Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

Mwigulu anajaribu kuepusha lawama, hizo pesa naamini ni za mkopo lakini kwasababu anajua walishaambiwa kukopa sio sifa wakamsuta aliewaambia, matokeo yake ndio haya anachanganya maneno "mkopo" na "msaada" kwenye sentensi moja.

Haya ndio matokeo ya kujibu hoja kwa mipasho, kama ile hoja ya Ndugai ingejibiwa vizuri watu waridhike leo Mwigulu asingekuwa na hiki kigugumizi cha kuandika, lakini kwasababu waliamua kumsuta, sasa ndio wanaishi kwa hofu, mwisho wa ubaya....
Hapo la kulaumiwa ni bunge, yaani unakuta mbunge naye anasikia tu taarifa hizo kama mkulima aliyoko kijijini!!yaani kinachobakia ni jinsi waziri wa fedha atakavyosema, akisema ni msaada sawa tu kumbe ni mkopo!!halafu uniambie waafrika tuko sawa sawa kulinganisha na wazungu!!
 
Hakuna asiekopa,ila kwa sasa habari za selikari zinazungumziwa zaid kuliko kipindi cha awamu iliopita,hii ni kwa sababu uhuru wa kuzungumza umekuwa huru sana,tofauti na hapo awali
Issue ni unakopa kufanya nini???????? Si unakopa kununua barakoa au kujenga madarasa bali unakopa kumalizia bwawa la umeme au SGR ili baadaye unachokifanya kiweze kuzalisha. Madarasa unatumia kodi au tozo au kama hazitoshi unatengeneza temporary Shelters watoto wanasoma wakati ukitafuta pesa ya kujenga madarsa. Kwanini hamuelewi ndugu zangu!!!!!!
 
Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takribani Shilingi Trilioni 7.

Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.
View attachment 2077645
Duh,yaani bado wanaendelea kukopa?
 
Hivi kwa akili ya kawaida hii miradi mikubwa iliyoanzishwa toka awamu ya kwanza itaishaje bila fedha ya kutosha? Wakati inaanzishwa watu walishangilia kila siku kishindo Cha awamu ya tano. Maji umeyavulia nguo sharti uyaoge. Ilikuwa Bora kutokuanzisha chochote kabla ya kujiridhisha na uwezo wetu wa kifedha kwanza.
Wapunguze matumizi serikalini ili wapunguze kukopa!
Unataka maendeleo huku matumizi makubwa unategemea nn
 
Acha kujivua nguo mkuu, haya yote ni athari za Jiwe, japo ni ngumu sana kwa wewe kuelewa, jamaa ameleta maafa makubwa sana nchini. Ndiyo maana hata Mungu akaingilia kati kwani bila hivyo taifa kama taifa tungefika pabaya sana. Ukitaka kumjua vizuri Jiwe angalia watu wake wa karibu kama Bashite, Saambaya,Gamboshi, Ndungai, mzee wa jalalani na wengine wengi tu.
Hayo ndio majibu ya hoja iliyopo?

Muda ni mwalimu mzuri sana!
 
Duh!
IMG_20211227_235915.jpg
 
Mkuu ndiyo maana wanasema tenda mema ukiwa hai ili ukisepa watu wakuongelee mazuri. Hata Nyerere mpaka leo anaongelewa, ishu ni kuwa unaongelewa kwa mabaya au mazuri. Jiwe alikuwa muuaji na muongo sana ndiyo maana anaongelewa kwa mabaya.
Alimuua nani?

Na aliua kumzidi nani?
 
Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.
Tunaomba kujua unafuu (usoft ) wa masharti ya mkopo huu. Yatajwe hadharani moja baada ya lingine.
 
Sisi wa kukopa sisi kweli? Ni lini tutatumia pesa zetu kufanyaa maendeleo? Ipo siku nchi itapigwa mnada- ndugai
😂😂😂😂 Tanzania hii ya miaka 60, Ni lini tutatumia pesa zetu kufanya maendeleo_ Kizungu kidogo_ AND HOW?
Ndugai Nouma sana.
 
Mapema leo nimefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Dkt. Sidi Ould Tah, Mkurugenzi Mkuu wa @badeabank kujadili namna ya kuharakisha upatikanaji wa fedha za mkopo nafuu na msaada Dola Bilioni 3 sawa na takriban Shilingi Trilioni 7.

Benki ya BADEA iliahidi kuipatia Tanzania mkopo huu wa masharti nafuu (soft loan) katika kipindi cha miaka mitano ijayo, zitakazotumika kwenye miradi ya maendeleo sambamba na kuiwezesha sekta binafsi.

Zenji wanslamba 50% ya mikopo wakati ni ndogo mara 10 ya mkoa wa morogoro
 
Back
Top Bottom