ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,114
- 49,840
Kazi inaendelea,
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania na Wizara ya Fedha Kupitia Waziri Mwigulu zimesaini mkopo wa Dola mil. 560 sawa na shilingi Trilioni 1.3.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa ni kwamba mkopo huo ni kwa ajili ya Miradi ya Maji na Afya ya mama na mtoto.
====
Wizara ya Fedha na Mipango, imesaini mikataba wa miwili na Benki ya Dunia (WB), yenye thamani ya Sh1.264 trilioni kwa ajili ya kuboresha huduma endelevu za maji, usafi wa mazingira vijijini pamoja na afya ya mama na mtoto.
Mkataba huo umesaini leo Jumanne Februari 28, 2023 kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi Mkazi wa WB, Nathan Belete na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dk Amour Suleiman Mohamed.
Dk Nchemba amesema mkataba huo umekwenda sambamba na msaada wa jumla ya dola za Marekani 29.93 milioni (Sh68.78 bilioni) zitakazotekeleza miradi hiyo kwa mustakabali wa maendeleo ya Watanzania.
"Mpango endelevu wa maji na usafi wa mazingira vijijinj utapokea Sh689.51bilioni ambao ni mkopo wa masharti nafuu wa IDA, eneo la mradi wa afya ya mama na mtoto litapokea Sh574.59 bilioni," amesem Dk Nchemba.
Belete amesema WB inajisikia faraja kuisadia Tanzania katika kuboresha sekta hizo ikiwemo ya afya ili kuhakikisha Taifa hili linafikia malengo yake hasa kuwezesha huduma bora ya afya ya mama na mtoto.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema fedha hizo zitaboresha huduma za afya mama na mtoto, pamoja na ujenzi wa vituo vya upasuaji sambamba na kuwajenga uwezo watumishi wa kada ya afya.
Naye, Dk Mohamed amesema fedha hizo zitaleta mabadiliko katika sekta ya afya Zanzibar hasa katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto visiwani humo vinavyotokana na changamoto za afya