Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya Iringa ili ipewe jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya CCM.
Makonda amenukuliwa akisema “Hapa kuna Kaka yangu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya MimI nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau Mwana Mafinga Chongolo awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu"
Makonda ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20.
Credit - MillardAyo