BAJETI YA SERIKALI 2022/23: Mwigulu Nchemba akitoa Taarifa kuhusu hali ya Uchumi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,965
Tufuatilie hapa kwa taarifa zote kuhusu bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajia kusoma bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23 leo Juni 14, jioni bungeni. Bajeti inayopendekezwa ni Tsh. Trilioni 41.9 ikiwa ni ongezeko la 16% ukilinganisha na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22.

Kati ya matarajio ya bajeti ya mwaka 2022/23 ni Pamoja na ongezeko la bajeti ya kilimo kwa 155% na ongezeko la kima cha chini cha mishahara. Pamoja na chanzo kipya cha mapato cha kodi ya huduma za mtandaoni.

Kwa taarifa Zaidi kwa yatakayopatikana endelea kufuatilia uzi huu Mwigulu akianza kazi yake bungeni

Waziri Mwigulu Nchemba amesema Vipaumbele vya mwaka huu ni Mifugo, Kilimo na Uvuvi amesema hayo akitoa hoja bungeni.

Dkt. Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha): Sote tunafahamu Nchi yetu na dunia kwa ujumla inaendelea kushuhudia athari za UVIKO-19 ambazo zimesababisha kushuka kwa shughuli za kiuchumi duniani zikiwemo uzalishaji, biashara za ndani, utalii na usafirishaji wa bidhaa.

Dkt. Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha): Katika mwaka 2021, Uchumi wa Taifa letu na dunia kwa ujumla ulianza kuimarika baada ya kupitia kipindi cha kukabiliana na athari za UVIKO-19

Wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuimarisha Uchumi, iliibuka vita ya Urusi na Ukraine

Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha): Vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi vimepelekea kupanda bei za bidhaa mbalimbali ktk soko la dunia zikiwemo mafuta na gesi

Kumekuwa na uhaba wa baadhi ya bidhaa katika soko la dunia ikiwemo mbolea, ngano na mafuta ya kula

Dkt. Mwigulu Nchemba: Serikali imeendelea kuchukua hatua kukabiliana na athari hizo ikiwemo kupokea mkopo wa masharti nafuu wa Trilioni 1.3 zilizoelekezwa kwenye Sekta za Afya, Eimu, Maji na Utalii ili kuchochea Uchumi

Kingine ni kuongeza Bajeti ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Dkt. Mwigulu Nchemba: Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2022/23 imeandaliwa kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria vya uchumi

Maandalizi ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa yamezingatia vipaumbele vya Serikali

Dkt. Mwigulu Nchemba: Katika kutekeleza Mpango wa 2022/23, msukumo mkubwa utawekwa katika sekta za uzalishaji ambazo ni Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Nishati kwani sekta hizi ndizo zinazochochea uzalishaji na huzalisha ajira zinazowagusa wananchi wengi

Dkt. Mwigulu Nchemba: Serikali itaendelea na utekelezaji wa Miradi mingine ya kimaendeleo ikiwemo Miradi ya kielelezo kama Ujenzi wa SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, uboreshaji wa Shirika la Ndege pamoja na miradi ya Afya, Maji, Usafiri wa Anga/Majini, Bandari, Barabara na TEHAMA

Dkt. Mwigulu: Kwa upande wa Mwenendo wa Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2021, Taarifa ya IMF ya Aprili 2022 inaonesha Uchumi wa Dunia uliimarika kufikia wastani wa 6.1% ikilinganishwa na ukuaji hasi wa 3.1% Mwaka 2020

Kuimarika kulitokana na Hatua za Nchi mbalimbali kuimarisha Uchumi

Dkt. Mwigulu Nchemba: Uchumi wa Dunia unatarajiwa kupungua na kufikia ukuaji wa 2.6% Mwaka 2022

Hii inatokana na vita ya Urusi na Ukraine iliyosababisha kuongezeka bei za Vyakula na Nishati, hivyo kudhoofisha matarajio ya kurejea kwa shughuli za uchumi zilizoathiriwa na Corona

Dkt. Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha): Katika mwaka 2021, Uchumi wa Taifa letu na dunia kwa ujumla ulianza kuimarika baada ya kupitia kipindi cha kukabiliana na athari za UVIKO-19

Wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuimarisha Uchumi, iliibuka vita ya Urusi na Ukraine

Dkt. Mwigulu Nchemba: Kufikia mwaka 2023 na kuendelea, Uchumi wa Dunia unatarajiwa kupungua zaidi na kufikia ukuaji wa wastani wa 3.3% kwa kipindi cha muda wa kati iwapo vita ya Urusi na Ukraine itaendelea, na kuzidisha vikwazo vya kiuchumi kwa Nchi ya Urusi

Dkt. Mwigulu Nchemba: Kwa upande wa Uchumi wa Afrika na kikanda, mwaka 2021, Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zilikuwa wa ukuaji wa wastani wa 4.5%

Hii inatokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ikiwemo kuboresha Huduma za Afya na kuimarika kwa Bei za Bidhaa

Dkt. Mwigulu Nchemba: Ukuaji wa Pato la Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulikuwa 5.9% kwa Mwaka 2021 ikilinganishwa na ukuaji hasi wa 1.1% wa 2020

Ukuaji chanya umetokana na kulegezwa masharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya COVID-19 na hatua za Kisera na Kibajeti

Dkt. Mwigulu Nchemba: Ukuaji wa Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 ulikua kwa 4.9% ikilinganishwa na ukuaji wa 4.8% mwaka 2020

Ongezeko limetokana na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa Serikali ikiwemo ikiwemo uwekezaji wa kimkakati ktk Miundombinu ya Nishati, Maji, Afya, Elimu

Dkt. Mwigulu Nchemba: Pato ghafi la Taifa lilikuwa Trilioni 161.5 kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na Trilioni 152.1 kwa mwaka 2020

Kwa mwaka 2021, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu Milioni 57.7 ikilinganisha wa Milioni 55.9 mwaka 2020

Dkt. Mwigulu Nchemba: Mfumuko wa Bei ulifikia wastani wa 3.8% Aprili 2022 ikilinganishwa na 3.3% Aprili 2021

Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kulichangiwa na sababu zilizo nje ya udhibiti wa kibajeti/kisera zikiwemo kuvurugika mnyororo wa uzalishaji na usambazaji bidhaa

Dkt. Mwigulu Nchemba: Mikopo kwa sekta binafsi inaendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha kutokana na Sera wezeshi za kifedha na kibajeti

Mikopo kwa Sekta Binafsi ilikua kwa wastani wa 8.4% katika kipindi cha Julai 2021 - Aprili 2022

Dkt. Mwigulu Nchemba: Mikopo kwa sekta binafsi inaendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha kutokana na Sera wezeshi za kifedha na kibajeti

Mikopo kwa Sekta Binafsi ilikua kwa wastani wa 8.4% katika kipindi cha Julai 2021 - Aprili 2022

Dkt. Mwigulu Nchemba: Thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola za Marekani imeendelea kuwa Tulivu

Dola 1 ilibadilishwa kwa wastani wa Tsh. 2,308.87 ktk soko la jumla kwa kipindi cha Julai 2021 - Aprili 2022 ikilinganishwa na wastani wa Tsh. 2,309.48 Julai 2020 - Aprili 2021

Dkt. Mwigulu Nchemba: Hadi Aprili 2022, Deni la Serikali lilikuwa Tsh. Trilioni 69.44 ikilinganishwa na Trilioni 60.72 za kipindi kama hicho mwaka 2021, sawa na ongezeko la 14%

Katika kiasi hicho, deni la nje lilikuwa Trilioni 47.07 na la ndani lilikuwa Trilioni 22.37

Dkt. Mwigulu Nchemba: Ongezeko la deni la Serikali limetokana na kupokelewa kwa mikopo kutoka vyanzo vyenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo hapa nchini
 

Attachments

  • HOTUBA_YA_HALI_YA_UCHUMI_WA_TAIFA_KATIKA_MWAKA_2021_NA_MPANGO_WA.pdf
    275.9 KB · Views: 23
Bajeti kuu inasomwa mkuu yupo kuuza nchi
20220614_102117.jpg
 
Waziri wa fedha Dr Mwigullu amesema chini ya uongozi mahiri wa mama Samia na CCM kwa ujumla Thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dollar ya Marekani imeongezeka kwa 0.03%

CCM oyeeee

Source Star tv bungeni
 
Hapo anaenjoy balaa
Maskini mna shida sana tena mnoo mnaumiaaa......mnataka abebe sijui vyuma! Asote mijasho ndo mfurahi??....ana enjoy nini?? wkt hata chai ya maziwa/nyama/sukari/pombe/sigara/naniliu .... mwili ulisha kataa???... Taabu taabu zebu kuleee!
 
Back
Top Bottom