Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 1,773
- 3,878
- Thread starter
- #61
Duh hatari.. Kukaa na wanawake hiyo lazima ikuharibu kisaikolojia pakubwa sanaKwa mwanaume dawa ya mapenzi ya uhakika ni Tigopesa. Hayo mambo ya uchawi wa mapenzi wanatakiwa kufanya wanawake na sio wanaume
. Hao wazee ni mamwinyi na hawanaga akili hao. Kule Liwale kuna mganga mmoja wa mapenzi anatumia UCHAWI WA MTO ( Huu unatajwa ndio uchawi wenye nguvu sana kwenye kumuita mpenzi. Ni uchawi unatengenezwa kwa kutumia tope za kwenye mto unao tembea. Tope zinachukuliwa kwenye pande mbili za mto kulia na kushoto then zinakaushwa na madawa ya porini na panzi walionaswa wakiwa wanajamiiana wakafungwa wakafa hivyo hivyo wakiwa wamenasana wakifanya mapenzi.. Huu uchawi hutumika kumchomea mpenzi anakufuata kesho yake)
Ila sasa kwa huyo mganga ukienda kwake mwanaume halafu akagundua shida yako ni mapenzi ata kwambia ukasubirie nje ukae sehemu ambayo wateja wake wanawake wanasubiria zamu ya kuingia Kilingeni.. Hapo kwake ana wateja wengi sana ,wanawake kwa wanaume. Wanawake wanasubiria sehemu Yao na wanaume wanasubiria sehemu Yao.. Msaidizi wake anakuwa anakuja kuita majina kwa namba ataanza na wanawake watatu kisha baadae wanaume watatu hivyo hivyo Hadi usiku. Sasa wewe kidume ukienda kwa ajili ya dawa ya mapenzi anakuweka pamoja na wanawake na zamu yako inakuwa mwishoni kabisa na usipo angalia zamu yako inaweza kuwa baada ya siku tatu..
Anakuweka ukae pamoja na wanawake kwa sababu amekudharau amekuona wewe akili zako ni kama za wanawake na haustahili kuchangamana na wanaume.
Ni mwanamke ndio anaenda kwa mganga kutafuta dawa za mapenzi. Mwanaume anaenda kutafuta dawa za biashara
