Naibu Waziri Dkt. Dugange: Halmashauri ya Mwanga Yawasilisha Andiko la Bilioni 3.2 Ujenzi wa Stendi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
NAIBU Waziri TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Halmashauri ya Mwanga imeandaa andiko lenye thamani ya Sh.bilioni 3.2 na kuliwasilisha Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa wilayani humo.

Mhe. Dkt. Dugange ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha sita mkutano wa 13 unaoendelea jijini Dodoma.

"Mhe Spika Serikali inatambua ufinyu wa stendi ya magari katika Halmashauri ya Mwanga lakini tayari Ofisi ya Rais-TAMISEMI tumepokea andiko lenye thamani ya Sh. bilioni 3.2 tokea Agosti mwaka huu na hatua iliyopo hivi sasa ni ya watalaamu wetu wizarani kuendelea na mapitio ya andiko hilo kulingana na vigezo" - Dkt. Dugange.

F-QjQ_dWYAAklAq.jpg
F-QjQ_eXIAAyWMp.jpg
F-QjQ_aXoAAvFE_.jpg
F-QjQ_bXoAAVEHb.jpg
 
Back
Top Bottom