Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 3, leo Agosti 31, 2023.

Ratiba:
  • Dua
  • Hati za kuwasilisha Mezani
  • Maswali
  • Hoja za Serikali

WAZIRI GWAJIMA: MILA YA KUWEKEZA MKE AKIWA TUMBONI INACHOCHEA UKATILI WA KIHISIA
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima amesema mila hiyo ina madhara, inachochea ukatili wa kihisia, ndoa za utotoni na inamnyima mhusika haki ya msingi ya kumchagua mwenza wa kuishi naye umri utakapofika.

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya hoja ya Mbunge Maryam Azan Mwinyi aliyehoji mpango wa Serikali kutokomeza Mila ya kuwekeza mke akiwa tumboni kwa mama hasa katika maeneo ya Mikoa ya Manyara na Arusha.


Luhaga Mpina: Serikali inasema Uwekezaji umeongezeka, je dola zimeenda wapi?
Mbunge Luhaga Joelson Mpina akichangia hoja Bungeni kuhusu Azimio la Bunge kuhusu mapendekezo ya kuridhia Hitifaki ya Biashara ya Huduma ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Mwaka 2012.

Amehojia “Rais Jakaya Kikwete alisaini mkataba huo mwaka 2012, leo unarejeshwa kuna marekebisho gani? Dola nazo zimeadimika, Serikali inasema Wataelii wameongezeka na Uwekezaji umeongezeka, Dola zimeenda wapi? Serikali lazima iwajibike kwa kutatua uhaba wa Dola Nchini.


MSITUME NYARAKA ‘WHATSAPP’ Ni marufuku
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema sheria inayosimamia nyaraka za Serikali inaelekeza kuwa mawasiliano ya Serikali yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo.

Kufuatia kuwepo kwa sheria hiyo, Naibu Waziri Kikwete amewaonya watendaji wa Serikali ambao wanatumia njia ambazo sio rasmi kutuma nyaraka.

“Haitokuwa sawa na ni marufuku ya Serikali kuwasilisha au kutumiiana ‘Documents’ za Serikali kupitia njia ya WhatsApps na njia nyingine zisizo rasmi, isipokuwa kwa maelekezo ambayo yatakuwa yametolewa vinginevyo katika mamlaka,” amesema Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.

Ameyasema hayo Bungeji jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Janejelly Ntate James ambaye amehoji uhalali wa matumizi ya makundi ya WhatsApp kutumiana nyaraka.

Aidha, Naibu Waziri Kikwete amelihakikishia Bunge kuwa Serikali bado inaendelea kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itaileta Serikali yote katika adabu ya utendaji.
 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema Sheria inayosimamia masuala ya nyaraka za serikali inaeleza wazi kwamba mawasiliano yote ndani ya serikali ni lazima yafanyike kwa njia ya barua na wala haielekezi vinginevyo.

Kikwete ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 31, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Jane Jerry na lile la nyongeza la Mbunge mwingine wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda waliotaka kujua neno la serikali dhidi ya watumishi wa serikali wanaotumia mtandao wa WhatsApp kutuma taarifa za serikali hali inayosababisha wakati mwingine nyaraka za serikali kuvuja mitandaoni.

"Sheria inayosimamia nyaraka za serikali inaelekeza wazi kwamba mawasiliano ya serikalini yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo. Si sawa na ni marufuku kwa watumishi wa serikali kuwasilisha au kutumiana nyaraka za kiserikali kupitia njia ya WhatsApp na njia nyingine zisizo rasmi isipokuwa kwa yale maelekezo yatakua yametolewa vinginevyo katika mamlaka." Alisema Naibu Waziri Kikwete.

Katika swali la nyongeza la Mbunge mwingine wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda aliyeuliza serikali kama kwa kufanya hivyo itakuwa nje ya teknolojia na kuitaka serikali kuweka mifumo itakayolinda nyaraka za serikali lakini pia itakayopeleka taarifa kwa haraka kupitia teknolojia.

Katika kujibu swali la Mwakagenda, Naibu Waziri Kikwete amesema mpaka sasa baada ya kupitisha Sheria No. 10 ya 2019, serikali imetengeneza na kujenga mifumo ya TEHAMA zaidi ya 860 kwa ajili ya kusimamia utendaji wa serikali na bado serikali inaendelea kutengeneza mifumo mbalimbali ya usimamiaji ambayo italeta adabu ya kiutendaji serikalini.
 

Attachments

  • IMG-20230831-WA0047.jpg
    IMG-20230831-WA0047.jpg
    50.9 KB · Views: 1
Siri ya Serikali...., Wanamficha nani na Wanaficha nini ? Huu ni muedelezo wa kujiona wao ni Bora zaidi; Huo muda wakuficha wangeutumia kuwajibika wala wasingehitaji kuficha vitu bali wangevianika kama magazeti
 
Kwahiyo na matangazo ya kazi, kuitwa katka interview na kuitwa kazini yatumwe kwa emails
 
Back
Top Bottom