Waziri Jafo apendekeza Stendi mpya ya Mbezi ipewe jina la Dkt. John Magufuli

Itaongeza ufanisi ?, Au ndio muendelezo wa kusifia na kupeana pongezi ?

Mi nashauri lipewe jina la viongozi / watu / matokio yaliyopita au legends waliopita huyu tutaanza kumpa pongezi zake miaka 20 ijayo baada ya kufanya upembuzi yakinifu...

Tusipoangalia tutashindwa kutofautisha sehemu A na B sababu zote zitakuwa zinaitwa jina moja.., kuanzia stand, magari hadi abiria
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema kutokana na stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya kimataifa, anapendekeza ipewe jina la Dkt. John Magufuli kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya, ambapo amesema atamuomba Rais aridhie ombi hilo.

Kama amependekeza iitwe kwa jina la Rais JPM kwakuwa ina Hadhi ya Kimataifa je, ingekuwa ina Hadhi ya Kiuswahili jina gani lingependekezwa?
 
Kuna masinior wengi sana waliolipambania taifa hili,hawa Mawaziri waoga tumewachoka.....kama vipi iitwe Chato tu
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema kutokana na stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya kimataifa, anapendekeza ipewe jina la Dkt. John Magufuli kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya, ambapo amesema atamuomba Rais aridhie ombi hilo.

Masikini Kikwete
 
Ikiwezekana wabadilishe na jina la nchi kabisa liwe Jamhuri ya Muungano wa Magufuli. Nadhani hii itafikisha shukrani zaidi kwa Mheshimiwa maaana kabla yake tulikuwa hata hatuvuti hewa lakini toka kuingia yeye madarakani tunavuta oxygen kwa wingi, mvua zimeongezeka na hata ardhi imekuwa na rutba zaidi.
Mkuu nimecheka hapa kwenye mwendokasi hadi nimepatapo pisi
 
Back
Top Bottom