Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU), Umoja wa Mataifa(UN) na Mabalozi mbalimbali waendelea kufuatilia kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,232
Pamoja na Serikali ya Tanzania kutopendezwa na Wawakilishi wa kimataifa kutoka EU , UN na Waheshimiwa Mabalozi kujionea dhuluma dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Mbowe Mahakamani , lakini Wazungu hao wameendelea kupuuza wito huo wa Wizara ya mambo ya nje na kuendelea kumiminika kwenye Mahakama ya Uhujumu Uchumi ili kujua kinachoendelea .

Kuna_uwakilishi_wa_Jumuiya_ya_Ulaya,_ubalozi_wa_Marekani,_ubalozi_wa_Canada,_ubalozi_wa_Uinger...jpg
Deogratius_Mahinyila_alipopewa_mashtaka_ya_uhujumu_uchumi,_akafanya_mitihani_na_kufaulu_akiwa_...jpg

Muathirika wa utawala wa kidikteta wa awamu ya 5 aliyeponea tundu la sindano Tito Magoti naye amejivuta kusikiliza ugaidi wa Laki 6

Ndani_ya_chumba_cha_mahakama_muda_huu_Kesi_ya_Ugaidi_ya_Mh._Freeman_Mbowe_na_Wenzake__inaendel...jpg
 
Kutoka barazani mwa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

1hr ago·

Kwa mujibu wa Shahidi wa ACP Ramadhan Kingai (pichani), Freeman Mbowe alimuahidi Luteni Dennis Urio kuwa wakifanikisha kuchukua nchi [kwa njia ya mapinduzi] yeye Mbowe angempa nafasi kubwa.

Hata hivyo, aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais kupitia CHADEMA alikuwa Tundu Lissu. Hivyo kama CHADEMA ingeshinda, Lissu ndio angelikuwa Rais wala siyo Mbowe. Hapa kuna maswali kadhaa:

1. Kama Tundu Lissu ndiye ambaye angelikuwa Rais endapo CHADEMA wangelishinda Urais, Mbowe angewezaje kuahidi kutoa nafasi kubwa kwa watu wengine?

2. Inaonekana Mbowe [kama ushahidi wa ACP Kingai unavyodai] alikuwa tayari kupindua hata Serikali ya Tundu Lissu ili atimize ahadi yake?

3. Kuna kujikanganya kidogo katika mtiririko wa ushahidi: (a) Kuna kauli 'kuelekea Uchagauzi Mkuu'; (b) Kuna mazingira yanayoonyesha kuwa ACP Kingai alipanda cheo na kuushughulikia jambo hilo Novemba 2020, baada ya Uchagauzi Mkuu. Wakili wa Serikali hamuongozi vizuri Shahidi huyo kujibu maswali yaliyojificha, hivyo majibu yake bado yanaacha maswali mengi!

4. Kwa mantiki ya hoja ya 3 hapo juu, ni lini hasa Mbowe et al walipanga kufanya ugaidi wao? Je, ni kabla ya Uchaguzi Mkuu, kuelekea Uchaguzi Mkuu au baada ya Uchaguzi Mkuu?

5. Wakili wa Jamhuri anayemhoji Shahidi ACP Kingai hakuonekana kutilia sana maanani kipengere cha 'lini' katika hojaji yake. Hatujui kama ni makusudi, mkakati, au kupitiwa.

6. Je, hayo mambo yalikuwa kabla ya Uchaguzi Mkuu au kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mbowe alikuwa amejua kuwa CHADEMA kitashindwa Uchaguzi Mkuu?

7. Inakuwaje Mwenyekiti wa Chama kikubwa cha upinzani nchini apange njama nzito kama hizo peke yake na Askari Jeshi mmoja wa kukodi huku Chama chake hakijui?

8. Ni Kiongozi gani wa Chama alijua mpango wa Mbowe au ni kikao gani cha Chama kilijadili kwa siri mpango huo na kilifanyika wapi na kiliwahusisha viongozi gani?

Kesi ya Mbowe na wenzake inavuta hisia za watu wengi. Mambo ndio kwanza yameanza katika Kesi hiyo ambayo ingawa haijatamkwa hivyo, lakini kwa mujibu ushahidi wa ACP Kingai, ilipaswa kuwa ni 'Kesi ya Uhaini'! Kwa kadiri ushahidi utakavyoendelea kutolewa, tutashuhudia mengi sana katika Kesi hii ya kusisimua! Endelea kutega sikio Mahakamani!
Uchambuzi wa Askofu ni mantiki (logic) ya mantiki (Reasoning of a Reason)!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Kutoka barazani mwa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

1hr ago·

Kwa mujibu wa Shahidi wa ACP Ramadhan Kingai (pichani), Freeman Mbowe alimuahidi Luteni Dennis Urio kuwa wakifanikisha kuchukua nchi [kwa njia ya mapinduzi] yeye Mbowe angempa nafasi kubwa...
... pamoja na kwamba ni ushahidi wa kutunga lakini inategemea! Kama Mbowe aliahidi baada ya uteuzi wa nafasi za urais Chadema kufanyika hapo kweli kuna walakini mkubwa sana! Ila kama ilikuwa kabla ya uteuzi, hoja ipo! Sikumbuki Lissu aliteuliwa lini na Mbowe alitoa ahadi hiyo lini kwa mujibu wa Urio! Naona upande wa Serikali ukiomba kwenda kubadili charge sheet!
 
Pamoja na Serikali ya Tanzania kutopendezwa na Wawakilishi wa kimataifa kutoka EU , UN na Waheshimiwa Mabalozi kujionea dhuluma dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Mbowe Mahakamani , lakini Wazungu hao wameendelea kupuuza wito huo wa Wizara ya mambo ya nje na kuendelea kumiminika kwenye Mahakama ya Uhujumu Uchumi ili kujua kinachoendelea .

View attachment 1938700View attachment 1938701
Namuona bibi akidharau mwiba kama alivyofanya kaka yake marehemu...
 
... pamoja na kwamba ni ushahidi wa kutunga lakini inategemea! Kama Mbowe aliahidi baada ya uteuzi wa nafasi za urais Chadema kufanyika hapo kweli kuna walakini mkubwa sana! Ila kama ilikuwa kabla ya uteuzi, hoja ipo! Sikumbuki Lissu aliteuliwa lini na Mbowe alitoa ahadi hiyo lini kwa mujibu wa Urio! Naona upande wa Serikali ukiomba kwenda kubadili charge sheet!
Nilivyomwelewa Mwamakula ni kwamba, Mwongoza ushahidi ham-guide Shahidi kwenye tarehe hasa za matukio hayo yalitokea lini. Sasa kwakuwa mahakama itaamua kwa ushahidi usio na shaka kwenye hili sijui mahakama italichukuliaje.

Ila interestingly ni kuwa Peter atapata muda wa kumfanyia cross examination hapo ndio utajua askari wetu kichwani wapoje....Tundu alikuwa anawatesa sana kwenye kuwafanyia cross examination
 
Nilivyomwelewa Mwamakula ni kwamba, Mwongoza ushahidi ham-guide Shahidi kwenye tarehe hasa za matukio hayo yalitokea lini. Sasa kwakuwa mahakama itaamua kwa ushahidi usio na shaka kwenye hili sijui mahakama italichukuliaje. Ila interestingly ni kuwa Peter atapata muda wa kumfanyia cross examination hapo ndio utajua askari wetu kichwani wapoje....Tundu alikuwa anawatesa sana kwenye kuwafanyia cross examination
... ajabu sana kwa kweli! LINI (WHEN) ni kitu muhimu sana katika ushahidi! Kama wanataka kupanga ushahidi/matokeo vile!
 
Nilivyomwelewa Mwamakula ni kwamba, Mwongoza ushahidi ham-guide Shahidi kwenye tarehe hasa za matukio hayo yalitokea lini. Sasa kwakuwa mahakama itaamua kwa ushahidi usio na shaka kwenye hili sijui mahakama italichukuliaje. Ila interestingly ni kuwa Peter atapata muda wa kumfanyia cross examination hapo ndio utajua askari wetu kichwani wapoje....Tundu alikuwa anawatesa sana kwenye kuwafanyia cross examination
Kingai aweza kuwa mweupe kuliko hata koplo , subiri uone
 
... pamoja na kwamba ni ushahidi wa kutunga lakini inategemea! Kama Mbowe aliahidi baada ya uteuzi wa nafasi za urais Chadema kufanyika hapo kweli kuna walakini mkubwa sana! Ila kama ilikuwa kabla ya uteuzi, hoja ipo! Sikumbuki Lissu aliteuliwa lini na Mbowe alitoa ahadi hiyo lini kwa mujibu wa Urio! Naona upande wa Serikali ukiomba kwenda kubadili charge sheet!
Dudus, these are assertions, lazima uzithibitishe. Mahakama haikubali kusema tu bila ushahidi. Unatoa vielelezo, maana Mbowe atakataa, Sasa Ni wewe ku prove unayoyasema au wasemaje
 
Dawa ya Gaidi ni kumrudisha kwa muumba Hilo ndilo jukumu la Serikali jukumu la Muumba ni kutoa hukumu

Kama ilivyo kwa shetani atapata wafuasi WENGI Sana na ukikosea tu atapewa nafasi ya kututesa kama hatutawahi kumpa anachostahili.

Siwahamini Sana hawa wadau wanaowakilisha na wanatafsiri SHERIA
 
Nilivyomwelewa Mwamakula ni kwamba, Mwongoza ushahidi ham-guide Shahidi kwenye tarehe hasa za matukio hayo yalitokea lini. Sasa kwakuwa mahakama itaamua kwa ushahidi usio na shaka kwenye hili sijui mahakama italichukuliaje. Ila interestingly ni kuwa Peter atapata muda wa kumfanyia cross examination hapo ndio utajua askari wetu kichwani wapoje....Tundu alikuwa anawatesa sana kwenye kuwafanyia cross examination
Lisu level nyingine, lkn definitely atawasiliana na Lisu for some inputs. Hata Mimi kwa ushahidi huu ningelifanya cross examination kali
 
Dawa ya Gaidi ni kumrudisha kwa muumba Hilo ndilo jukumu la Serikali jukumu la Muumba ni kutoa hukumu

Kama ilivyo kwa shetani atapata wafuasi WENGI Sana na ukikosea tu atapewa nafasi ya kututesa kama hatutawahi kumpa anachostahili.

Siwahamini Sana hawa wadau wanaowakilisha na wanatafsiri SHERIA
Kufa wewe ma a yako na baba yako na wote wanaokuhusu
 
Back
Top Bottom