Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. John Pima na wenzake wameshinda rufaa ya kupinga kifungo cha miaka 20 jela

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma:
 
hizi kesi zishakua za mchongo!kila kesi serikali inashindwa ktk rufaa
 
Michezo tu hiyo nia ilikuwa sio kuwafunga bali nia ni kuwazuga wananchi ndiyo maana hata hiyo kesi wameipeleka mahakama isiyo stahili.
 
Sinema hizo

Kesho utasikia hao wamepewa vyeo

Serikalini nchi hii inaenda bora liende tu

Ova
 
Aiseee! Hii hukumu itachochea wizi na Ufisadi kwenye Halmashauri! PM Majaliwa alitembelea Arusha alijionea Ufisadi wa kutisha akiongozwa na RC Mongela! Leo Majizi yameachiwa! Waziri Mchengerwa ana kazi nzito kupambana na Majizi kwenye wizara yake! Serikali inapeleka pesa nyingi kwenye Halmashauri!
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
Kama wana hatia basi hukumu ikasomwe na huyo hakimu mwenye mamlaka siyo kuwaachia.
Kingine hapo mteule wa rais ni mmoja unaachiaje wote?
 
Huyo hakimu aliyetoa hukumu ya mwanzo kabla ya Rufaa, hakujua kuwa kesi sio hadhi yake. Msitufanye mapopoma jamani.
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
Sarakasi tu hamna lolote msitufanye watanzania wote hamnazo, mashitaka yameandaliwa na ofisi ya DPP, Kwani hawakujua kuwa Pima ni mteule wa Rais hivo kinahitajika kibali maalum
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.
 
Aiseee! Hii hukumu itachochea wizi na Ufisadi kwenye Halmashauri! PM Majaliwa alitembelea Arusha alijionea Ufisadi wa kutisha akiongozwa na RC Mongela! Leo Majizi yameachiwa! Waziri Mchengerwa ana kazi nzito kupambana na Majizi kwenye wizara yake! Serikali inapeleka pesa nyingi kwenye Halmashauri!
Sote tunajuwa ilikuwa geresha la mama Samia kudanganya kwamba wanaingia
 
mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Maneno mazito katika hukumu hii ya Dkt. John Pima mkurugenzi. Mteule wa rais anakuwa na immunity ya aina fulani.

Sasa hii ziara ya muenezi itakuwa na matokeo chanya au ni maigizo. Maana wateule inakuwa ngumu kungoka kazini.

Toka maktaba :

12 February 2025​

KESI YA KUPINGA WATU KUSHTAKIWA KWENYE MAHAKAMA ZISIZO NA MAMLAKA YAAHIRISHWA MAHAKAMA YA RUFAA

View: https://m.youtube.com/watch?v=igFJxQi48PE

Wakili msomi Paul Kisabo kwa niaba ya Onesmo OleOlengurumwa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) imeahirishwa baada ya benchi la majaji 3 wa mahakama ya rufaa kuwemo jaji aliyesikiliza kesi ilipokuwa katika mahakama kuu ya Tanzania.

Mawakili wa pande mbili walikubali kuwa kupandishwa cheo jaji wa mahakama kuu mheshimiwa jaji Masoud aliyesikiliza kesi hiyo ngazi ya Mahakamu Kuu kutaathiri mwenendo wa kesi akiwemo tena kama jaji wa Mahakama ya Rufaa kusikiliza tena kesi hiyo ya kihistoria.

Kesi ya msingi inayokatiwa rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania :
Feb 13, 2020
February 13, 2020
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amefungua kesi namba 36 ya mwaka 2019 dhidi ya Mwanasheria mkuu wa serikali katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ya Dar es Salaam akipinga watuhumiwa wa mbalimbali nchini humo kufikishwa kwenye mahakama zisizokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi zao (committal proceedings).

Katika kesi hiyo, mwanaharakati huyo wa haki za binadamu nchini Tanzania, anapinga watuhumiwa wa makosa mbalimbali kukamatwa bila upelelezi kukamilika.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa leo Februari 13, 2020 kwa mara ya kwanza majira ya saa saba mchana mbele ya majaji watatu, Jaji Masoud, Jaji Mlyambina na Jaji Juliana Masabo.

Akizungumzia msingi wa kesi hiyo aliyoifungua tangu Desemba 16, 2019, Olengurumwa amesema kuwa analenga kuiomba Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa tamko la kufuta vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 (Toleo la mwaka 2002), ambavyo amedai vinakiuka haki na uhuru wa watuhumiwa, kuminya utawala wa sheria, na kufifisha mchakato mzima wa uendeshaji wa kesi kwa usawa, sababu ambayo ameitaja kuwa inahamasisha matumizi mabaya ya mamlaka ikiwemo kufanya upelelezi kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Olengurumwa amesema kesi hiyo pia inalenga kuiomba mahakama hiyo kutoa tamko kwamba kifungu namba 178, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 256, 257, 258 na 259 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 (Toleo la mwaka 2002) kuwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba vifungu hivyo vipaswa kufutwa na kuondolewa kabisa.

Olengurumwa ambaye ni msomi wa sheria na mchambuzi wa sera za umma nchini Tanzania ameeleza zaidi kuwa mtuhumiwa anapofunguliwa mashtaka kwenye mahakama ambayo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi yake, mtuhumiwa huwa haruhusiwi kusema chochote, hivyo humfanya akose haki yake ya msingi ya kusikilizwa kwa wakati.

Akifafanua zaidi amesema kuwa sheria nayo pia bado haijaweka utaratibu wa namna ya kuhakikisha upelelezi unafanyika haraka na kwa wakati ili kuhakikisha kwamba mtuhumiwa anafikishwa mbele ya mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi yake.

Akinukuu kifungu namba 178 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 (Toleo la mwaka 2002), Olengurumwa amesema kifungu hicho kinasema kuwa, "pale ambapo kesi itaunguliwa kwenye mahakama ambayo haina mamlaka ya kuisikiliza, baada ya upelelezi kukamilika, mahakama hiyo inapaswa kutoa amri ya kesi hiyo kwenda kusikilizwa mahakama kuu."

Olengurumwa ameelezea changamoto ya kifungu hicho. ambapo amedai kuwa, kwakuwa upelelezi umekuwa ukichukua muda mrefu kwenye kesi nyingi ama pengine kutokamilika, kifungu hiko cha 178 kimekuwa hakina uhalisia, hivyo kinastahili kufutwa.

Olengurumwa ameeleza kuwa Ibara ya 64 (5) ya Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 inaweka bayana kuwa, Bunge linawajibu wa kutunga sheria ambazo hazikinzani na Katiba.

Vilevile, Olengurumwa ameeleza zaidi kuwa, serikali inawajibu wa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili wameshinda rufaa waliyokata kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Hukumu hiyo imesomwa leo Ijumaa, Februari 16, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna.

Mbali na Dk Pima, wengine walioachiwa huru ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Katika uamuzi wake huo, Lukuna amesema mahakama imeona mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo inayomhusu mteule wa Rais, bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

Chanzo: Mwananchi
Kama hakimu alipokea maelekezo toka juu basi wasahau watasumbuka sana bora wakae miaka yao iishe
 
Back
Top Bottom