Mohammed Dewji: Kurithi inakuja na responsibilities. Adai ni 5% tu ya wajukuu wanafanikiwa kupitia urithi, waliobaki wanapoteza

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,507
8,129
Mfanyabiashara, Mohammed Dewji wiki hii alianza kampeni yake ya 'Mo Cares' akiielezea kama Moo anajali watanzania ikiwemo kuwapa zawadi washindi wataojibu maswali yake. Dewji anasema alitekwa miaka mitano iliyopita na wasiojulikana na anawashuru watanzania wote waliomuombea.

Miongoni mwa maswali aliyouliza ni muanzilishi wa kampuni ya Moo lakini alianza na kutoa elimu juu ya kurithi. Moo amesema urithi ukitoka kwa baba kwenda kwa mtoto ni asilimia 50 tu ndio huwa wanafanikiwa kwenye maisha yao na ni asilimia 5 pekee ya wajukuu wanafanikiwa akimaanisha mali za urithi hupotea na wahusika kuanza upya.

Dewji amesema kurithi ni vizuri lakini pamoja na kurithi zinakuja responsibilities ya kuzikuza. Amesema yeye anashukuru alilirithi lakini ameweza kuzizidisha fedha hizo maradufu ikiwemo kufanya kazi kwa jitahada na nidhamu ya hali ya juu.

Amewaasa wanaorithi inabidi wajitume ili wafanikishe.

Mwisho Moo alitoa jibu mwenyewe kwa kumtaja muanzilishi wa Mohammed Enterprise kuwa ni bibi yake anayeitwa Fatma Hassanali Fazal Dewji na alianzisha biashara hiyo mikoa ya Singida, Dodoma na Arusha na baadae baba yake Ghulam Dewji alipokea kijiti na baadae kumpa yeye Moo mwaka 1998.
 
Mwaka gani ilianza ME?

Hizo pesa za uanzilishi alipatia wapi ?

Yeye ni muhindi huku Tanganyika kizazi chake kilifika lini ?

Nini sababu ya wao kufika huku Tanganyika ?
 
Mwaka gani ilianza ME?

Hizo pesa za uanzilishi alipatia wapi ?

Yeye ni muhindi huku Tanganyika kizazi chake kilifika lini ?

Nini sababu ya wao kufika huku Tanganyika ?
😂😂😂😂 Ss maswali yt hayo ya nn Kwa tajiri mkuu
 
Jamani tujitahidi tupate kitu cha kurithisha watoto wetu. Inasikitisha sana kusikia kijana akisema nasomesha mwanangu aje anisaidie au we zaa tu hujui ni nani atakutoa kwenye shida. ni miongoni mwa kauli za kijinga sana kwa kizazi hiki cha upinde​
 
Inawezekana na yupo sahihi
Kuna kipindi aliingia katika siasa za CCM, ule ndo muda ambao aliutumia kujijenga kwa kuweka mazingira mazuri ya kupata Defense katika biashara zake.

Kupewa mtaji na kuuendeleza it takes time and commitment.
 
Mzee Gulam Dewji baba yake moo ndiye alieifilisi GAPEX alikuwa akichukua mazao ana export pesa hawalipi GAPEX mpaka ikafilisika. Mwl Nyerere alimweka jela kama mhujumu uchumi kwa muda wa kama miaka minne hivi. Kwa hiyo asilimia kubwa ya utajiri ni wizi wa mali umma.

GAPEX lilikuwa ni shirika la Serikali likinunua mazao kwa ajili ya ku export nchi za nje.
Huyu Mzee Gulam ni master minder mkubwa sana. Huyo Moo kaikuta hii pesa ya wizi.
 
Mzee Gulam Dewji baba yake moo ndiye alieifilisi GAPEX alikuwa akichukua mazao ana export pesa hawalipi GAPEX mpaka ikafilisika.Mwl Nyerere alimweka jela kama mhujumu uchumi kwa muda wa kama miaka minne hivi.Kwa hiyo asilimia kubwa ya utajiri ni wizi wa mali umma.
GAPEX lilikuwa ni shirika la serikali likinunua mazao kwa ajili ya ku export nchi za nje.
Huyu Mzee Gulam ni master minder mkubwa sana.Huyo Moo kaikuta hii pesa ya wizi
Kwahiyo
 
Back
Top Bottom