- By the way, naomba kusema neno moja dogo sana, ni kwamba ninawaomba wananchi hapa JF tufike mahali tuelewe sababu ya kuwepo kwetu hapa JF, mimi ninaamini kwamba ni taifa na sio anything else, na ninaamini kwamba wananchi wote tulioko hapa JF tuna uchungu ulio sawa kwa taifa letu na besides hapa ni mahali pa mapambano ya fikra pia, lakini lengo ni kulisaidia na ili tulikomboe taifa letu kutoka mikononi mwa viongozi wachache waliotusaliti wananchi wa taifa hili Tanzania.
- Ninasikitishwa sana na baadhi yetu wananchi kushindwa kuelewa kwamba kila kitu kwenye maisha kina wakati wake na msimu wake, katika mapambano ya fikra za kisiasa kama ilivyo hapa JF, sio ajabu kuwepo na patashika za hapa na pale, lakini tatizo linakuja pale wengine wetu wanaposhindwa ku-let it go, kuna msimu wa kucheka na msimu wa kulia, lakini haiwezekani ikawa mkisha pitia msimu wa kulia tu basi iwe kila siku kurudia rudia yale yale ya msimu wa kulia, tunapoteza focus wakuu yaani taifa.
- Mambo mengi yanafanyika na kutupita wakati tunapoteza muda, hivi unajua sasa hivi ni marufuku kwa wafanyakazi wa serikali kufungua JF? Hivi unajua kua ni marufuku kwa wafanyakazi wa serikali kukutwa na kijarida cha Fikra za cheche? Hivi unajua mafisadi sasa wanakaribia kulishika taifa tena maana hapa kati kati walianza kuishiwa nguvu? Lakini finally nguvu zimeanza kuwarudia tena, huku sisi tukipoteza muda hapa kusifiana na kuchekana wakuu tuamke!
- Hivi ni nani anakuwa na sifa kubwa hapa JF, kwamba ni mchambuzi makini, kwamba ni bingwa this or that? Nani huyo ambaye wananchi wetu wa mijini na vijijini wamemsikia na kumjua kua ni mkombozi wao mkubwa? JF tulikuwa na sifa kubwa sana huko nyuma kwa sababu we were working together kwa manufaa ya taifa, kwenye kila hotuba ya rais in the first two years in power tulikuwa hatukosi kuwemo, akituita "watu wa internent" tulikuwa hatukosi kwenye hotuba za rais, mara ya mwisho tulitajwa kwenye hotuba yake bungeni mwaka jana, that was it hajarudia tena kututaja, WHY? ni kwa sababu tumeanza kukosa muelekeo, tumeanza kuwa mimi, mimi, mimi, na me myself and I, tumeanza kukalia ya jana tu yaani mambo ya Jumapili mpaka leo bado tuu, vipi wakuu tunarudi nyuma sasa amukeni twende mbele.
- Ndugu zangu lets get serious tena, hakuna wa kusifiwa hapa wakati taifa linadidimia huku bongo, acheni wananchi wa nje ya forums wasifie iwapo wanaguswa na kinachoendelea hapa, lakini haya ya kuvunjiana heshima na maneno mengi yasiyosaidia taifa sidhani kama yanaweza kutusadia kwenye long run, sawa hatuwezi kuzuia malumbano, lakini yakiisha yaishe tusonge mbele sio kukalia yale yale tu ya jana inakatisha taamaa wananchi walio serious wakuu, zamani tulikuwa tunasifiwa na magazeti na hata viongozi wetu, lakini sasa tumegeuka kutafuta sifa tu wenyewe tena sometimes kwa nguvu nguvu na ujanja ujanja as if wananchi wa vijijini wanafadika anything na hizi sifa, please lets work together wakuu, too much division hapa sasa,
- I mean hatuwezi wote kua na msimamo sawa, lakini ni lazima tuheshimiane kwamba lengo letu ni moja nalo ni kulikomboa taifa, tunakua na nguvu sana tukiwa pamoja, lakini sio tukigawanyika kama tulivyo sasa, we are losing this war na mafisadi wakuu, tulumbane lakini yakiisha yaishe yakija yaje, lakini yakipita yapite na tusonge mbele ndugu zangu, taarifa nilizoazipata leo kutoka Dodoma zinasikitisha sana wakuu, hebu tupunguze yasiyokuwa na faida kwa taifa na hasa wananchi wanaotuangalia sana hapa JF kama darasa la kuwakomboa kimawazo, maana ni wengi sana kuliko wengi wetu tunavyofikiri.
Haya ndugu zangu sana Fundi Mchundo, Kuhani, Uwiano Maalum, Nyani, Yoursnameismine, na wengineo wote tukaze buti sasa taifa linadidimia hili, ya jana ya jana, ya kesho ya kesho, lakini one day at a time.
Ahsante Wakuu wote, na Mungu Aibariki JF.
Baharia - FMES!