Hivi kwa nini TUTUMIE cards zenye microchip? Mimi nafikiri kwa nchi masikini kama Tanzania laminate cards inatosha. Bei yake ni karibu na bure. Ila tu ni kukomputerise huo utambulisho wa wahusika NA HAPO ITACHUKUA BILLION KIDOGO SANA.Sidhani wakati wote unahitaji local professionals kufanya kazi.Kuna suala la security na ufichaji teknolojia watu wasiibe wakaanza kuvitengeneza ovyo.
Swali ni je Mpiga chapa wa serikali anayo credibility ya kuficha siri ya tecknolojia yake ya kuchapisha document za siri? Wafayakazi wake waweza aminika na wana historia ya uaminifu wa kuficha siri na kutochapisha vya ziada na kuwapa wageni mamluki?
Documents nyingi zenye features za siri zikiwemo passport,fedha,cheki na kadhalika za nchi nyingi tu duniani huchapishwa na nchi nyingine si kuwa wataalamu wanakuwa hawapo katika nchi hizo nadhani hata marekani hawachapi passport na pesa zao huchapishwa kwingine pamoja na uwezo mkubwa wa teknolojia walionao.India pekee ndio nasikia wanachapa pesa zao wenyewe nchini mwao.Nadhani inawezekana kwao sababu culture ya wahindi ni wasiri mno wao labda wwanaweza mambo haya.Ila kwa watanzania sijui.Mtu akipewa hiyo kazi kusema akilewa hataropoka kwenye baa sijui.
Labda kama mpiganaji nitoe siri ndogo ya kivita kwa wanaojenga nyumba.Unapojenga nyumba unapoweka dari usimchukue fundi wa kupiga dari wa karibu na eneo unaloishi.Mtafute fundi toka mbali hata kama wapo mafundi wengi tu kwenye eneo unaloishi.Sababu ni kuwa kwenye dari kuna lile tundu unalomalizia kufunga dari ambalo mtu aweza kupanda akitaka kuingia darini.Lile tundu unalomalizia kufunika dari ni eneo la vita hatakiwi mtu ajue liko wapi asijue liko sebureni,chumbani,jikoni,au wapi.Wakija majambazi waweza panda kwa spidi ya mwewe darini ukawasubiria kwenye eneo la tundu ya dari na bastola au bunduki yako au jiwe lako la fatuma.Sasa majambazi yakikaribia hilo eneo unalifungua kwa spidi ya mwewe na kuwamiminia risasi na kurukia mbali eneo lingine ambako hata warushe risasi hawakupati au ukishawamiminia risasi kwa spidi unafumua bati au kigae na kuruka nje na kukimbia kwa spidi ya kenge aliyejeruhiwa kusalimisha maisha yako au kuitia msaada au kuhamishia vita nje kweupe kwenye uwanja mnapoweza kuonana vizuri.
Sasa kama kazi ya kumalizia dari ukimpa fundi wa maeneo jirani aweza mwaga siri kwa majambazi wakajua eneo lako la kujidai kivita liko wapi.Ina maana unampa fundi wa mbali si kwa sababu mafundi hawapo bali una vitu hutaki vijulikane hovyo kwa usalama wako.
Sipingi wazawa kuchapisha lakini kuna vitu vingine kinachoangaliwa si uwezo tu wa kufanya kazi lakini pia usiri,usalama n.k Kama waweza na wana historia ya usiri na usalama wapewe si kuchapa vitambulisho tu bali hata pasipoti na kazi za kuchapa pesa wawape tu.
Nyani Ngabu,
Mkuu unajua hakuna kitu kigumu duniani kama utatumia elimu yako ya darasa kwa wale ambao hawana elimu..Na ukijaribu kuwa kama wao ndipo unapozidi kuharibu...
Acha elimu tu exposure pia unaweza kuchekesha vilevile, nakumbuka mwaka 1995 nilitaka kupeleka nyumbani matairi ya gari tubeless jamaa wakanambia hayawezi kuuzika Tanzania..Nikajaribu kuwaelekeza hawakunielewa zaidi ya kuona kuwa Mkandara kachanganyikiwa! Ikabidi nianze kutafuta matairi ya tube... mkuu kila mtu niliyemuuliza huku aliniona hamnazo na dunia gani naishi..
Wanabodi,
Tatizo la Masha naweza kuliweka sehemu mbili, kwanza aidha yupo ktk Mtandao na alikuwa anafanya deal Ama alikuwa akijaribu kubadilisha mentality ya watu ktk udanganyifu na ma deal ambayo hayana maslahi ya Taifa. Kwa kufanya hivyo amejikuta akifanya makosa ambayo sii makosa ila kwa yule mwenye kukisia kuna mchezo!
Nina hakika hata mimi katika position yake ningejaribu kuhakikisha nakwenda sambamba na taasisi ya tender kwa sababu record ya taasisi hii ni mbaya sana na ndiyo iliyotuingiza ktk hasara nyingi kubwa za kitaifa hasa nikipata malalamiko ya shirika hata moja tu..Hivyo Masha kachemsha kweli lakini hadi leo nashindwa kuelewa kama alichemsha kwa nia nzuri au mbaya!
Ajabu basi pamoja na makosa yote ya Masha, sisi wananchi na hasa hapa JF tumemkalia Masha kooni tumesahahu kabisa kwamba Taasisi hii ya tender ndiye yenye scandals kubwa sana na ulaji wote huanzia pale..
Ni rahisi sana kumkamata Masha au kiongozi yeyote nje ya board ya tender kuliko kufahamu kinachoendelea humo na hakika kama mnakumbuka tuliwahi kusema kama kweli viongozi wetu wanataka UWAZI basi tender yoyote ya kitaifa ni lazima ipitishwe na Bunge... Hili limeshindikana na limepigwa vita sana na viongozi tena wamelijengea hema kuwa ni siri ya serikali.. WHY?..
tk,
Ripoti gani hiyo ya madini? Siye huyu huyu Masha aliyekuwa wakili wa kampuni ambazo hivi sasa zinapora madini ya Watz?
Hongera tk. Wewe ni mfano wa mawakili bora, wenye uwezo na upeo mkubwa na unaitumia vema elimu yako kumtetea Waziri Masha kwani hii si mara yake ya kwanza kupindua jahazi ukianzia ripoti ya kuvinjari Keko usiku.[/QUOTE/)
Mimi si wakili wa Masha bali mtu anayepima mambo kutokana na facts. Katika Points 5 nilizozitoa utausaidia umma zaidi kama utonyesha wapi huyu waziri alipokosea kipengele kwa kipengele. Tuachane na Majungu ya mambo binafsi hapa tunazungumzia masuala mazito ya kitaifa sio mambo ya keko usiku...what the hell is that!!!. I though JF was the home of great thinkers!!
Hongera tk. Wewe ni mfano wa mawakili bora, wenye uwezo na upeo mkubwa na unaitumia vema elimu yako kumtetea Waziri Masha kwani hii si mara yake ya kwanza kupindua jahazi ukianzia ripoti ya kuvinjari Keko usiku.
Haya mkuu, tunazisubiri hizo habari,
asiishie kukanusha bila uthibitisho. Nakumbuka nipashe walitaja hoteli na chumba alichokutana nao, sasa atueleze kinagaubaga ukweli wa mambo maana isije ikawa ile bifu ya waziri kijana ndo inamtafuna!!!!Na kama ikithibitika kwamba hakukutana na SAGEM na kama hana mawasiliano yoyote ya siri ili kuunufaisha upande mmoja basi achukue tahadhari siku nyingine asijaribu kumtunishia misuli mfanyabiashara mwanasiasa!!!
Hongera tk. Wewe ni mfano wa mawakili bora, wenye uwezo na upeo mkubwa na unaitumia vema elimu yako kumtetea Waziri Masha kwani hii si mara yake ya kwanza kupindua jahazi ukianzia ripoti ya kuvinjari Keko usiku.[/QUOTE/)
Mimi si wakili wa Masha bali mtu anayepima mambo kutokana na facts. Katika Points 5 nilizozitoa utausaidia umma zaidi kama utonyesha wapi huyu waziri alipokosea kipengele kwa kipengele. Tuachane na Majungu ya mambo binafsi hapa tunazungumzia masuala mazito ya kitaifa sio mambo ya keko usiku...what the hell is that!!!. I though JF was the home of great thinkers!!
TK with due respect, mbona umerukia bunduki mwenyewe na kuanza kuhukumu? you sound to be prejudice too. Slow down, utajibiwa hizo 'hoja zako 5' na wadau.
Hyperthetically speaking!..maswali tunayojiuliza leo kuhusiana na Masha yanatokana na wasiwasi yetu kwake kutokana na barua ile? au ni huu mradi mzima!
Je, iweje hatukuweza kujiuliza maswali kama hayo wakati Dr. Slaa alipowasilisha EPA au Zitto na Buzwagi!..still nadhani tungeweza kujenga maswali kama haya..
Wakuu, naomba kufahamishwa zaidi maanake sipendi kumhukumu mtu wakati hatuna ushahidi wa kutosha hata kwa kuunganisha unganisha mbali na kwamba kachemsha!..
Nitarudia swali langu..
Kama wewe upo ktk nafasi yake kama waziri wa mambo ya ndani na umenusa harufu ya Rushwa toka taasisi ambayo imewahi kufanya mabaya kama haya utachukua hatua gani?..[/QUOTE]
Nita-REPORT taasisi ya kupambana na rushwa... (Si tunahimizwa hivyo na hao kina Masha??? au?

Kama wewe upo ktk nafasi yake kama waziri wa mambo ya ndani na umenusa harufu ya Rushwa toka taasisi ambayo imewahi kufanya mabaya kama haya utachukua hatua gani?..

Wakuu Mkandara na Macho_Mdiliko, heshima kwenu. Mimi naamini kuwa Masha ameingia kwenye matatizo baada ya ku-challenge ulaji wa watu. Nasema hivyo kwasababu tender hiyo inaelekea kuwa ina interest za watu wengi sana na wenye uwezo na ushawishi mkubwa. Ni kweli kuwa Masha kuamua kuandika barua kwa PM na kumuelezea hofu yake kuhusiana na jinsi mambo yanavyokwenda, alikuwa akidhani kuwa alikuwa anafanya jambo jema kwa Taifa. Nadhani kama Waziri, alihisi pia kuwa kuandika kwake barua ile kusingeweza kumsababishia matatizo makubwa ya kimtazamo. Hayo yote ni mawazo yangu na yanatokana zaidi na kumsikia kwangu akielezea suala zima. Japokuwa maelezo yake hayakuwa straight na yenye kujitosheleza sana.
Mkandara umeuliza swali la maana sana. Swali la "Kama wewe upo ktk nafasi yake kama waziri wa mambo ya ndani na umenusa harufu ya Rushwa toka taasisi ambayo imewahi kufanya mabaya kama haya utachukua hatua gani?".
Jibu rahisi na lenye maana ni kuandika barua kuelezea hisia zangu za rushwa na jinsi inayoonekana kutokea katika utekelezaji mzima (kama alivyofanya, ila kwa maelezo zaidi). Hasa nikiamini kuwa serikali yangu inafanya kazi kwa kumbukumbu na taratibu kama hizo. Na pia kwa kuamini kuwa siri za serikali hutunzwa vizuri na sio rahisi maandishi hayo kuchukuliwa kinyume na makusudio yake.
Mkuu kujibu swali lako kwa namna tofauti ni kufuatilia bila kuacha traces. Yaani kuongea na PM bila kuandika ama kupigia kelele matatizo yanayojitokeza bila kuacha kumbukumbu za kimaandishi. Hii ingeweza kueleweka vizuri zaidi kwa maana labda angeweza kueleza kwa undani zaidi kuliko ilivyo kwenye barua yake.
Ila kwa upande mwingine, ni vyema angefahamu nafasi yake kama Waziri katika mchakato wa siri kama huo na kuepuka kulalamikia/kuzungumzia ama kutolea kauli mchakato kwa utetezi wa bidder mmoja tu (nadhani hapo ndipo kosa lake lilipo). Angelalamika bila kutaja bidder yeyote, angeweza kuwa na hoja. Ila kwa kulalamika kuwa bidder fulani anaonewa peke yake, wakati kuna wengine ambao pia walienguliwa, inazua maneno mengi na kumsababishia kashfa kama hizo zilizojitokeza.
Halafu cha kuchekesha eti tunaambiwa huyu Masha ni msomi....
Kama Masha kabobea sijui Johnnie Cochran alikuwaje....
=Recta;377208]Hapo mkuu sikubaliani na wewe au labda sikuelewi. Hivi Waziri ambaye kweli anajua kazi yake vizuri anaweza kuanza kulalamika kwa barua kwa jambo ambalo ana hakika nalo?? Kama huo ndo mwendo wa mawaziri wa JK kumwandikia PM au Rais barua za malalamiko tena ndefu namna hiyo basi au wakubwa watakuwa wanafanya kazi moja tu ya kusoma barua!!Mkandara umeuliza swali la maana sana. Swali la "Kama wewe upo ktk nafasi yake kama waziri wa mambo ya ndani na umenusa harufu ya Rushwa toka taasisi ambayo imewahi kufanya mabaya kama haya utachukua hatua gani?".
Jibu rahisi na lenye maana ni kuandika barua kuelezea hisia zangu za rushwa na jinsi inayoonekana kutokea katika utekelezaji mzima (kama alivyofanya, ila kwa maelezo zaidi). Hasa nikiamini kuwa serikali yangu inafanya kazi kwa kumbukumbu na taratibu kama hizo. Na pia kwa kuamini kuwa siri za serikali hutunzwa vizuri na sio rahisi maandishi hayo kuchukuliwa kinyume na makusudio yake.
Ila kwa upande mwingine, ni vyema angefahamu nafasi yake kama Waziri katika mchakato wa siri kama huo na kuepuka kulalamikia/kuzungumzia ama kutolea kauli mchakato kwa utetezi wa bidder mmoja tu (nadhani hapo ndipo kosa lake lilipo). Angelalamika bila kutaja bidder yeyote, angeweza kuwa na hoja. Ila kwa kulalamika kuwa bidder fulani anaonewa peke yake, wakati kuna wengine ambao pia walienguliwa, inazua maneno mengi na kumsababishia kashfa kama hizo zilizojitokeza.
Hapo uko sahihi.Hilo suala la kula sahani moja na Tender Board kwa ajili ya kampuni moja tu kati ya 54 lazima limpe mashaka kila mtu atakayesikia habari hizo. Kwamba LM ana undugu gani na Segem hadi awaonee huruma sana kwa kuenguliwa?? Hilo swali naona hakuna hata aliyediriki kumuuliza. Labda angetueleza kuwa hiyo kampuni sasa ina ubia na IMMA???🙄
Hata hivyo sina imani na viongozi wengi wa Tz na kwa hiyo hata hiyo orodha iliyotolewa inawezekana kila kampuni ilibebwa kwa mbeleko yake. Labda tunachoona ni kuwa mbeleko ya Masha ilizidiwa uzito na kuchanika. Hii ni Bongo na kila kitu si kama kinavyoonekana, USANII UNATISHA!!😕