Wajapan wana moyo wa Kizalendo sana, wakati nipo Kenshu Japan kwenye Jiji la Tokyo kuna Wabongo tulikuwa nao Kenshu wana tabia kama za hili jingajinga,
Wakati wa kupita kwenye gate za kuingia kwenye platform za kupanda treni ni miaka mingi wameendelea hakuna mtu unascan tu kadi, sasa kukawa na mchezo wa kadi moja ukiscan mnaweza kupita wote kuna Mjapan raia mwema aliona alikomaa mpaka wote wasiokuwa kadi walikwenda kununuwa kadi ndio wapite kupanda treni na hiyo tabia ilikoma siku hiyo, imagine hapo hakuna security wala nini zimewekwa electronic mashine mjiongoze wenyewe, wenzetu wana kiwango cha juu sana cha ubinadamu na wanawalea watoto hivyo.