inaundwa na vyama. Nilisoma habari za Mtikila nadhani jana nikaona ana make sense kuhusu suala la Zenji, mtikila amekataa serikali ya mseto kwa kuwa uundaji wa serikali ya mseto ni kitu ambacho kinatakiwa kiwe kwenye katiba kitu ambacho ni kweli kabisa. Kwa hiyo amesema tatizo liko kwenye katiba siyo sehemu nyingine. Lazima tukubali kwamba Sheria/katiba na Haki ni vitu tofauti.
 
Sam usipandishe bure,

Mwanasiasa amesema kuwa siyo sahihi kutumia resources za ikulu kutangaza sera za chama hata kama ni chama tawala, hakusema kuwa ni kinyume cha sheria. Ni kweli hakuna sheria inayosema kuwa kufanya hivyo ni makosa, hata hivyo katiba ya nchi nayo haisemi kuwa serikali itasimimamiwa au itatangaza sera za chama tawala. Kumbukuka kuwa sheria za nchi yetu hutungwa na bunge, hazitungwi na wapiga kura. Baada ya uchaguzi na watu wa CCM kushinda, haikumaanisha kuwa kila walichohubiri wakati wa kampeini inakuwa sheria ya nchi moja kwa moja. Kwa hiyo wananchi wa vyama vingine hawalazimiki kufuata hiyo manifesto. Ili manifesto ya CCM iwe sheria ya nchi, ilitakiwa ipitishewa na bunge kwa cover kama Mwelekea wa Nchi kwa miaka mitano ijayo. Ikisha pitishwa na bunge, inakuwa ni document ya nchi siyo ya chama na hivyo bado hakuna nafasi ya CCM kutangazwa kwenye vyombo vya serikali.


Ni lazima tujenge utaratibu wa kutofautisha mambo ya serikali na ya kisiasa. Pamoja na kuwa rais ni wa CCM na anatekeleza ilani ya CCM aliyotumia katika uchaguzi uliomtia madarakani, akisha kuwa kiongozi wa serikali anawajibika kwa wananchi wote bila kujali itikadi zao.
 
I am confused. What are we talking about? Is it "Is it correct for Ikulu website to host pages for CCM". Well, a website is a collection of pages. Can the collection of pages hosts pages? Absolute No. A server (computer) can host a page or the collection of pages. Let us just talk about what you mean, we all make mistakes. Mwanasiasa amesema siyo halali. Kitu kinakuwa halali kama hakijakatazwa au kimeruhusiwa. Je, ni halali kwa website ya Ikulu kuwa na information za chama tawala. Absolute. Ndiyo maana vyama vya upinzani wakiambiwa waeleze matatizo ya katiba no one makes sense. Guys, let us move to another topic.
 
sam said:
I am confused. What are we talking about? Is it "Is it correct for Ikulu website to host pages for CCM". Well, a website is a collection of pages. Can the collection of pages hosts pages? Absolute No. A server (computer) can host a page or the collection of pages. Let us just talk about what you mean, we all make mistakes. Mwanasiasa amesema siyo halali. Kitu kinakuwa halali kama hakijakatazwa au kimeruhusiwa. Je, ni halali kwa website ya Ikulu kuwa na information za chama tawala. Absolute. Ndiyo maana vyama vya upinzani wakiambiwa waeleze matatizo ya katiba no one makes sense. Guys, let us move to another topic.

Sam sasa unaleta ujuaji wa kitoto kutaka kuvuruga discussion kwa kuchezea maneno yasiyokuwa na substance yoyote. Acha hiyo Kasumba ya kiswahili ya kudhani kuwa ukishajua maneno fulani basi ndiyo unajua encyclopedia yote kichwani. Matumizi sahihi ya maneno website, webpage, server hosting, url and the like hayakuwa point ya discussion hapa and you know it. In any case, if you get confused just as easily as that, then you must have a mental problem; seek professional care.
 
jasusi,
si mchezo wakati wa mapokezi small house alikuja pia akiwa na vogue range rover new model [namba..]wapambe wakapakia mabegi mawili yaliyosheheni zawadi,,,,ndio mafanikio ya ziara zetu,...anyway wanaotetea wanasema pamoja na zipu clinton alifanikiwa sana kuliko huyu bush muhafidhina ,lets wait and see...so na presida wetu sijui anafuata nyayoo
 
hapo nyuma niliandika yanayomsibu bwana JK na PR team yake laini sasa nadhani hali inazidi kutisha na kwa kweli naona hili haliwezi kusubiri

Hivi kwa nini IKULU HAINA/HAIUPDATE WEBSIE YAKE?

Je ni nani communications director wa IKULU? kwa sababu hali hii ya kulipuuza hili inaona inabckfire na sielewi kwa nini wsilisort out oce and for all kwa sababu mimi sipendi kupitia website ya Bwana MARO (ambaye ni manyakazi wa Ikulu) ya KIKWETESHEI kupata taarifa au updates on what the President is up to

Pili naona is not fair kuwalaumu Ubalozi wetu London kwa kutoupdate website yao kwa sababu huyo ASHA ROSE MIGIRO huko Dar naona haoni umuhimu wa FOREIGN kuwa na updated website na inawezekana kuwa HAWAONI UMUHIMU huo lakini ningependa kupata podcast za JK na stream videos

Vile vile kutokana na mijadala inayoendelea kule ETHINKTANKTZ inaelekea kuwa serikali yetu haikuona umuhimu wa kuwa na website na hata hiyo wesite ya BUNGE domain name yake iliwahi kutokwa na watu walioamua kupost mapicha ya uchi..hiii ni aibu kwa serikali ambayo ilikuwa na uwezo wa kulipa pesa na hili likaisha

Na kwa nini mambo ya WEBSITE ya BUNGE aachiwe huyo MJERUMANI?

Unajua hii inatisha na hili kwa kwei sio kosa la JK bali hao wanaotakiwa kuwajibika na kwa kweli inaonyesha jinsi gani walivyokuwa incompetent

hivi hiyo dream ya kuwa na E-GOVERNMENT inaweza kuwa achieved kwa mwendo huu?

Halafu huko Ikulu kwa nini Potraits za rais zinapotolewa zisiwe zinaandikwa PICHA KWA NIABA YA IKULU badaya ya PICHA NA MARO?

Ningeomba IKULU wajibu hizi hoja


by the way TAZAMENI huko Kenya walivyokuwa intouch na wanainchi

http://www.statehousekenya.go.ke/


huko UGANDA tazameni bwana KAGUTA alivyokuwa bize

http://www.statehouse.go.ug/
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema watendaji wa Rais Jakaya Kikwete wanamwangusha katika utendaji wake na kumfanya aonekane kama mbabaishaji.
Akijenga hoja yake, Lipumba alitoa mfano wa wasaidizi wa karibu wa rais wanaotakiwa kuchapisha hotuba zake katika tovuti kuwa hawajawahi kufanya hivyo tangu Juni mwaka huu.

Alisema kutokuwekwa kwa hotuba hizo za Rais Kikwete kwa miezi minne, kunawanyima fursa watu ya kufahamu hali ya maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Tanzania kupitia tovuti hiyo ya serikali.

Alisema hotuba ya mwisho ya Rais Kikwete iliyochapwa katika tovuti ya serikali, ni ya Juni 20, iliyotolewa wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi ya kuhifadhi misitu na wanyamapori.

Pia hotuba ya kiswahili ya mwisho, ni ile aliyoitoa mkoani Dodoma wakati akifungua jengo jipya la Bunge Juni 12 na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari ya mwisho iliyoko kwenye tovuti hiyo ni ya Juni 23, mwaka huu, inayozungumzia "China imeipatia Tanzania Yuan milioni 80".

"Kasi mpya ya wanamtandao haijafika kwenye mtandao wa elektroniki. Hili siyo jambo la mzaha...viongozi wa nchi ambazo Rais anatembelea wanatayarishiwa maelezo ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa hotuba za Rais.

Hivi katika miezi ya Julai, Agosti, Septemba, Oktoba na Novemba, Rais hajatoa hotuba inayostahili kubandikwa kwenye tovuti ya serikali. Wachambuzi wa nje wanaweza kufikiria kuwa Rais wetu ni mbabaishaji tu kumbe anaangushwa na wasaidizi wake," alisema.
................
Full article at: http://www.habaritanzania.com/articles/1670/1/Wasaidizi-wa-Rais-Kikwete,wasaidizi-wake-wakosolewa
 
Back
Top Bottom