Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

Hakuna asiekopa,ila kwa sasa habari za selikari zinazungumziwa zaid kuliko kipindi cha awamu iliopita,hii ni kwa sababu uhuru wa kuzungumza umekuwa huru sana,tofauti na hapo awali

Nop yaani ndani ya kipindi cha miezi 9 amekopa zaidi ya 10% ya fedha yote ya mkopo tokea awamu ya kwanza
 
Ukitoka huo mkopo ina maana ndani ya miezi 9 tutakua tumekopa 17trilion kama deni la nje. Hio trend unaona nzuri? Magufuli alikopa kwa akili na vitu alivyofanya vimeonekana.

Hiyo lugha ya vitu vimeonekana naona iliwaingia sana, sasa ndio mnatulisha wote, hivyo vitu vinaendana na alichokopa?
 
Mkuu ndiyo maana wanasema tenda mema ukiwa hai ili ukisepa watu wakuongelee mazuri. Hata Nyerere mpaka leo anaongelewa, ishu ni kuwa unaongelewa kwa mabaya au mazuri. Jiwe alikuwa muuaji na muongo sana ndiyo maana anaongelewa kwa mabaya.
Muuaji alimuua nani? Uongo upi alioufanya? Acheni chuki na propaganda za kipumbavu Kwa kipindi cha Miaka 5, Magu amefanya Maendeleo makubwa kuliko awamu zote. Kama alikopa basi kilichofanyika kinaonekana kwa macho. Meli zimejengwa kwenye maziwa yote, SGR, Stieglers Gorge, lami mpaka Barabara za mitaani tena zenye viwango, madaraja, magati kwenye Bandari zetu, mambo ni mengi sana.
 
Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takriban Shilingi Trilioni 7.

Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.


F4EA5E5F-CE0F-418A-8F8D-B6B95BAC9404.jpeg
 
Wakati washindani wa Tanzania kwenye biashara ya Logistics wakikopa kwa njia ya ku engage China Ili wajenge reli na miundombinu mingine ,huku Tanzania kuna Watu wenye akili mdogo hawataki.

Hata Kodi kulipa hawataki sasa unajiuliza Labda watapata maendeleo kwa kushushiwa na mvua.Ni hatari Sana kuwa na Nchi yenye Watu wenye akili kiduchu na mdomo mkubwa kama Tzn.

Matunda ya Ziara ya Foreign Minister wa China Kwenye baadhi ya Nchi za Africa.China imepanga kujenga reli ya sgr kutoka mpakani mwa Kenya/Uganda hadi Rwanda na DRC.

Kutoka Djibouti hadi Ethiopia ndani kabisaa.Watatumia model ya Belt and Road Initiative.

Ngoja Tzn tuendelee kujivuta na kubishana ujinga.

View attachment 2077682

View attachment 2077683

View attachment 2077684
Na kitendawili cha mama wameshindwa kukitegu!"KUNA KIJUGU CHAPWAGA BILA YA MOTO JIKONI,SASA SIJUI KITAPWAGA NA NINI?" Kifupi nchi haina fedha za kuikamilisha miradi na chungu ni lazima kipwage.
 
Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takriban Shilingi Trilioni 7.

Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.

https://www.bloomberg.com › articles
Tanzania to Get $3 Billion in Loans, Grants From Arab Lender


11 Dec 2021 — The decision was reached following talks between Tanzania's Finance Minister Mwigulu Nchemba and the lender's Director-General Sidi Ould Tah ...


16 December 2021
Abu Dhabi, UAE

FEDHA ZAIDI ZA KUKAMILISHA MRADI MZIMA WA UJENZI WA RELI MPYA SGR ZASAKWA

Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba na ujumbe wake wapo Abu Dhabi UAE kusaka fedha za kugharamia miundo mbinu ikiwemo michepuko ya mtandao wa reli mpya SGR kama kipande cha Tabora Kigoma n.k ( Source ITV Tanzania news)
Source : Kwa kirefu : (Habari na Picha ,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha na Mipango-Abu Dhabi)

……………………………………………….

Na Benny Mwaipaja, Abu Dhabi

SERIKALI ya nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya Abu Dhabi imeahidi kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na kijamii na Serikali ya Tanzania ili kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan, baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliowasilishwa kwake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Ikulu ya nchi hiyo.

Akizungumza baada ya mazungumzo yao ya faragha, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Sheikh Mansour ameahidi kutuma ujumbe maalum nchini Tanzania kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa hivi sasa na mingine mipya kwa ajili ya kutoa fedha.

Dkt. Nchemba aliitaja miradi iliyowasilishwa kwa Serikali ya Abu Dhabi kuwa ni ile ya uendelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Nishati ya Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere JNHPP Rufiji, ujenzi wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, kilimo na uvuvi pamoja na elimu.

“Kwenye sekta ya elimu tumejenga madarasa mengi, tumejenga vituo vya afya vingi sana na vingine viko vijijini lakini hatujajenga nyumba za watoa huduma wanaotakiwa kufanyakazi kwenye maeneo hayo” alisema Dkt. Nchemba.
Pia waziri huyo wa fedha wa Tanzania alifika katika Kasri ya Al Watan (Qasr Al Watan) na kuwasilisha Salaam kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwenda kwa mwana wa mfalme wa Abu Dhabi His Highness Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan aliye pia naibu amiri jeshi mkuu wa majeshi (Crown Prince of Abu Dhabi and Deputy Supreme Commander of the Armed Forces).



medium_2021-12-16-b52b50b51d.jpg

His Highness Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Crown Prince of Abu Dhabi and Deputy Supreme Commander of the Armed Forces, received a written message from Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of Tanzania, regarding the development of relations between the two countries.
The message was received by His Highness Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan, Deputy Prime Minister and Minister of Presidential Affairs, when His Highness received today at Qasr Al Watan His Excellency Mwigulu Nchemba, Minister of Finance and Planning of Tanzania.
During the meeting between His Highness and the Tanzanian delegation, they discussed the friendly relations between the UAE and Tanzania, development opportunities, economic partnership and enhancing trade exchange between the two countries .

Source : Mohamed bin Zayed receives Tanzanian President's note
 
Hapo la kulaumiwa ni bunge, yaani unakuta mbunge naye anasikia tu taarifa hizo kama mkulima aliyoko kijijini!!yaani kinachobakia ni jinsi waziri wa fedha atakavyosema, akisema ni msaada sawa tu kumbe ni mkopo!!halafu uniambie waafrika tuko sawa sawa kulinganisha na wazungu!!
Bunge lilishapitisha kitambo.
 
Yaani huyu bibi hana maana! Trillion saba anakopa ukijuisha hapo na mikopo kibao ameshakopa anakimbilia trillion 15 halafu kwa vile CCCM mengi ni makondoo yanashangilia! Pesa zaidi ya trillion mbili hapo lazima ziende Zanzibar! Wadanganyika wanatoa macho!
Mama muhuni huyu
 
Ukiambiwa na nani kwamba tozo no kwa ajili ya madarasa tuu? Shida serikali inapo table bajeti huwa mko busy kusikiliza ujinga na umbea wa machadema.

TOzo ina Kazi nyingi kama barabara Vijijini,maji,vituo vya afya na madarasa pia.
Mama anataka kufikisha Til 2.5 kwa mwezi
Very stupid pato la taifa limeshuka makusanyo yameshuka ndiyo sababu anategemea mikopo hadi jana makusanyo ya mwezi yamepungua na kuwa 46% tukifika mwezi wa 8 mwaka huu makusanyo ya mwezi yatakuwa 30% tu
 
Magufuli ameacha deni la sh. Ngapi? Na mbna waziri wa Fedha kipindi hicho alikua anatoa takwimu za deni la Taifa? Ukiona jambo linaongelewa sana ujue kuna shida- Akili mtu Wangu
Ndani ya miezi 9 amevuka nusu ya deni la JPM la miaka 6…hili unaliongeleaje..
Na Magufuli ambae ndani ya miaka mitano amekopa kiasi sawa na alichokopa Jakaya kwa miaka kumi nalo unaliongeleaje?
 
Mama anataka kufikisha Til 2.5 kwa mwezi
Very stupid pato la taifa limeshuka makusanyo yameshuka ndiyo sababu anategemea mikopo hadi jana makusanyo ya mwezi yamepungua na kuwa 46% tukifika mwezi wa 8 mwaka huu makusanyo ya mwezi yatakuwa 30% tu
Kwa upande wa makusanyo kushuka chanzo cha data zako ni nini?
Acha uongo.

TRA wanazungumzia kuvunja record wewe nae unakuja na yako.

Zungumzia kukopa labda utakuwa na ufahamu maana mama Hana siri anaweka wazi mikopo yake.
 
Hawa wanasiasa wa Lumumba is beyond me.

Week aijaisha toka speaker wa bunge kujiuzulu kwa sababu ya kulaumu mikopo.

Na kuna watu wengi wanaodhani alikuwa na hoja; ata vuguvugu alijatulia waziri anapost akikimbizia mkopo wa trillioni 7. Huku sasa si ku justify speaker alikuwa sahihi.

Kuna ulazima kweli wa kuutangazia umma kila mara serikali inapokopa.

Only in Tanzania
 
Matumizi mzee…huwezi kuwa unajenga halafu unaendelea kula bata na kwenda vacation…
Hapo sasa !! Ndio huwa tunasema kila mara kwamba sisi kama Taifa kwa udogo wetu haiwezekani eti tuwe tunafanya kazi na kula bata !! Wanasemaga eti " kazi na Bata " !! Haiwezekani haiwezekani hata siku moja !! Falsafa ya kazi na bata katika hizi nchi ambazo tunasema bado ni changa kiuchumi ! Kazi na bata ni sawasawa na kutwanga maji kwenye kinu !!
 
Magufuli alikopa kwa akili!
Kukopa kwa akili maana yake nini?

Magufuli alikopa halafu akawa anaturubuni kila Jambo analolifanya ni kwa pesa zetu ilihali deni la taifa linakuwa.

Kinachomgharimu mama ni uwazi si vinginevyo.
Magufuli alikuwa anakopa kutoka mabenki ya ndini zaid ya kutoka nje; unakumbuka hii hapa?

 
Hakuna asiekopa,ila kwa sasa habari za selikari zinazungumziwa zaid kuliko kipindi cha awamu iliopita,hii ni kwa sababu uhuru wa kuzungumza umekuwa huru sana,tofauti na hapo awali
Kukopa siyo tatizo tatizo lina kuja hatuo matumizi ya mkopo Bora magufur alikopa tumeviona vitu alivyo viacha ata tukiambiwa mnadaiwa mlikopa pesa mkajenga reli, bwawa la umeme, daraja la surrender, busisi, barabara Morocco, kimara tutakubali kulipa kwakuwa vutu vipo tuna viona na tuna vitumia
 
Back
Top Bottom