Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Yaaah, hamna kitu mkuu lakini naona watu wanaendelea na discussion, sijui wamepata wapi wanachojadili!

You almost got me mkuu! Wanasema "never say never". Nimeng'ang'ana mpaka ikafunguka. Ngoja niifanyie homework sasa!
 
Mkuu Inv,

Mbona zipped folder iko empty? Au ni kwangu tu?

Yaaah, hamna kitu mkuu lakini naona watu wanaendelea na discussion, sijui wamepata wapi wanachojadili!

Ndio maana huyo mtu akasema "au ni kwangu tu"?

Msaidie member wako, sio kum blast, obviously he is doing something wrong, tusimjibu kinyume nyume!

Zamani ulikuwa unabandika PDF hapa directly, inafunguka bila hata haja ya ku download, siku hizi unaifunga kwenye zipper, why? Mpaka ku down load, halafu ku unzip, ya nini?
 
Yaaah, hamna kitu mkuu lakini naona watu wanaendelea na discussion, sijui wamepata wapi wanachojadili!

hihiiii..danganya toto siyo?!...tumeshaiona mkuu.

Kweli wewe ni invisible maana hata kwenye avatar yako naona macho yanafumba na kufumbua tu.

Thanx man!
 
Ndio maana huyo mtu akasema "au ni kwangu tu"?

Msaidie member wako, sio kum blast, obviously he is doing something wrong, tusimjibu kinyume nyume!

Zamani ulikuwa unabandika PDF hapa directly, inafunguka bila hata haja ya ku download, siku hizi unaifunga kwenye zipper, why? Mpaka ku down load, halafu ku unzip, ya nini?

...angelikuwa 'she' labda angeliweza kwa urahisi, who knows!
 
Wakuu hapa kazi ipo, mimi nimeona matatizo yafuatayo:-

1) uandishi wa barua siyo makini kabisa. Mhe. ni msomi (Masters holder) tena mwanasheria aliyebobea, inakuwaje aandike barua shallow hivyo! 60% ya barua ni malalamiko kutoka sagem, nilitegemea kuona kiambatanisho A, kiwe malalamiko ya sagem.

Kuandika ameandika vizuri tu kiswainglishi swaafi ILA TU HAMNA SUBSTANCE. Yaani hiki ndicho Mh. JK alichowatuma mawaziri wetu?

Kaazi kweli kweli..
 
....same thing iliyoleta disaster and loss of billions kwa ubabe and favoritism za Lowassa kulazimisha na kuingilia kazi za bodi zilizokuwa zinaamua umeme ndio kinachofanyika hapa na huyu Masha,huyu hana tofauti na alichofanya Lowassa kwenye Richmond na anataka kutuletea incompetent company kwa ajiri ya 10% or for whatever reason ambayo cost yake still tunalipia in billions every month kwa makampuni kama IPTL,Richmond etc,this is abuse of power and corruption...he must go,fisadi mkubwa huyu!
 
Ndio maana huyo mtu akasema "au ni kwangu tu"?

Msaidie member wako, sio kum blast, obviously he is doing something wrong, tusimjibu kinyume nyume!

Zamani ulikuwa unabandika PDF hapa directly, inafunguka bila hata haja ya ku download, siku hizi unaifunga kwenye zipper, why? Mpaka ku down load, halafu ku unzip, ya nini?
.....Kuhani, nadhani payload ya open page kwenye jamiiforums inakuwa more bearable kwa kuondoa open image files ziambatanazo na quoted messages. Offcourse, hii ina translate moja kwa moja to monetary value kwa ku-conserve bandwith usage na kurahisishia wale walioko kwenye low bandwidth connection katika kufungua page. Btw mkuu kunawezekana kukawa pia na conditions alizopewa katika kupata hiyo document.
 
Ndugu zangu ktk JF, nadhani hapa kuna tatizo la ushabiki na la pili ni kutokujua mfumo wa uongozi ktk wizara. Waziri anawajibika na masuala yote ya kisera na kisiasa ktk wizara, bosi wake ni Rais. Katibu Mkuu anawajibika na masuala yote ya kiufundi na kiutendaji, bosi wake ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Watumishi wote wa serikali wapo chini ya Chief Secretary. Sheria za manunuzi ziliwaondoa wana-siasa kujihusisha na mchakato wa manunuzi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wao sio watendaji ktk serikali, ndio maana vigezo vya kumpata Diwani au Mbunge havizingatii elimu au uzoefu alionao.

Tatizo la waziri Masha ktk sakata hili ni kuwa, yeye alizuia mchakato wa kumpata mzabuni, kwa sababu tu, eti kampuni ya Sagem iliondolewa ktk hatua za mwanzo. Ikumbukwe ya kuwa, ktk tenda hii kulikuwa na makampuni 104 yaliyochukua tenda document, na 54 pekee ndio yaliyorudisha.

Utaratibu wa Open enda ni kuwa, kila kampuni iliyoomba itafahamishwa kwa maandishi sababu za kuondolewa kwao, na wale wote walioshinda watafahamishwa kujiandaa na hatua ya pili.

Kila kampuni inaruhusiwa kupinga sababu za kuondolewa kwao. Hatua ya kufanya hivi ni kuwa, kwanza wanamuandikia barua ya kupinga katibu mkuu wa wizara, na kama hawataridhika na majibu, basi watapeleka malalamiko yao kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), kama hawataridhika na uamuzi wa PPRA basi watakata rufaa PPAA (Public Procurement Appeal Authority). Kila hatua imepewa muda wake kushughulikiwa, hivyo hakuna suala la ucheleweshaji hapo.

Kama kweli Masha alitaka kuisaidia Serikali anayoitumikia, angewashauri Sagem wafuate taratibu hizo za kisheria. Haki ya mtu huwa haipotei, bali huwa inacheleweshwa tu.

Baada ya kutokukubaliana na maamuzi ya Katibu Mkuu wake na tenda bodi yake inayowashirikisha watu mahili toka idara ya usalama wa Taifa na TAKUKURU, Katibu Mkuu aliiamuru tenda bodi iapitie malalamiko ya Masha tena. Baada yakuyapitia na kuichambua vizuri kampuni ya Sagem, bodi ikagundua makosa mengine zaidi, ikayaweka bayana ktk taarifa yao kwa Katibu Mkuu minajili ya kumfikishia Waziri Masha. Kwanini hili halisemwi?

Kwanini Masha alipoambiwa na Sagem kuwa wameenguliwa alikurupuka na kusimamisha mchakato ilhali akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria?

Kamati ya Bunge inayoshughulikia suala hili mpaka sasa haijamuhoji mtendaji yeyote ktk mradi huu. Ili kuwa sahihi kwa maamuzi stahili, ilitakiwa Kamati imuhoji vizuri Katibu Mkuu aliyepita kwani yeye aliondoka akiwa ameishafana maamuzi yote, Katibu na M/Kiti wa tenda bodi, na Consultants wa mradi.

Suala hili tusifikirie ni dogo kama linavyosomeka. Hapa kuna sheria zimekiukwa, LAZIMA HATUA zichukuliwe.
 
Ogah nilimiss sio bungeni ila ni kwenye baraza la mawaziri. Inawezekana kweli sijui system inavyofanya kazi, nielimishe wewe unayejua ukipata muda tafadhali.

Nziku kama kweli Waziri alikuwa akipata briefings, inakuwaje hapa analalamika


.......ndg yangu.....uandishi Cabinet paper ni solely responsiblity ya PS sana sana anaweza ku-delegate kwa DPS..........Material inputs kwenye cabinet paper inatoka kwa senior technical/Administration staff........na hii Cabinet paper inapoandaliwa.......kunakuw ana constant liaison kati ya PS na Waziri husika kwani hata Waziri naye anakuwa na input yake ikibidi.........na isitoshe yeye ndiye atakayei-present mbele ya Cabinet.

....cabinet paper ikishakamilika.......PS huiwakilisha kwa CS.....CS ndiye muandaaji wa muhtasari/ajenda ktk Cabinet........CS ndio huandaa extract ya Cabinet resolutions (hii ni SIRI) na kutuma kwa PS........kwa further utekelezaji..........

.......Inashangaza Masha kulalamika kwa Waziri Mkuu..........ndio maana kuna wakati nilimuita Masha ni MTOVU WA NIDHAMU...........

Kwenye Barua inaonyesha Waziri hajui yafuatayo

1.Open tender............(i.e all are invited....kuna kuwa na post pre-qualification........)

2.Limited/Restricted Tender....... (i.e. prequalification inakuwa ilishafanyika so only selected few are invited to Bid)

nasema hajui kwa sababu kuna sehemu anasema..........eti kamati inajaribu kurudisha utaratibu wa restricted Tender rrom open tender.......ni kichekesho........
 
Kazi kweli kweli~~~~~waacheni wafu wazike wafu wao~~~~

na bado
 
....same thing iliyoleta disaster and loss of billions kwa ubabe and favoritism za Lowassa kulazimisha na kuingilia kazi za bodi zilizokuwa zinaamua umeme ndio kinachofanyika hapa na huyu Masha,huyu hana tofauti na alichofanya Lowassa kwenye Richmond na anataka kutuletea incompetent company kwa ajiri ya 10% or for whatever reason ambayo cost yake still tunalipia in billions every month kwa makampuni kama IPTL,Richmond etc,this is abuse of power and corruption...he must go,fisadi mkubwa huyu!

........nilishasema huko nyuma........jambo alilolifanya Masha halina tofauti sana na upuuzi wa Lowassa kwenye RDC.........sijui kijana ansubiri nini wakati Lowassa alishamuonyesha njia...........
 
Kuandika ameandika vizuri tu kiswainglishi swaafi ILA TU HAMNA SUBSTANCE. Yaani hiki ndicho Mh. JK alichowatuma mawaziri wetu?

Kaazi kweli kweli..

sawa Mkuu, lakini msingi wa barua yake ni malalamiko ya sagem kuondolewa , 60% ya maudhui ya barua ni kuondolewa kwa sagem, lengo la barua ni kujilinda dhidi ya malalamiko ya sagem, hivyo kiambatanisho kikuu ilipaswa kuwa ni malalamiko ya sagem. Kama hakuna kiambatanisho, alipaswa kutoa maelezo ya awali (introduction) ya malalamiko ya sagem. The way barua ilivyo, mimi ningekuwa PM nisingemuelewa hivyo ningemtaka alete malalamiko ya sagem.

kosa la kiuandishi nililolizungumzia ni kukosa ukamilifu (incomplete).
 
Kinvaba.. unachosema ndicho kilichosababisha kuanguka kwa Lowassa pale alipoingilia mchakato wa tenda ya kutafuta majeneretta. Yawezkana alikuwa na nia nzuri lakini hakuwa na uwezo wa kisheria kufanya hivyo. The same applies to Masha. Kusema kuwa "nimefanya hivi kulinda maslahi ya nchi na taifa" ni cliches kwani hata mafisadi wa EPA wanaaweza kutuma mstari huo kujitetea.

Masha anahitaji kutolewa madarakani, kukbakia Mbunge, ili ajijenge vizurri kiuongozi. Nina uhakika baada ya muda anaweza kuwa waziri mzuri..
 
Masha hapa kosa lake nini? hebu tuambizane kwa mapana jamani. Katika hiyo barua, Masha kafanya nini kinachoonyesha kuwa yuko guilty? After all bado details zinahitajika hapa, hao Sagem walijuaje kama wameenguliwa kwenye mchakato? Nani anajua hili?

Kuna nini kimefichwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Katibu Mkuu Kiongozi? Kwa nini wanafanya mambo bila kumjulisha Waziri wa Mambo ya ndani? Wamemwona, mtoto sana hivyo hawezi kuwaelekeza wazee wenye uzoefu au wanataka kumwangusha Masha kisiasa?

Hao makatibu wote wawili wamemdharau waziri Masha na wanapaswa kuwajibika/shwa regardless Masha ni Fisadi, mtoto au hawezi kazi!

UW, shalom!

Suala, liko kwenye appeal procedure ambayo SAGEM alitakiwa kuappeal na si kufanya 'lobbying' kwa mtu wao ( facts zaonyesha hivyo). Kosa limelala hapo, Mkuu. Yeye si ni lawyer, akujiuliza kuhusu code of conducts na issue za trust. Katibu mkuu alishaanza kuondoa hiyo trust ndio maana akatumia turufu yake ya discretionary power na kuongea na katibu mkuu mambo ya ndani.

Huyu lawyer Masha kasigina hizo kanuni na sasa zinamtafuta. Anyway, he is presumed innocent until proved guilty BUT for public interest, he may be asked to resign.

Shadow.
 
Una uhakika kuwa yeye ni "He"?

...sina uhakika. yawezekana kuna sehemu alishadislose jinsia yake, labda ndiyo maana Kuhani alisema 'he'.

...mimi nimesema 'angelikuwa she' bila kuconclude kama sivyo au ndivyo. Btw, je kuna nafsi mbili tu?!
 
sawa Mkuu, lakini msingi wa barua yake ni malalamiko ya sagem kuondolewa , 60% ya maudhui ya barua ni kuondolewa kwa sagem, lengo la barua ni kujilinda dhidi ya malalamiko ya sagem, hivyo kiambatanisho kikuu ilipaswa kuwa ni malalamiko ya sagem. Kama hakuna kiambatanisho, alioaswa kutoa maelezo ya awali (introduction) ya malalamiko ya sagem. The way barua ilivyo, mimi ningekuwa PM nisingemuelewa hivyo ningemtaka alete malalamiko ya sagem.

kosa la kiuandishi nililolizungumzia ni kukosa ukamilifu (incomplete).

Sawasawa..

Kwa jinsi alivyo-address hii barua ni wazi kuwa alikuwa na malengo fulani ya 'ndani', ambayo anayafichaficha ili mwenye kuelewa aelewe na mjinga aendelee kutoelewa.

Kwa mtizamo wangu hii barua imekaa kimtego-mtego.
 
Watumishi wote wa serikali wapo chini ya Chief Secretary.

Mtumishi wa umma Jakaya Kikwete yuko chini ya Chief Secretary?
Tatizo la waziri Masha ktk sakata hili ni kuwa, yeye alizuia mchakato wa kumpata mzabuni...

Husemi kweli. Aliandika barua kwa Pinda kudadisi questionable moves za bodi ya zabuni. Hakuwa na nguvu ya kuzuia process ya tender.

Kama kweli Masha alitaka kuisaidia Serikali anayoitumikia, angewashauri Sagem wafuate taratibu hizo za kisheria. Haki ya mtu huwa haipotei, bali huwa inacheleweshwa tu.

Si kweli. Tenda angepewa mtu mwingine kinyume na taratibu ingekuwa imetokea irreparable injury.
 
Back
Top Bottom