Waziri Jafo apendekeza Stendi mpya ya Mbezi ipewe jina la Dkt. John Magufuli

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema kutokana na stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya kimataifa, anapendekeza ipewe jina la Dkt. John Magufuli kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya, ambapo amesema atamuomba Rais aridhie ombi hilo.

1611581597644.png

============

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo ameelekeza Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha Stendi Mpya ya Mabasi ya Mbezi Luis inaanza kutumika muda wowote kuanzia sasa baada ya kujiridhisha kukamilika kwa miundombinu yote muhimu kasoro Barabara ya kuingia kituoni hapo ambayo ipo hatua ya mwisho.

Waziri Jaffo amesema hayo wakati alipofanya ziara Katika Stendi hiyo ambapo amesema muda wowote ambao TANROAD watathibitisha kuwa Barabara ya kuingia kituoni hapo imekamilika ni vyema kituo kikaanza kutoa huduma.

Aidha Waziri Jaffo amesema Kutokana na Stendi hiyo kuwa na hadhi ya kimataifa anapendekeza ipewe jina la Rais Dkt. John Magufuli Kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitiada alizofanya ambapo amesema atamuomba Mhe. Rais aridhie ombi hilo.

Hata hivyo Waziri Jaffo amemuelekeza Mkandarasi anaejenga eneo la maegesho ya magari madogo kuhakikisha anakamilisha kazi ndani ya wiki mbili kuanzia leo huku akitaka taa zifungwe ndani ya wiki moja kuanzia leo.

Pamoja na hayo Waziri Jaffo ametoa pongezi kwa uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa usimamizi madhubuti uliosaidia Stendi hiyo kukamilika ikiwa na ubora uliokusudiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bi.Spora Liana amesema kazi zinazoendelea kwa Sasa ni Ufungaji wa Viyoyozi, Lifti, ufungaji wa taa na Vifaa vya matangazo, uunganishwaji wa maji kwenye Vyoo na miundombinu mingine ambayo nayo ipo hatua ya mwisho kukamilika na kusisitiza kuwa kwa Sasa Stendi inaweza kuanza kutumika.
 
Mi naona abadilishe jina na mkewe pia. Kwa sababu ya juhudi
Ikiwezekana wabadilishe na jina la nchi kabisa liwe Jamhuri ya Muungano wa Magufuli. Nadhani hii itafikisha shukrani zaidi kwa Mheshimiwa maaana kabla yake tulikuwa hata hatuvuti hewa lakini toka kuingia yeye madarakani tunavuta oxygen kwa wingi, mvua zimeongezeka na hata ardhi imekuwa na rutba zaidi.
 
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema kutokana na stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya kimataifa, anapendekeza ipewe jina la Dkt. John Magufuli kama sehemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya, ambapo amesema atamuomba Rais aridhie ombi hilo.

View attachment 1685905
Ingependeza sana kama angepewa Jina la Matonya, raia mwenye ulemavu wa macho lakini mwenye akili na ubunifu wa kuishi aliyewashinda viongozi wengi waliojaribu kumuondoa toka Dar es Salaam kwa nguvu bila kutumia akili na busara.

Huo Mradi ni wa wakazi wa Dar es Salaam na ndio wanatakiwa kuombwa, kama mimi ninavyomwombea Matonya, maana anayepewa zawadi haombwi bali anapewa tu atupe kama hataki.

Hao wengine kama wamefanya lolote la maana kwa kujitolea na kwa fedha toka mifukoni mwao, basi wapewe heshima kwa kuipa majina yao miradi hiyo ikikamilika. Kokote aliko sasa, ingefaa wakazi wa Dar wampe heshima hiyo sote na wa bara tufurahi.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom