DOKEZO Waziri Jerry Silaa, imekuwaje Kituo hiki cha Mafuta kinafanya kazi wakati ulisimamisha matumizi yake?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari Wakuu?

Nimepita Mitaa ya Mikocheni leo na kukuta Kituo cha Mafuta cha Barrel kilichopo Mikocheni kinaendelea kufanya kazi ikiwa ni takriban mwezi mmoja tangu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kusimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam.

Kituo Mafuta Mikocheni 2.jpg
Kituo Mafuta Mikocheni 1.jpg


Soma: Waziri Silaa apiga marufuku ujenzi holela wa Vituo vya Mafuta na kusimamisha matumizi ya Kituo cha mafuta cha Barrel cha Mikocheni

Napata wakati mgumu sana na kusema Serikali inadharau sana Wananchi wake. Waziri Jerry Silaa alipotembela alisema kabisa yeye si mtoto wa masikini na hawezi kuchukua rushwa japo alitafutwa na wenye Kituo ili waweze kumpatia Milioni 300 na akataa. Lakini leo Kituo hiki kinafanya kazi na tangu baada ya tamko la Waziri hatujawahi kuambiwa nini kilitokea lakini sasa tunaona Kituo kinafanya kazi.

Soma: Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300 | JamiiForums

Nikukumbushe Waziri Silaa, ulipokuwa kwenye Kituo hiki ulisema Mchakato wa kujenga Kituo hicho haujafuata taratibu na pia nikukumbushe kuwa Wananchi tunacholilia ni ujenzi wa vituo vya mafuta karibu na Mkazi ya Watu. Kituo hiki iwapo kutatokea shida hapa ama mlipuko madhara yake hayatakuwa ya kawaida.

Je, nikuulize Waziri ulikuwa unafanya maigizo kama wenzako wengine? Nini kimetokea hadi Kituo hiki kikaendelea kufanya Kazi hatua gani zilichukuliwa? Hukuona haja ya kuufahaamisha Umma kama ambavyo uliufahamisha ulipokwenda pale kusitisha matumizi?
 
Bora hata hicho kina eneo kubwa, kuna kituo kimejengwa kawe stand kwa Mwamposa

Kina eneo dogo pia kimezungukwa na nyumba za hadi unawaza siku ikitokea shida ya moto itakuwaje,
 
Alituhadaa tu, pesa kashabugia hizo ndio maana mambo yanaendelea.

Nguvu ya pesa ni kubwa sana
 
Tuache uchawi. Kwani kinashida gani hadi mkikomalie hivyo?

Tena mleta mada ukitaka kujijua wewe mchawi jiulize, vituo unavyojazia mafuta, vipo kwenye makazi ya mbuzi au watu?

Pia jiulize, anaefungia vituo ni waziri wa Nishati au Ardhi?
 
Back
Top Bottom