Dar: Wananchi wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Wananchi wakazi wa Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi, Kata ya Mikocheni wilayani Kinondoni Dar es Salaam wamelalamikia kujengwa kwa Kituo cha kuuza mafuta cha Barrel Petrol Station karibu na makazi yao.

Kituo hicho kinajengwa katika Barabara ya Senga, Mtaa wa Ally Hassan Mwinyi Kata ya Mikocheni.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa huo, ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema sheria ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi haikufuatwa kabla ya ujenzi huo.

Mwananchi huyo ambaye amejitambulisha kuwa yeye ni mtaafu serikalini, alisema kabla ya kuanza kwa ujenzi huo, sheria inamtaka mtu anayetaka kubadilisha matumizi ya ardhi kushirikisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka matangazo eneo la wazi kwa muda wa siku 21 ili kama kuna pingamizi litolewe.

“Haya mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika eneo hili haikutushirikisha, matangazo hayakuwekwa. Tumekuja kushtuka ujenzi umeanza.”amesema mwananchi huyo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Profesa Anna Tibaijuka amesema kituo hicho cha mafuta kinajengwa kwenye makazi ya watu kinyume cha sheria.

“Kwanza barabara hii si barabara kuu, hii ni access road (barabara ndogo ya mtaani), huyu anajenga kituo cha mafuta, yatakuja magari maroli makubwa hapa hakuna hata nafasi, barabara hii ni finyu sana, na si eneo zuri kwa usalama na afya za wananchi ” alisema Profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka ambaye amepata kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kuwa suala hilo tayari wamelifikisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye analishughulikia.

“Tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya ameanza kulishughulikia kwa kufika eneo kinapojengwa kituo hiki cha mafuta, tunaamini suala hili litapata ufumbuzi.”aliongeza Profesa Tibaijuka.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amekiri kupokea malalamiko hayo na wananchi wa Mikocheni.

“Kweli nilipokea malalamiko ya wananchi hao, jana nilikwenda kujionea mazingira ya kituo hicho kinachojengwa, nilichokigundua kampuni inayojenga kituo hicho inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha Baraza la Mazingira (NEMC).

“Ni kweli nilipokea malalamiko ya kituo cha mafuta kujengwa katika makazi ya watu, jana nilikwenda (Novemba 14,2023) kujionea mwenyewe.

“Nilichokigundua ni kwamba hiyo kampuni inavyo vibali vyote vya ujenzi kikiwamo cha NEMC (Baraza la Mazingira), hatua inayofuata sasa ni kuangalia kama zile hatua za utoaji wa vibali hivyo ulifuatwa au kuna kilichokosewa. Baadaye nitakwenda kuwaeleeza wananchi tulikofikia”alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni.

Mmoja wa makandarasi wanaosimamia ujenzi wa Kituo hicho (jina tunalo), alipopigiwa simu kuzungumzia suala hilo, aliahidi kupiga simu baadaye. “Nitakupigia, subiri”ulisomeka ujumbe wa simu kutoka kwa mkandarasi huyo.
IMG-20231115-WA0022.jpg
IMG-20231115-WA0021.jpg
IMG-20231115-WA0020.jpg

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mikocheni kuhusu madai ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika makazi ya watu.
 
MFANO WA BANGO LA KUSUDIO LA KUBADILI MATUMIZI YA ARDHI

Mimi………………………………wa S.L.P…………… Dar es Salaam, mmiliki halali wa Kiwanja

namba………Kitalu………………............Ninakusudia kubadili matumizi ya kiwanja changu kutoka

makazi pekee na kuwa………………………….Yeyote mwenye pingamizi na mabadiliko haya awasilishe

pingamizi lake kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ndani ya siku 30 kuanzia leo

Tarehe………………………………………. mpaka Tarehe…………………
 
Jkt napo mlalakuwa wamejenga karibu na makazi ya watu naona watu
Hapo wamewashindwa
Vituo vingi sahv vilivyojengwa viko karibu na makazi
Kinondoni Road sahv napo kuna sheli inakuja njia ya kuelekea mataa ya salender
Ukienda huko tandale ndy balaaa

Ova
Jina la kituo si umeliona lkn?
 
Back
Top Bottom