Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Kuna tetesi nimeisikia kutoka kwa reliable source kwamba hata hiyo tender doc ya Sagem Securite iliandikwa na Masha. Well it is easy to connect the dots kama kuna ukweli wowote hapo si unajua hawa wanasheia wetu ni wazee wa kukopy na kupaste. Hivyo basi kama mtu anayo hiyo tender doc ya SAGEM alete hapa tujaribu kuilinganisha na tender docs kadhaa zilizoandaliwa na IMMA na especially Masha.
 
Nasema hivi... fanyeni uchunguzi mdogo sana... uliziieni makampuni ya Tanzania ya biashara tu... makubwa ambayo yanatumia technology ya access control, ambayo ndiyo hiyo hiyo ambayo itatumika... all most yote yana vifaa vya SAGEM...

Mimi simo.... endeleni na siasa zenu... mheshimiwa Masha kama unasoma thread hii... nipe PM... nikupatie dada za kusema ukweli... Watanzania wakuhukumu kwa kukataa ujinga wa kufuata kanuni hata kama hazilisaidii taifa....

It is just a bullshit.... Masha you are very right brother... kwenye taifa la... ajabu kama hili ukionekana hivyo ujue ndio uko sawa.

Du, na wewe umeanza yaleyale ya mkimkuta mtu anaua albino ua. Tufuate sheria kaka. Ndio utawala bora. Lalamikia sheria.
 
Wakuu,
Lililovunda halina ubani... wacha watu wake wahangaike kulifukiza leo, kama kweli limevunda kesho litanuka tu, tena bila aibu hata iweje. Si mnamkumbuka Lowassa??... Mwalimu alisema zamani hili limevunda,...Ben akajitia pamba maskioni na kulifukiza. Matokeo yake wote tunayajua, mpaka watoto wadogo ukitaja Lowassa wanamalizia FISADI.... Na huyu Masha naona anaelekea hukohuko...Mpaka leo hajatoa his side of the story zaidi ya blah blah za wapambe. Halafu akishamwagwa bungeni, ndio ataenda TBC kutaka interview kutoa his side of the story kama mentor wake EL.
 
It is just a bullshit.... Masha you are very right brother... kwenye taifa la... ajabu kama hili ukionekana hivyo ujue ndio uko sawa.

- Katika siasa za taifa kama hizi, kiongozi wa chini ya rais anakuwa a political distraction na liability, kwa agenda ya rais na chama tawala anapokuwa kwenye media kila siku ya Mungu kukicha either kwa mabaya au mazuri. Hapa nilipo ninaishi karibu na kiongozi mmoja mzito wa serikali, ambaye kuna wakati na yeye alikuwa kwenye magazeti kila kukicha tena kwa habari nzuri sana kwa taifa letu, lakini watawala wakaanza kuniuliza kama anataka nini huyo? Ikabidi nimfahamishe kuwa a slow down maana watawala wana tatizo na habari zake kwenye media wanafikiri anataka cheo zaidi kwenye serikali, ndio tabia za watawala, wawe wazuri au wabaya ikabidi mkulu awaombe media waache kumuandika andika.

- Masha is all over the map, hii ni kawaida katika siasa kwa kiongozi mmoja kuwa na this kind of unwanted political attetion kuna wakati ilikuwa Idd Simba, Mbilinyi, Ngasongwa, Mapuri, Mkuchika, Lowassa, na sasa Masha. Kwa habari mpya nilizonazo uwezekano wa yeye kutoka sasa ni mdogo sana na almost haupo, lakini still haimuzii yeye kufanya the right thing kwamba maisha sio uwaziri tu na kutangazwa kwenye media kila siku, jana nimesikia habari njema kwamba hatimaye ameamua kuacha kiywaji sasa hiyo aiongeze mbele zaidi na kuachia madaraka pia kwa faida yake na ya taifa pia maana sio siri kua sasa ameshakuwa ni tatizo kwa agenda ya chama tawala na rais tu, bali hata kwa maisha yake binafsi pia licha ya taifa at large.

Thanxs!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu INVISIBLE hivi katika hiki kimbembe cha Lau wewe uko upande gani? nauliza kwa sababu mkuu unanichanganya na 'thanks'zako,wanaomkandia Masha unawapiga 'thanks' wanaompa mbeleko unawapa'thanks',fafanua mkuu!
 
mmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhh yamekuwa hayo,yaani Lau kaacha ulabu?aangalie asije akaishia kwa Kakobe!
 
Mkuu INVISIBLE hivi katika hiki kimbembe cha Lau wewe uko upande gani? nauliza kwa sababu mkuu unanichanganya na 'thanks'zako,wanaomkandia Masha unawapiga 'thanks' wanaompa mbeleko unawapa'thanks',fafanua mkuu!
Mh... Ningekuwa nimeandika ingependeza, angalia alikoandika Kasheshe, FMES, Kuhani na hata Uwiano Maalum (pana thanks yangu) hapo utajua nipo upande gani.

Am always ready for change, and I believe change is inevitable!

You told me nothing over your own stand Bishanga...
 
Mkuu INVISIBLE hivi katika hiki kimbembe cha Lau wewe uko upande gani? nauliza kwa sababu mkuu unanichanganya na 'thanks'zako,wanaomkandia Masha unawapiga 'thanks' wanaompa mbeleko unawapa'thanks',fafanua mkuu!

Duuh ! Kumbe humu kuna watu wanaochangia kwa kuangalia "fulani" amesema nini? Mi nilidhani watu tunaandika humu kwa na maoni na misimamo binafsi, na si kwa kuangalia who is for and who is against. Atakuja siku moja mtu akakupeleka pabaya kwa sababu tu ya kukariri kwamba uko upande wake siku zote! Be flexible mkuu Bishanga!
 
Kazi.... Ngoja niwe mpole kidogo hapa maana kama kusemwa yameishasemwa saaana, na karibu yote yana maana. Jambo la msingi ni kuangalia sheria za manunuzi zinasomekaje, na ktk sakata hili nani amezikiuka.

Wahenga walisema... La kuvunda halina ubani.

Ushauri wa BURE kwa Waziri Masha: CHANGE YOUR BEHAVIOR, YOU HAVE LOST THE QUALITY OF LEADERSHIP. ALTHOUGH LIFE IS WHAT YOU MAKE IT, A PUBLIC FIGURE LIKE YOU MUST BE READY TO BE ACCOUNTABLE.
 
Nasema hivi... fanyeni uchunguzi mdogo sana... uliziieni makampuni ya Tanzania ya biashara tu... makubwa ambayo yanatumia technology ya access control, ambayo ndiyo hiyo hiyo ambayo itatumika... all most yote yana vifaa vya SAGEM...

Mimi simo.... endeleni na siasa zenu... mheshimiwa Masha kama unasoma thread hii... nipe PM... nikupatie dada za kusema ukweli... Watanzania wakuhukumu kwa kukataa ujinga wa kufuata kanuni hata kama hazilisaidii taifa....

It is just a bullshit.... Masha you are very right brother... kwenye taifa la... ajabu kama hili ukionekana hivyo ujue ndio uko sawa.

Kwa sababu makampuni ya bongo yanawatumia ndiyo ku-legitimise wao kukiuka taratibu? Pengine uzoefu huu ndio uliompa kiburi cha kufikiri anaweza kutumia njia za chini chini. Katika open tenda kinachoangaliwa ni kilichokuwa submitted na si kingine!
 
Kuna taarifa zimepikana sasa hivi kuwa Masha na Wapambe wake wameisha wanunua baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti fulani ili wamsafishe, na pia wawachafue washauri wa Mradi na Waziri mmoja, Zitto na Dr. Slaa. Majina ya waandishi hao, magazeti watakayoyatumia yametajwa na report wanayoiandaa imepatikana pia. Naifanyia kazi kabla ya kuitoa hadharani (Katika JF).

Ijumaa ya tarehe 30.01.2009, Waziri Masha alionekana akimpa "documents" mwandishi wa habari ambae ni Mhariri wa moja ya magazeti yaliyonunuliwa kufanya kazi hiyo. Inaaminika kuwa moja ya "documnts" hizo zilitmika ktk matoleo ya magazeti yalifuata, yaani kuanzia Jumatatu ya tarehe 2 February 2009 na Alhamis ya tarehe 5 February 2009.
 
habari toka gazeti moja maarufu hapa nchini zinasema kuwa baada ya kikao kizito cha kamati ya bunge ya mambo ya nje,ulinzi na usalama,imeoneka ni mapema mno kwa waziri masha kujitetea kwani kufanya hivyo ni kuweka uwazi mchakato mzima wa zabuni ta ID AMBAPO ni kinyume na kanuni ya manunuzi(procurement act no:-21).

Hivyo tunarudi kwenye jibu la msingi la mh.waziri mkuu alipokuwa anajibu hoja ya Mh.Dr.Slaa.

Vilevile baadhi ya vielelezo alivyokuwa navyo Mh.Dr.Slaa ni makosa kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu.

Inaonekana Mh.Masha atapeta mpaka mchakato mzima umalizike ila kamati na baadhi ya wabunge wanazipitia sheria kwa umakini na ukaribu mkubwa kuona uwezekano wa hoja ya Dr.Slaa kuwasilishwa bungeni.
 
Baada ya yote haya wanadhani kuna mtu atakayeamini matokeo ya mchakato huo?
 
Kasheshe,

Kampuni ya Sagem ina utaalam mzuri sana ktk eneo la Automated Finger Print System (AFIS), na sio ktk mradi wa Vitambulisho vya Uraia. National IDs ina components nyingi sana, AFIS ni moja wapo. Kwa kujua component moja kati ya kumi hakumaananishi kuwa wao wanajua National Identity Cards Project.

Sio kweli kuwa Sagem alipewa alama nzuri ya rushwa ktk mchakato unaoendelea nyumabni (TZ). Ninavyojua mimi ni kuwa, ktk hatua za mwanzo kampuni zinatakiwa kutoa a "certificate of anti-bribery". Hatua ya pili ni kuchunguza kwa kina yale uliyoyasema ktk "Pre-Qualification Tender Document". Naamini ktk hatua hii ambayo huwahusisha kwa kiwango kikubwa sana UWT wangemkamata Sagem kwa kuongopa.

Naomba kusema tu kuwa, Sagem is not a right company to implement national ID project.
 
Ni vizuri kufuata sheria na kumkamata mtu akitenda kosa. Tatizo ninaloliona hapa ni kuwa Waziri Masha ameingilia mchakato na ameusimamisha. Hatuwezi kusubiri mchakato uishe wakati umesimamishwa, na Masha analazimisha sheria zikiukwe ili kampuni ya Sagem ipachikwe ktk hatua ya pili.

Kwa kuwa yeye hana mamlaka kisheria, basi anataka kuilazimisha ministerial tender board ifanye kazi hiyo, lakini wajumbe wa tenda bodi wameapa kuwa, kwakuwa wao wameapa kwa mujibu wa sheria, hawatakubali kutumiwa kama muhuri ktk suala hili, eti tu kwa maslahi ya Waziri, wameahidi kujiuzuru ikibidi.

Ninachomshangaa Masha ni kuwa, haya yote yanatokea ktk wizara yake yeye amekazania Sagem, hivi Tenda Bodi ikijiuzuru, atakuwa na neno gani kwa wananchi wa Tanzania? This is typical "cost of corruption". Huenda alichopewa na Sagem ni kikubwa zaidi kuliko hata akifukuzwa kazi, hivyo yupo tayari kufukuzwa lakini Sagem wapate mradi. Sidhani kama atafanikiwa ktk hili.

Kuna mawaziri wengi wanamdharau sana JK na hivyo wanapoteza radha ya kumsoma kiongozi wao. Masha ni mmoja wao. Angemsoma vizuri JK asingethubutu kufanya upumbavu wake anaoufanya.
 
Masha piga chini naona ujana unamsumbua na izi hela za mapema.
Ngeleja inabidi aende can yuo imagine bei ya mafuta sehemu nyingi imerudi kama ya zamani sasa huu si uhuni.
Kwa nchi zilizo serious mwangunga nae piga chini amekula mlungula toka kwa wenye vitalu akaamua kuzarau maamuzi ya bunge kumbe mzee wa Kwela anamchola tuu
 
kuna tetesi kuwa tuhuma za masha zilikuwa kwenye ajenda kwenye mkutano wa kabineti hapo dodoma juzi.
kuhusu ushauri kwa mkuu wa kaya, kazi hiyo anatakiwa kuifanya Dr. Ndumbaro, ambaye anapaswa kuwa mshauri wake wa kisiasa lakini bahati mbaya tunaona anafanya kazi za ukarani. kazi yake kubwa inaonekana siku hizi ni kuchukua minutes kwenye vikao vya mzee. Angalieni luninga kila awapo mzee mtaona hilo.Mshauri gani ambaye wakati huohuo ni karani? Ndumbaro fanya kazi ya kitaalamu umsaidie mkuu wetu kuongoza nchi vizuri

Mpa
 
Nasema hivi... fanyeni uchunguzi mdogo sana... uliziieni makampuni ya Tanzania ya biashara tu... makubwa ambayo yanatumia technology ya access control, ambayo ndiyo hiyo hiyo ambayo itatumika... all most yote yana vifaa vya SAGEM...

Mimi simo.... endeleni na siasa zenu... mheshimiwa Masha kama unasoma thread hii... nipe PM... nikupatie dada za kusema ukweli... Watanzania wakuhukumu kwa kukataa ujinga wa kufuata kanuni hata kama hazilisaidii taifa....

It is just a bullshit.... Masha you are very right brother... kwenye taifa la... ajabu kama hili ukionekana hivyo ujue ndio uko sawa.

Hao dada unawotaka kumpa watasaidia nini. Ama typing error mkuu.
 
Back
Top Bottom