Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Hawa viongozi wetu wanacheza tu na akili zetu! Haya ni maonesho tu yasiyokuwa na uhalisia! Mbona mengine hatuambiwi? Kwani ni wizara ya frdha tu wanalipana maposho makubwa? Ubadhirifu upo kila mahali lakini mnachagua sehemu ambayo mnajua mtawapumbaza wananchi! In fact hakuna litakaloendelea kwa sababu sheria navtsratibu zinawaruhusu kujilipa walivyojilipa! Acheni kutuchezea akili nyie!
Nchi hii mtumishi ambae hana posho ni mwalimu tu. Huyu kila kitu ataambiwa awe mzalendo.
 
Tuhuma hapa ni zaidi ya sh bilioni moja!! Mama upo?? Wanataka kukufanya kama bibi yao! Onyesha kuwa wewe ni mama na siyo bibi!! Vuta masikio yao mpaka wakome!
 
Huwa anakurupuka!!,unawasimamisha bila uchunguzi,na vyombo vya habari vinaitwa.
Lakini,jamii inataka kujua malipo ya kati ya mwezi wa JANUARI na FEBRUARI,kabla ya ule msiba wa taifa.Sasa mbona haya matumizi yameanzia mwezi MACHI.
Hii nayo inaweza kuwa ni mchezo wa kuigiza,makubwa yameachwa wameshughulika na jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi.
Huu ni upuuzi tu, unless mwandishi kakosea. Sina hakika kama ni kazi ya Mkaguzi Mkuu kufanya kazi ya Pre-Audit. My understanding pre-audit inafanyika kabla malipo hayajafanyika.

Hii ni kazi ya Mweka Hazina/ Accountant. Lingekuwa ni tukio la mwaka uliopita ambao tayari Mkaguzi ameufanyia kazi, basi ningemuelewa Majaliwa.

Napataga shida kumuelewa huyu bwana.
 
Very smart prime minister.

Ila kuwa Makini mzee maana imani ya Watanzania imeelekezwa zaidi kwako sasa,Japo Kundi la mafisadi,watumishi wazembe na wezi wa mali za umma bado linakuona wewe ni kikwazo kwao
Namkubali Sana majaliwa 100%,baada be ya kifo Cha JPM huyu ndo amebaki kuwa faraja yangu katika usimamizi wa pesa za imma.

Mungu amlinde daima
 
Kwahio unadhani enzi zake kulikuwa hakuna upigaji ? Tofauti ni kwamba enzi zake upigaji mwingine usingesikia ingawa hata sasa angalau tunasikia robo tatu ingawa sio wote..., enzi za mwendazake ungesikia tu ule aliotaka yeye usikie...
Sio kweli mkuu.wizi haukuwepo walimuogopa Mwendazake maana ukibainika ulikua una hatari ya kupoteza kila kitu.sema miradi mingine aliyoibariki na kuiendesha ndo ilikua unaleta hasara kutoka kwenye riport ya ndugu CAG ,pia matumizi mengi nje ya bajeti lakini tutamkumbuka kwa kutukomeshea wezi walipotea kabisa naona wameanza kurudi taratibu.kazi iendelee
 
Huwa anakurupuka!!,unawasimamisha bila uchunguzi,na vyombo vya habari vinaitwa.
Lakini,jamii inataka kujua malipo ya kati ya mwezi wa JANUARI na FEBRUARI,kabla ya ule msiba wa taifa.Sasa mbona haya matumizi yameanzia mwezi MACHI.
Hii nayo inaweza kuwa ni mchezo wa kuigiza,makubwa yameachwa wameshughulika na jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi.
Kusema PM amekurupuka sio ustaarabu acha chuki mkuu hata Kama we ni mpinzani Kuna Mambo ya kupongeza pale hatua nzuri zinapochukuliwa kwa maslahi mapana ya Taifa
 
Hii habari haijakaa sawa.

Taratibu za fedha zina mtu aliyeomba hiyo fedha, wapo walioidhinisha hayo malipo, ndo na mkaguzi ni mmojawapo, yupo aliyelipwa, aliyetumia nk.

Na kila kitu kipo kwenye mfumo wa fedha.

Mtu muhimu ni aliyeinitiate hayo malipo. Faili la malipo lipo online.
Ninao wasiwasi huenda PM hajui utaratibu wa malipo hasa kiuhasibu.

Internal audit department/unit/section wanakuja kuona hiyo PV wakati hiyo pesa ishalipwa na inawezekana ishaliwa na kuisha hasa kwa kawaida yetu ya kuandaa taarifa in Monthly/quarterly bases. Unless hapa kuwe na mis information kuwa azungumzia Kitengo cha Pre Audit au Examination.

Wa kwanza kumtia ndani hapo alitakiwa initiator(aliye-sign Dokezo) origination department mkuu wa idara ambaye activity iko chini yake na authorizer (afisa maduhuli) haiwezekani hadi dokezo linapita wote wasinuse wizi huu.
 
I still consider the whole approach “idiotic” hii kwenda public kwenye issue kama hii kunawavunja moyo walipakodi na wakusanya kodi.
Hapa inatakiwa kumkimbiza mwizi na ku-deal naye kimya kimya
 
Tuliza mshono. Lazima watumbiliwe. Ala.
Huwa anakurupuka!!,unawasimamisha bila uchunguzi,na vyombo vya habari vinaitwa.
Lakini,jamii inataka kujua malipo ya kati ya mwezi wa JANUARI na FEBRUARI,kabla ya ule msiba wa taifa.Sasa mbona haya matumizi yameanzia mwezi MACHI.
Hii nayo inaweza kuwa ni mchezo wa kuigiza,makubwa yameachwa wameshughulika na jambo ambalo halijafanyiwa uchunguzi.
 
Kama walioinitiate process ya kukwapua hizo pesa ni wanene sana, mwisho wa siku watakwambia hizo pesa zilitoka katika process nzima ya mazishi ya the late JPM.
 
Sio kweli mkuu.wizi haukuwepo walimuogopa Mwendazake maana ukibainika ulikua una hatari ya kupoteza kila kitu.sema miradi mingine aliyoibariki na kuiendesha ndo ilikua unaleta hasara kutoka kwenye riport ya ndugu CAG ,pia matumizi mengi nje ya bajeti lakini tutamkumbuka kwa kutukomeshea wezi walipotea kabisa naona wameanza kurudi taratibu.kazi iendelee
Unajuaje ?
Sababu haukusikia ?, Kwa uongozi ambao information inafinywa na kuna propaganda unawezaje kujua ?
By the way nini maana ya wizi / kuiba / ufisadi ?

Kufanya vitu bila utaratibu / kufuata sheria sio wizi / ufisadi ?
 
Waibe wengine ajiuzulu waziri!. Dawa ni kufukuza kazi hao wezi na kuwafikisha mahakamani. Ajiuzulu waziri halafu wale wezi waendelee kudunda mtaani!!.

Hili sio suala lenye kufanana na Mwinyi alipojiuzulu mwaka 1975. Kipindi kile walikufa watu kwa ujinga wa waliokuwa chini ya waziri wa mambo ya ndani. Hili la Mwigulu hajafa mtu bali kuna wezi wa chini yake, fukuza kazi hao waheshimiwa kama ushahidi upo wenye kujitosheleza, ili wengine wajifunze kupitia adhabu wanayopewa.
 
Back
Top Bottom