Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Hii ni barua ya kujitetea kwa waziri mkuu au ndiyo ya kuomba kampuni ya Sagem ipendelewe?

Ndio hivyo maana nimesoma marambilimbili sijaona madudu zaidi ya best dili na kule karibu ya mwisho kuna kitu mlango wa nyuma , nilifikiria labda pengine habari itakuwa na uzito wa kusema mambo ya wiziwizi.
Ikiwa tu kuna mtu ameifahamu lugha ya hapo labda ni ya kikubwa au ya kifisadi wengine itatuwia vigumu kugundua kuwa kuna rushwa ,na zaidi kwani hapa kuna rushwa au ni mtu kuingilia jambo si lake na kuharibu dili za watu wengine,fafanuweni.
 
Kuna taarifa toka Dodoma kuwa kuna barua toka PPRA inayomsafisha Masha. Kama hivyo ni kweli, basi, imani yangu kwa chombo hicho haipo tena. Sioni ni vipi PPRA wataweza kujibu maswali yale kumi yaliyoandikwa ktk gazeti la Nipashe yaliyopewa kichwa cha habari, "MASWALI KUMI KWA WAZIRI MSHA". Ni ngumu sana kuziamini taarifa hizo.

Taratibu za kwenda PPRA hufanywa na Katibu Mkuu, nae hufanya hizo kama hakubaliani na maamuzi ya Tenda Bodi yake. Kabla ya kwenda PPRA kwanza hukaa na Bodi yake na kuishawishi ikubaliane nae, na kama Tenda Bodi haikubaliani nae, basi hulazimika kwenda PPRA kupata mwongozo.

Katibu Mkuu ni ofisi, na ktk suala hili, ni kuwa, Katibu Mkuu aliyepita aliishafanya maamuzi ya kuendelea na hatua ya pili. Narudia tena, sitaki kuamini kuwa ni kweli, Patrick Rutabanzibwa alienda kuomba ushauri PPRA. Ugumu ni kuwa, ofisi yake iliishafanya maamuzi, sasa yeye anaenda huko kufanya nini? Kumsafisha rafiki yake, Waziri Masha? Nasema sitaki kuamini kwa sababu Patrick ni mtu mzima na mwenye uzoefu mkubwa sana Serikalini, sidhani kama yeye ni mgeni na sheria za manunuzi, hivyo hili analitambua kinagaubaga. Lakini ugumu mwingine ninaoupata hapa ni kuwa, mbona Patrick hakukaa na Tenda Bodi yake na kuwaambia kuwa yeye hakubaliani na maamuzi yao, na maamuzi ya Katibu Mkuu aliyepita?

Naingia kupata ugumu zaidi baada ya kutambua kuwa, PPRA kabla hawajatoa tamko lolote, huwataarifu wajumbe wa Tenda Bodi kuwa kuna malalamiko toka kwa Katibu Mkuu wao na wao watoe taarifa ya kutetea maamuzi yao, lakini ktk sakata hili mbona mambo hayo hayakufanywa, na tunasikia tu kuwa kuna barua toka PPRA inayomsafisha Waziri Masha?

Kama kuna ukweli ktk suala hili la barua a PPRA, basi kuna haja ya kufanya uchunguzi zaidi ktk chombo hiki, na LAZIMA wawajibike kwa mujibu wa sheria.
 
bbc wamemhoji RPC jioni hii, RPC anasema huenda ikawa ni vi-toy. polisi wetu LOL
 
Itakubidi ui-download, halafu inakubidi uwe na software ya kufungulia ZIP FILES.

Kama vipi Invisible aiweke kwenye PDF. Au..?
Mtindio,

Nadhani SI LAZIMA mtu atumie Winzip kufungua Zipped file. Ni ku-right click kisha ku-explore file na kuona kilichomo ndani.

Ingekuwa .rar file hapo ingemlazimu mtu hapa a-search JF (hiyo software ipo) kisha ainyakue na kuweka kwenye kompyuta yake.
 
Ndugu zangu ktk JF, nadhani hapa kuna tatizo la ushabiki na la pili ni kutokujua mfumo wa uongozi ktk wizara. Waziri anawajibika na masuala yote ya kisera na kisiasa ktk wizara, bosi wake ni Rais. Katibu Mkuu anawajibika na masuala yote ya kiufundi na kiutendaji, bosi wake ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Watumishi wote wa serikali wapo chini ya Chief Secretary. Sheria za manunuzi ziliwaondoa wana-siasa kujihusisha na mchakato wa manunuzi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wao sio watendaji ktk serikali, ndio maana vigezo vya kumpata Diwani au Mbunge havizingatii elimu au uzoefu alionao.

Tatizo la waziri Masha ktk sakata hili ni kuwa, yeye alizuia mchakato wa kumpata mzabuni, kwa sababu tu, eti kampuni ya Sagem iliondolewa ktk hatua za mwanzo. Ikumbukwe ya kuwa, ktk tenda hii kulikuwa na makampuni 104 yaliyochukua tenda document, na 54 pekee ndio yaliyorudisha.

Utaratibu wa Open enda ni kuwa, kila kampuni iliyoomba itafahamishwa kwa maandishi sababu za kuondolewa kwao, na wale wote walioshinda watafahamishwa kujiandaa na hatua ya pili.

Kila kampuni inaruhusiwa kupinga sababu za kuondolewa kwao. Hatua ya kufanya hivi ni kuwa, kwanza wanamuandikia barua ya kupinga katibu mkuu wa wizara, na kama hawataridhika na majibu, basi watapeleka malalamiko yao kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), kama hawataridhika na uamuzi wa PPRA basi watakata rufaa PPAA (Public Procurement Appeal Authority). Kila hatua imepewa muda wake kushughulikiwa, hivyo hakuna suala la ucheleweshaji hapo.

Kama kweli Masha alitaka kuisaidia Serikali anayoitumikia, angewashauri Sagem wafuate taratibu hizo za kisheria. Haki ya mtu huwa haipotei, bali huwa inacheleweshwa tu.

Baada ya kutokukubaliana na maamuzi ya Katibu Mkuu wake na tenda bodi yake inayowashirikisha watu mahili toka idara ya usalama wa Taifa na TAKUKURU, Katibu Mkuu aliiamuru tenda bodi iapitie malalamiko ya Masha tena. Baada yakuyapitia na kuichambua vizuri kampuni ya Sagem, bodi ikagundua makosa mengine zaidi, ikayaweka bayana ktk taarifa yao kwa Katibu Mkuu minajili ya kumfikishia Waziri Masha. Kwanini hili halisemwi?

Kwanini Masha alipoambiwa na Sagem kuwa wameenguliwa alikurupuka na kusimamisha mchakato ilhali akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria?

Kamati ya Bunge inayoshughulikia suala hili mpaka sasa haijamuhoji mtendaji yeyote ktk mradi huu. Ili kuwa sahihi kwa maamuzi stahili, ilitakiwa Kamati imuhoji vizuri Katibu Mkuu aliyepita kwani yeye aliondoka akiwa ameishafana maamuzi yote, Katibu na M/Kiti wa tenda bodi, na Consultants wa mradi.

Suala hili tusifikirie ni dogo kama linavyosomeka. Hapa kuna sheria zimekiukwa, LAZIMA HATUA zichukuliwe.

.........sawa kabisa Kinvaba.......


Kuhani.....
.........sijui una maana gani unaposema........ "irreparable injury".........hakuna kitu kama hicho ktk zoezi zima la procurement ili mradi tu mtu uwe umefuata timings za appeal.......no tender will be awarded.......
 
Mtumishi wa umma Jakaya Kikwete yuko chini ya Chief Secretary?

Kuhani, kwa muibu wa sheria ya utumishi wa umma (Public Service Act) , Rais, Waziri mkuu na Mawaziri, Wabunge na wale wote ambao huchaguliwa kwa kupigiwa kura, sheria haiwatambui kuwa watumishi wa serikali. Bali ni viongozi wa kisiasa. Japokuwa tunaweza kusema kuwa nao ni watumishi wa umma. Ndio maana kuna sheria pia mahususi inayomhusu rais (Presidential Act). Otherwise, Chief Secretary ndiye mkuu wa atumishi wote wa umma kwa mujibu wa sheria ya watumishi wa umma.
 
[QUOTE]Mtumishi wa umma Jakaya Kikwete yuko chini ya Chief Secretary?

Kuhani, kwa muibu wa sheria ya utumishi wa umma (Public Service Act) , Rais, Waziri mkuu na Mawaziri, Wabunge na wale wote ambao huchaguliwa kwa kupigiwa kura, sheria haiwatambui kuwa watumishi wa serikali. Bali ni viongozi wa kisiasa. Japokuwa tunaweza kusema kuwa nao ni watumishi wa umma. Ndio maana kuna sheria pia mahususi inayomhusu rais (Presidential Act). Otherwise, Chief Secretary ndiye mkuu wa atumishi wote wa umma kwa mujibu wa sheria ya watumishi wa umma.[/quote]

yaani hapo sijui kigumu kukielewa ni kipi? geeeeeeeeez
 
KUHANI,

Rais wa nchi huwa anakula kiapo cha Urais na kuweka timu yake ya watumishi. Unapojibu swali jaribu kuwa makini kwa kulisoma na kulielewa kwanza, ndio maana tuna Rais mmoja tu ktk nchi.

Wewe ndio husemi ukweli hapa. Masha kama Waziri alimuagiza Katibu Mkuu kusimamisha mchakato wa zabuni mpaka atakapopata majibu toka kwa Pinda. Kama unasema kweli ktk hili, mbona unasema kama asingezuia kungetokea "irreparable injury".?

Acheni janja yenu ya kupindisha ukweli kwa kuweka maneno mazuri ktk mistari. Ninyi ndio munaokena sio washauri wazuri wa Masha, munamuangamiza rafiki yenu, nchi hii sasa hivi watu wameamka.
 
Are u mad or toxicated?
nauliza swali la maana unaleta utani.......

...i'm mad yoyo!
...nilikuwa nayoyoma tu baada ya kuwa intoxicated by your question. calm down son!
 
Last edited:
...sina uhakika. yawezekana kuna sehemu alishadislose jinsia yake, labda ndiyo maana Kuhani alisema 'he'.

...mimi nimesema 'angelikuwa she' bila kuconclude kama sivyo au ndivyo. Btw, je kuna nafsi mbili tu?!

What if that person is a hermaphrodite?
 
...i'm mad yoyo!
...nilikuwa nayoyoma tu baada ya kuwa intoxicated with your question. calm down son!
Umeshanipa jinsia ya kiume......
.......anyway ma pundits mmesema Masha ajiuzulu kwa lipi?
 
Umeshanipa jinsia ya kiume......
.......anyway ma pundits mmesema Masha ajiuzulu kwa lipi?

...kwa sababu ulishamtaka Irene Uyowa na kusema kuwa unatengeneza maburungutu kisha utamzukia Kelly01 ili aanze kukuita uncle! Vipi tena mkuu, au unataka kurudi kwenye maswala ya avatar yako iliyokuwa inaonesha sindiria tena ili tuweze kuhakiki?!
 
Back
Top Bottom