Waziri Silaa apiga marufuku ujenzi holela wa Vituo vya Mafuta na kusimamisha matumizi ya Kituo cha mafuta cha Barrel cha Mikocheni

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam na kupiga marufuku ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchi nzima vinavyojengwa kwenye makazi ya watu hatua inayohatarisha usalama wa watu na mali zao.

Waziri Silaa ametoa agizo hilo Desemba 23, 2023 alipoenda kukagua eneo kilipojengwa kituo hicho na aliambatana na Kamati ya ulizi na usalama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

"Kufuatia agizo hili, nawaagiza Wakuu wote wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji nchi nzima wafanye uhakiki wa vituo vya mafuta kwa maana ya viwanja, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, mchakato uliotumika, ukubwa wa viwanja, ukaribu wa kituo kimoja na vituo vingine na ukaribu wa maeneo mengine ya kutolea huduma za jamii, hali ya uendeshaji wa vituo hivyo, taarifa hiyo ifike ofisini Januari 31, 2024" amesema Waziri Silaa.

Pia Waziri Silaa amewaagiza wafanyabiashara ya mafuta nchini wafanye uhakiki wa vituo vyao na Mafuta, mchakato wa namna walivyopata ardhi wanayotumia na kuwasilisha taarifa hiyo Ofisini kwake ifikapo Januari 31, 2024.

Aidha, Waziri Silaa amesema ni vema watumishi wa Ardhi na wafanyabiashara hiyo waheshimu Sheria za nchi kwa vitendo kwa kuwasikiliza watu wasio na sauti ili wapate haki zao katika masuala ya ardhi.

"Rais Samia Suluhu Hassan ni mtu wa haki, anataka watu wapate haki, ameniteua mimi kusimamia haki, hebu tusimamie Sheria, kwa mdomo tukisema tunamuunga mkono Dkt.Samia Suluhu Hasan, lakini tufanye kwa vitendo kwa kuwasililiza wale 'the voiceless, sisi tumewekwa hapa kuwa voice of the voiceless" amesema Waziri Silaa.

Naye mkaazi wa eneo hilo la Mikocheni Bw. Stephen Rupia amesema wananchi wa eneo hilo hawakushirikishwa kwenye hatua yeyote ambayo ilitakiwa wananchi washirikishwe.

"Tupo hapa eneo hili lilikuwa na ukuta na miti mbele na lilikuwa eneo la mtu kwa matumizi yake, hatukuona bango la kubadilisha matumizi ya eneo hili kujenga kituo hiki cha mafuta" amesema Bw. Rupia.

Akizungumza kwa niaba ya mmiliki wa kituo hicho cha Mafuta Mhandisi Stanley Kitundu amesema wameyapokea maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ya ardhi na watayatekeleza na kuongeza kuwa kituo chao kimekamilika kwa asilimia 100 lakini kilikuwa hakijaanza kufanyakazi.




IMG_8606.jpeg

IMG_8605.jpeg


Pia soma; Kuongezeka kwa Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kwenye makazi ya watu Serikali inasubiri ya Morogoro yatokee ndio ichukue hatua?
 
Aisee
Kwa kweli imetosha...
Wabongo sasa kila mtu anataka kufungua kituo cha mafuta
 
Sema kipande hicho wapo majirani nao wazito na wengine walikuwa kwenye mfumo...shuguli
Barrel naona shuguli haikuwa ndogo
Huu upinzani nlitamani angeupata jamaa wa lake oil

Ova
 
Back
Top Bottom