Fundi, huyu Masha hana rekodi nzuri ya uongozi. Inawezekana kabisa alitaka kufanya ufisadi hapa.
Lakini nakuomba unifanyie hisani moja mzalendo. As hard as it may be, hebu assume kwamba Masha sio fisadi, assume hana rekodi ya erratic pronouncements wala uchafu wowote ule. Let's hypothesize briefly kwamba hapa pia nia yake ilikuwa ni nyeupe kama mwana kondoo, yani kuhakikisha mzabuni atakaeshinda tenda ni wa haki na kweli. Halafu tuangalie, je, alotenda ni sawa? Okay? Thank you.
Sasa bosi wa Katibu wa Wizara ni nani? Well, kwani huo utendaji huo, maagizo anayapata kwa nani? Anatekeleza na kutenda mipango na mwongozo wa nani? Nadhani sio jibu bovu nikisema ni waziri! Luhanjo haamki asubuhi kutuma daily projects kwa makatibu wakuu wa wizara. Na ukikubali kwamba Masha ndio msimamizi na mwongozaji mkuu wa kazi zote za wizara, huoni kwamba Masha yuko sahihi kuulizia na kufuatilia kazi zinazofanywa na wafanyakazi wake, akiwemo mtendaji mkuu, Katibu ? Halafu Masha akiulizia kitu akaona kuna tenda zinaenda kimizengwe (nilikuomba u-assume kwamba Masha alikuwa ana moyo mweupe) halafu akajaribu kuziwahi kabla tenda hajapewa Richmond mwingine wa vitambulisho hapo kosa litakuwa lake au ni mfumo mbovu wa itifaki?
Wewe unaona hakuna tatizo, unasema Makatibu Wakuu walikuwa wamefunikwa na mawaziri. Well, under your model, or the prevailing model, mimi naona ni mgongano wa majukumu kwa sababu organizational entity yeyote lazima iwe na itikafi, mfumo wa ngazi ya utawala, liwe kanisa, liwe duka la wachaga, iwe nchi, uwe msikiti, iwe familia ya kimafia.
Timu yetu ya uchochoroni ilikuwa na kapten, mweka hazina, na katibu. Wote tulikiwa chini ya mwenyekiti.