Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takriban Shilingi Trilioni 7.

Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.

20220112_065951.jpg
 
Mwigulu anajaribu kuepusha lawama, hizo pesa naamini ni za mkopo lakini kwasababu anajua walishaambiwa kukopa sio sifa wakamsuta aliewaambia, matokeo yake ndio haya anachanganya maneno "mkopo" na "msaada" kwenye sentensi moja.

Haya ndio matokeo ya kujibu hoja kwa mipasho, kama ile hoja ya Ndugai ingejibiwa vizuri watu waridhike leo Mwigulu asingekuwa na hiki kigugumizi cha kuandika, lakini kwasababu waliamua kumsuta, sasa ndio wanaishi kwa hofu, mwisho wa ubaya....
 
Mwigulu anajaribu kuepusha lawama, hizo pesa naamini ni za mkopo lakini kwasababu anajua walishaambiwa kukopa sio sifa wakamsuta aliewaambia, matokeo yake anachanganya maneno "mkopo" na "msaada" kwenye sentensi moja.

Haya ndio matatizo ya kukimbia kujibu hoja kwa hoja, kama ile hoja ya Ndugai ingejibiwa vizuri watu waridhike, leo Mwigulu asingekuwa na hiki kigugumizi cha kuandika, lakini kwasababu waliamua kumsuta, sasa ndio wanaishi kwa hofu, mwisho wa ubaya....
Ndungai ni mtu wa kupuuzwa, uzuri ameshapuuzwa tayari. Magu alikopa alivyojisikia na yeye ndiyo kwanza akaja na ile kauli yake ya atake asitake.......
 
Ndungai ni mtu wa kupuuzwa, uzuri ameshapuuzwa tayari. Magu alikopa alivyojisikia na yeye ndiyo kwanza akaja na ile kauli yake ya atake asitake.......
Yaani huyu bibi hana maana! Trillion saba anakopa ukijuisha hapo na mikopo kibao ameshakopa anakimbilia trillion 15 halafu kwa vile CCCM mengi ni makondoo yanashangilia! Pesa zaidi ya trillion mbili hapo lazima ziende Zanzibar! Wadanganyika wanatoa macho!
 
Mwigulu anajaribu kuepusha lawama, hizo pesa naamini ni za mkopo lakini kwasababu anajua walishaambiwa kukopa sio sifa wakamsuta aliewaambia, matokeo yake anachanganya maneno "mkopo" na "msaada" kwenye sentensi moja.

Haya ndio matatizo ya kukimbia kujibu hoja kwa hoja, kama ile hoja ya Ndugai ingejibiwa vizuri watu waridhike, leo Mwigulu asingekuwa na hiki kigugumizi cha kuandika, lakini kwasababu waliamua kumsuta, sasa ndio wanaishi kwa hofu, mwisho wa ubaya....
Hivi kwa akili ya kawaida hii miradi mikubwa iliyoanzishwa toka awamu ya kwanza itaishaje bila fedha ya kutosha? Wakati inaanzishwa watu walishangilia kila siku kishindo Cha awamu ya tano. Maji umeyavulia nguo sharti uyaoge. Ilikuwa Bora kutokuanzisha chochote kabla ya kujiridhisha na uwezo wetu wa kifedha kwanza.
 
Matumizi mzee…huwezi kuwa unajenga halafu unaendelea kula bata na kwenda vacation…
 
Ukitoka huo mkopo ina maana ndani ya miezi 9 tutakua tumekopa 17trilion kama deni la nje. Hio trend unaona nzuri? Magufuli alikopa kwa akili na vitu alivyofanya vimeonekana.
Magufuli alikopa kwa akili!
Kukopa kwa akili maana yake nini?

Magufuli alikopa halafu akawa anaturubuni kila Jambo analolifanya ni kwa pesa zetu ilihali deni la taifa linakuwa.

Kinachomgharimu mama ni uwazi si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom