Hili la vituo vya mafuta maeneo ya makazi halikubaliki

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,033
Wadau nawasalimu.Wakati Waziri wa Ardhi Jerry Silaa anateuliwa moja ya hotuba yake ilikuwa kupambana na Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kinyemela kwa maana Tajiri ndio anaamua Watendaji wa Serikali wanabadilisha Matumizi kutoka yaliyokuwepo kuwa Kituo cha Mafuta bila kujali ATHARI na Taratibu za Sheria za Mipango Miji.

Nilitarajia Waziri baada ya kuwataka Makamishna wasaidizi wampelekee Report ya Vituo vyote vya Mafuta Mikoani mwao nanma Vilivyopatikana Waziri angeueleza Umma wa Watanzania Taarifa ya Report ile lakini YUPO KIMYA Kama vile hakuagiza.

WATANZANIA madhara ya Vituo vya Mafuta kwenye Makazi ya Wananchi ni janga kubwa kwani linaweza kuua Wananchi na Mali zao kwa ajili ya Biashara ya Mtu mmoja. Tukumbuke kuwa huyo mwenye Kituo haishi hapo yeye na familia yake hivyo watakaokufa ni wananchi wengi. Mifano ipo mingi Juzi Nchini Kenya kuna Kituo cha Mafuta kimelipuka na kuua wananchi.

Leo pale Kigamboni kuna MATANGI MAKUBWA ya mafuta katikati ya Makazi.Nenda Sumbawanga kuna kituo cha Mafuta kinajengwa katikati ya Makazi inapakana na Jengo la ccm wakati mita 30 kuna vituo vingine vya Mafuta. Napata shida kuamini kama Nchi hii kweli ina Maafisa Mipango Miji waliosoma na kupewa Degree?

Waziri wa Ardhi acheni SIASA kwenye Majanga ya Moto kuna siku Wananchi watateketea kwa Uzembe wa Wizara yako. HILI LA VITUO VYA MAFUTA kwenye MAKAZI halikubaliki.
 
Mkuu ni kuwafanyia push back, hii ndio lugha watakusiliza kinyume cha hapo yatakua yale yale ya kulalama humu
 
Sheria ya kujenga vituo vya mafuta na gesi zinasemaje?

Hapa majanga kwanza yatokee ndipo utasikia MALAIKA WA TANZANIA WAKILAANI AU KUWAKAMATA WAMILIKI WA VITUO HIVYO.

Utasikia tuna masterplan ya miji na majiji.

Complete nonsense
 
Na haliepukiki Mawaziri wanatoa matamko ambayo hawayafatilii wizara ya nishati na ardhi ni wahusika wakuu katika hili, binafsi naona Lukuvi angeliweza hili ana uthubutu
 
Sidhani hata kama CHADEMA wanaweza kuja kutoa utatuzi kwa hili.

Sijaona hata bango moja kwenye maandamano yao linalogusia suala hili.

Rushwa ni mbaya sana, na haina Chama.
 
Wadau nawasalimu.Wakati Waziri wa Ardhi Jerry Silaa anateuliwa moja ya hotuba yake ilikuwa kupambana na Ujenzi wa Vituo vya Mafuta kinyemela kwa maana Tajiri ndio anaamua Watendaji wa Serikali wanabadilisha Matumizi kutoka yaliyokuwepo kuwa Kituo cha Mafuta bila kujali ATHARI na Taratibu za Sheria za Mipango Miji.

Nilitarajia Waziri baada ya kuwataka Makamishna wasaidizi wampelekee Report ya Vituo vyote vya Mafuta Mikoani mwao nanma Vilivyopatikana Waziri angeueleza Umma wa Watanzania Taarifa ya Report ile lakini YUPO KIMYA Kama vile hakuagiza.

WATANZANIA madhara ya Vituo vya Mafuta kwenye Makazi ya Wananchi ni janga kubwa kwani linaweza kuua Wananchi na Mali zao kwa ajili ya Biashara ya Mtu mmoja. Tukumbuke kuwa huyo mwenye Kituo haishi hapo yeye na familia yake hivyo watakaokufa ni wananchi wengi. Mifano ipo mingi Juzi Nchini Kenya kuna Kituo cha Mafuta kimelipuka na kuua wananchi.

Leo pale Kigamboni kuna MATANGI MAKUBWA ya mafuta katikati ya Makazi.Nenda Sumbawanga kuna kituo cha Mafuta kinajengwa katikati ya Makazi inapakana na Jengo la ccm wakati mita 30 kuna vituo vingine vya Mafuta. Napata shida kuamini kama Nchi hii kweli ina Maafisa Mipango Miji waliosoma na kupewa Degree?

Waziri wa Ardhi acheni SIASA kwenye Majanga ya Moto kuna siku Wananchi watateketea kwa Uzembe wa Wizara yako. HILI LA VITUO VYA MAFUTA kwenye MAKAZI halikubaliki.
Kwasumbawanga kama mahotel uwekezaji akuna sasa siwameamua kujiwekeza kwenye fuel station waache acha roho mbaya bwana.
 
Back
Top Bottom