Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,996
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi.

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu.

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.

I wish you a Merry Christmas 😀

======

Dar es Salaam

“Nimekataa Rushwa ya Tsh. Milioni 300”- Waziri wa Ardhi Mhe . Jerry Silaa

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa, ametangaza kusitisha matumizi ya kituo cha mafuta cha Barrel kilichopo Mikocheni, mkoani Dar es Salaam, kutokana na kituo hicho kujengwa bila kufuata utaratibu wa Wizara hiyo.

Mhe. Silaa amesema hayo alipotembelea eneo hilo, kilipojengwa kituo hicho, ambapo amebainisha kuwa, kuna watu walimfuata wakitaka kumpa rushwa ya Tsh. Mil. 300/= ambazo amedai amezikataa huku akibainisha kuwa ukichukua rushwa kila kitu utaona kipo sahihi.

Waziri huyo pia amewaagiza Wakuu wa Idara wa Ardhi na Mipango Miji nchi nzima kufanya uhakiki wa vituo vya mafuta vilivyo kwenye maeneo yao, kwa kuangalia matumizi yake pamoja na mchakato uliotumika kupatikana kwa viwanja hivyo
 
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni

I wish you a Merry Christmas
Mrudisheni Lukuvi Ardhi
 
Namfahamu Jery Slaa vyema. Naona ametamka kwamba hapokei rushwa. Fine kwa sasa akiwa waziri anaweza akaamua kuridhika na anachopata akakaa mbali na watoa rushwa.

Ila naomba kumkumbusha Jerry kwamba ubunge wake aliupata kwa rushwa. Hivyo kama hapokei rushwa anapaswa kwanza kuukataa ubunge wake. Rushwa ni rushwa tu....ni kitendo cha kupokea kisicho haki yako ambapo for sure ubunge siyo halali yako.

Lakini eneo la pili kwenye rushwa ya Ardhi namkumbuka mama Mabula, alijipambanua kwamba hapokei rushwa ila skendo za rushwa zilikuwa kumwondoa ofisini leo hana uwezo hata wakuwa tena mbunge.

Jeryy mapigano ya rushwa ni matendo siyo maneno, wewe baba yako alikuwa rubani na tunakubali wewe ni familia bora ila hakuna familia imewahi kuridhika na kile walichonacho, mwanao kufika hapo alipo katika Chipukizi kuna rushwa imetembea and you know.

Wapo watoto wazazi wao walikuwa marais na wengine watoto wa mawaziri lakini ndio vinara wa rushwa nchini.

Tuambie lini umeachana na rushwa ukiwa mwanasiasa? Labda useme umeacha kuchukua fedha za ardhi na viwanja
 
Back
Top Bottom