Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 3,824
- 5,812
Now mkuu tofautisha Nchi na urithi wa mali these are two different things ni impossible kufanya kuwa mfano wa kuthibitisha ulichoandika ni sahihi in anyway.Urithi ungekuwa ujinga hii nchi ingekuwa Yenu??
Itashangaza mtu ni msomi asielwe concept ndogo niliyoieleza, pia itashangaza Kama mtu anaumri wa zaidi ya miaka 25 asielewe mantiki ha kile kilichozungumzwa hapa.
Na Nchi sio urithi sababu sio mali ya mtu mmoja bali kila mtu aliyekuwepo nchini basi na yeye ataitwa mwananchi, au unataka kusema kuna mtu mmoja ambaye ameturithisha nchi?
Na ili kukuprove wrong vizuri na mfano wako wa nchi kama kithibitisho cha mtoto kupewa urithi.
Ni hivi yoyote aliyezaliwa nchini ni mwananchi na kuwa mwananchi haaimaanishi kwamba unaimiliki nchi bali ni mshiriki tu na ndio maana unalipia kodi ya ardhi, kodi za vichwa na kodi za aina nyingine, kuna viongozi na serikali, kuna sheria na kanuni.
Na pia ukifanya Utumbo wowote basi unahukumiwa, kifo, kifungo cha maisha nk
Mpaka hapo unaona hiyo nchi ni yako au bure?
Kwanini ufanyi unachokitaka kama ni yako ambayo umerithishwa sijui na nani?
Sababu nchi haiwezi kuendelea bila ya wananchi kufanya chochote ili kuongeza chochote kwenye nchi yao.
Ni lazima ufanye kazi ulipe kodi ili zijengwe shule, hospitali, maji na huduma nyingine za kijamii ambazo zitafanya nchi iendelee na kuweza kusurvive au Nchi itakufa kwa umasikini wa kutisha.
Na kama ilivyo nchi ndivyo ilivyo familia na mali ya urithi.
ni lazima isimamiwe means ipate uongozi na watoto wafanye chochote ili kuendeleza na kukuza hizo mali za urithi ili familia ikue.
Au kila mtu akipewa na kufanya anachokitaka lazima mali ipotee na umasikini kushamiri kwenye familia.
In simple terms as possible ni kuwa mali haitakiwi kurithishwa bali inatakiwa kuendelezwa na watoto.
Ni kama zile familia tajiri ambazo baba akifa na kugawa urithi kwa watoto basi ghafla familia inageuka masikini.
Again urithi ni ujinga unaofanya familia izidi kuwa masikini hii sio opinion bali ni fact na ukweli. utakataa only kama umeamua kukaza kichwa sababu ndivyo ulivyoamua kuamini.