Watoto wa mwisho tukutane hapa

Watoto wa mwisho tukutane hapa

Msalimie Dada mkubwa R mpe hongera kwa kazi nzuri aliyoifanya kwako hata jikoni hupati shida.

Mimi ni wa mwisho niliyetokea kwa bahati. Mpaka kesho kaka yangu ninaemfuata ana mind nimemnyang’anya title yake.

Kuna gap ya five years kati yetu. Maana yake wote walipokuwa boarding nilikuwa home alone kama the only child.

Dada mkubwa ndiye alinifundisha taugh life kama kufua , kupiga deki, kupika. Bila yeye ningekua spoilt rotten.

Karibuni ma last born wenzangu.
 
Dah si kwetu tupo sita halafu mwanaume peke yangu wa mwisho maza alishasemaga mtoto wa kiume sitakiwi niingie jikoni...ila sasa kwenye swala la shule ndo walinipa changamoto nliambiwa nikiferi ntaishia kukaa na mama na kutunza mifugo..ilinifanya nikomae sana niwaoneshe nmewazidi kitabu
 
Daa, Mimi kwetu ni wa mwisho na wa kwanza hadi wa tatu wote ni wa kike. Bahati Mbaya sisi wote tumekulia kwa Bibi mzaa mama ambaye naye alizaaga watoto watatu na wote wa kike. Sasa Mimi ndio amenifanya kama mtoto wake wa kiume, dada zangu wamenibeba hadi nikawa wakati mwingine nakata kutokana na kizomewa na watoto wenzangu kuwa nabebwa wakati mm ni mkubwa.Bibi ndo usiseme hadi Leo akiniona ni Kama ameona sijui kitu gani, amegombana Sana na mama, mama akilalamika kuwa Bibi ananidekeza, lakini pia mama anaamini nampenda Bibi kuliko yeye.
Namshukuru Mungu, pamoja na kunidekeza lakini Bibi alihakikisha nasoma shule, na huwa nasijiskia raha pale kila inapofika tarehe 24 ya kila mwezi namtumia madafu. Kuwa mtoto wa mwisho ni raha kwakweli.
 
Nadhani mi ndo nimecunja record nimekua wa mwisho na mpishano mkubwa sana miaka 11 usiombe ni shida sana na ndugu zangu baadhi tena wa kike wana roho mbaya sana coz wana watt zao wanaangalia familia zao tu
 
Ongeeni yooote, ila kudate na hawa ma last born inakubidi uwe na Moyo wa Chuma cha Pua.
 
Back
Top Bottom