Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

Hakuna asiekopa,ila kwa sasa habari za selikari zinazungumziwa zaid kuliko kipindi cha awamu iliopita,hii ni kwa sababu uhuru wa kuzungumza umekuwa huru sana,tofauti na hapo awali
Huo mkopo umefanya nini?na bado watu wanaendelea kukopa
 
Magu ndiye aliyemfunga Mbowe?
 
Kiasi gani kitapelekwa znz?
 
Huwezi kubaki unategemea vikodi vya kipuuzi kwa watu maskini,unaua uchumi wao na kuzidi kulididimiza Taifa.

Hao Waarabu wapunguze mda wa kutoa hizo pesa,miaka mi 5 ni mingi Bora hata watoe ndani ya miaka 3 inamaana tunaweza pata til.2.5 kila mwaka.
 
Unashangaa nini joh?! MITO ,BAHARA,. MAZIWA, MBUGA, MILIMA, MADINI, UTALII.etc.. VYOTE VIMESHINDWA KUTUPA PESA... sa tufanyeje?!
Hivyo vyote bila kubi unlock na kuvijengea mazingira ya kutupa pesa vinakua ni useless.

Imagine hakuna hata barabara za lami kuingia mbuga kama Ruaha,hakuna barabara za lami kifikia kwenye bandari za Ziwa Tanganyika ,hakuna jitihada za kutangaza utalii miaka yote,Rais alipotangaza akabezwa yet watu wanadhani kwa uwepo wake tuu vitaleta utalii,never lazima kutumia pesa kuviganya vilete pesa.

Yet serikali imekopa pesa kuweka mazingira mazuri ya kuimarisha rasilimali watu anakuja mtu anasema madarasa hayana maana.Matokeo yake tuna watu wengi wajinga hakuna tija wanaleta kwenye Nchi.
 
Afadhali hawa wanaokopa na kutangaza kuliko wale waliokopa kimyakimya na kuwaaminisha wadanganyika kuwa wanajenga kwa pesa za ndani ikafika hatua mpaka ya kubadilisha sheria ya takwimu ili Zitto Kabwe aache kuwafumbua macho
 
Kukopa kupo ila matumizi ya mikopo ndio shida…ukikopa bila kuzalisha mkopo utarudije..ndio hichi tunachokishuhudia hapa sasa tunakopa tena ili tulipe mikopo…tutatoboa
Hiyo inafanyika kote,kwa mfano unawekeza afu matarajio hayajafikia lazima utumie mkopo kulipa.

Unafanya investment kwa ku assume at ceteris paribus ikiwa ndivyo sivyo lazima utumie mkopo kulipa.

Kwa mfano tulikopa hapo awali kuwekeza sehemu then covid ikaja ikavuruga mipango lakini deni linaiva, unadhani njia rahisi ni nini? Ni Kukopa na kulipa deni la awali huku unasogeza mda wa deni mpya,hii ni kawaida .

Kila Nchi wanakopa,imagine Nigeria yenye mafuta mengi Afrika lakini mikopa kama kawa,tena Nigeria hapo kakopa bil.450 tuu .

 

Yani umeongea ujinga wa jumla sio rejareja.
Taifa lingefika pabaya kivipi, nahao unaowataja wanahusiana nini na mikopo, huyo bashite alisha wekwa nje sa system na magu.

Unaacha kutoa hoja ya kujadili hali ya sasa unachanganya changanya maneno yasiyo eleweka.
 
Mkuu siyo kila kitu ni kwa kila mtu, kama hujaelewa jua siyo level yako. Level zingine ni kwa IQ kubwa na siyo kama yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…