Je, wazazi mnaiona kesho ya watoto wenu?

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
518
901
Samahani jamani sikuanza na salamu sababu kichwa kina mambo mengi, navyosema kichwa namaanisha hiki kilichobeba ubongo, so sitaki ufikirie tofauti.

Nirudi kwenye hoja yangu, leo nimewaza tu kama mzazi, huku nikitambua wajibu wa mzazi kwa watoto wetu, kwani wazazi tunachangia kwa kiasi kikubwa kuandaa kesho ya watoto wetu, nadhani kila mmoja anajua kwamba maisha unayoishi hii leo kwa kiasi kikubwa kuna mchango wa wazazi wako ndio wamechangia wewe kua hivyo.

Je umeshawai kufikiria dunia ya miaka ishirini ijayo itakuaje? Yahani mzazi unatakiwa uwe na jicho la ziada uweze kuona mbali hii itakusidia kuweza kujua ni mazingira gani utamuandalia mtoto wako ili aje kua mtu miongoni mwa watu.

Labda tu niwakumbushe ulimwengu unabadilika Kwa Kasi ya ajabu sana, leo wanasayansi wanaleta vumbuzi za ajabu sana, na vumbuzi nyingine zinatishia mustakabali wa binadamu, Angalia matumizi ya akili bandia AI, kwa ufupi tu niwaambie bahada ya miaka kumi kutakua na vilio vingi sana katika dunia hii, kazi zote zinazofanywa na bindamu jamaa wanatengeneza miroboti inayoweza kuzifanya kazi hizo tena Kwa ufanisi zaidi na tena pasipo kuchoka.

Ukweli ni kwamba dunia ijayo itahitaji watu wabunifu, wavumbuzi na wenye vipaji zaidi, na sio wafanyakazi kwani kazi nyingi zitafanywa na maroboti.

Wazazi inabidi kua makini na elimu mnazo wapatia watoto wenu, kwani tunasema urithi, wa mtoto ni elimu, lakini lazima tuwe makini, je ni elimu gani unamrithisha mtoto ili iweze kumsaidia katika ulimwengu ujao, hizi elimu zenu za kufundishana historia za kina kinjekitile ngwale na biashara za utumwa hazitakua na mashiko kwa dunia ya kesho.

Hivyo kama mnataka watoto wenu wasijekuchapa viboko makaburi yenu inabidi uangalie kwa jicho la tatu ni elimu hipi sahihi utakayomrithisha mtoto itakayomsidia kukabiliana na ulimwengu ujao, ulimwengu utakaokua unatawaliwa na uvumbuzi wa akili bandia.
 
Kama unamihela, mwandae kijana wako jufuata nyao zako au mapema sana chini ya ungalizi wako waanze na wao kuingiza pesa kwa njia wataochagua wenyewe.
Ila kama ndio sisi tunaokamaa na Elimu ndio ufunguo wa maisha, jitahidi kumkazania kwenye masomo ya Sayansi.
 
Back
Top Bottom