Kukosa desturi ya kuandika Urithi na Wosia na kutowajulisha/husisha watoto kwenye biashara/mali unazomiliki kumesababisha matatizo mengi

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Mtu ni magonjwa na kashafika 60 cha ajabu hajaandaa Wosia wowote wala kuandika Urithi, anaacha kivumbi na kutoelewana pindi akifa.

Mtu hawajulishi watoto wake kwamba ana mali fulani, matokeo yake kuna wapangaji wanaweza kujimilikisha nyumba ambazo hawajajenga, watu wanajimilikisha mashamba, n.k.

Mtu ana falsafa za kizamani sana kwamba mtoto inabidi afike miaka 25 hadi 30 ndio amhusishe kwenye biashara zake huku akijua kabisa hata mnyama aliezeeka ni ngumu kumfundisha vitu vipya, Familia kama hizi kibao baba akifariki magari yanapaki yanaota kutu, nimeshuhudia watoto wanaouza hotel iliyowahi kuwa maarufu kwa Bei chee, vijana wanaouza duka waskisikia boss kafariki wanakomba kila kitu, n.k.
 
Kuna la kujifunza hapa hasa sisi ngozi nyeusi.
Utaskia "urithi wako ni elimu" 😂😂

Hio elimu hata wahindi wametuzidi tena mbali mno lakini kwenye suala la mali wapo strict sana kuwa husisha watoto wao.

Mtoto anapokuwa na wazazi ni bahati lakini akiwa na wazazi wenye mali ama biashara zao ni neema kubwa zaidi, ni jukumu la wazazi kumfundisha na kumhusisha mtoto kisha kuandaa urithi mapema ili akiaga Dunia watoto ama mtoto aendekeza utajiri wa kizazi hadi kizazi kwa faida ya vizazi hadi vizazi.
 
Mtu ni magonjwa na kashafika 60 cha ajabu hajaandaa Wosia wowote wala kuandika Urithi, anaacha kivumbi na kutoelewana pindi akifa.

Mtu hawajulishi watoto wake kwamba ana mali fulani, matokeo yake kuna wapangaji wanaweza kujimilikisha nyumba ambazo hawajajenga, watu wanajimilikisha mashamba, n.k.

Mtu ana falsafa za kizamani sana kwamba mtoto inabidi afike miaka 25 hadi 30 ndio amhusishe kwenye biashara zake huku akijua kabisa hata mnyama aliezeeka ni ngumu kumfundisha vitu vipya, Familia kama hizi kibao baba akifariki magari yanapaki yanaota kutu, nimeshuhudia watoto wanaouza hotel iliyowahi kuwa maarufu kwa Bei chee, vijana wanaouza duka waskisikia boss kafariki wanakomba kila kitu, n.k.
mengi si aliandika wosia,lakini ulipingwa mahakamani na ukatenguliwa
 
Back
Top Bottom