Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Wizara ya Mambo ya Ndani na wizara ya fedha ni kati ya Wizara ngumu sana...
 
Hii wizara ibomolewe kabisa ina staff wezi wa kubuhu. Sio leo wala jana hawa ni tabu.
 
Nn maana ya uwajibikaji???tuanzie hapo kwanza
Waibe wengine ajiuzulu waziri!. Dawa ni kufukuza kazi hao wezi na kuwafikisha mahakamani. Ajiuzulu waziri halafu wale wezi waendelee kudunda mtaani!!.

Hili sio suala lenye kufanana na Mwinyi alipojiuzulu mwaka 1975. Kipindi kile walikufa watu kwa ujinga wa waliokuwa chini ya waziri wa mambo ya ndani. Hili la Mwigulu hajafa mtu bali kuna wezi wa chini yake, fukuza kazi hao waheshimiwa kama ushahidi upo wenye kujitosheleza, ili wengine wajifunze kupitia adhabu wanayopewa.
 
Je kama Mwigulu ndo alimuambia PM kuhusu wizi????....Alaf Mwigulu ana muda mfuoi sana kwenye hiyo wizara. Wizi ulianza mapema hata kabla hajaingia
 
Haahaa, afrika inahitaji taasisi imara Sio watu imara mkuu, Sheria zetu nyingi Ni za uonevu mtupu badala ya kulinda rasilimali zetu, wizi upo muda wote na awamu zote.Tulishuhudia jpm akitembea na mabilioni kwenye magari na kugawa hovyo kwa watu binafsi wote ule Ni wizi mtupu
Hata hizo taasisi imara zitaongozwa na nani ambaye atakuwa imara chief?.

JPM tunamsingizia utadhani ni yeye tu ndiye alikuwa anatembea na hayo unayoita mabilioni, hata kina kikwete itwas the same although utakuwa umesahau.

Bado narudia Afrika inahitaji watu jasiri wasiyo vibaka, late Gadaffi alikuwa jasiri sana, kuna yule wa Nigeria alikuwa mwanajeshi alifanya makubwa sana mpaka waliokuja kina Goodruck waliteleza kuipaisha Nigeria kwa sababu yule mjeshi aliwafunga mikanda wananchi.

Na ndiyo Nigeria hii ambayo inapambana na kiuchumi na Afrika kusini.
 
Kama walioinitiate process ya kukwapua hizo pesa ni wanene sana, mwisho wa siku watakwambia hizo pesa zilitoka katika process nzima ya mazishi ya the late JPM.
Wanene pekee ndiyo wenye uthubutu wa kuomba malipo ya m250+, wasioulizwa, wengine hawawezi.
Nafikiri PM kama anajitutumisha fulani hivi, ila hii inaweza kum-cost, jamaa watamfix na matukio aonekane hafai kabisa!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Ingelikua ni dagaa "wanashikiliwa na jeshi la polisi"
Papa "wamesimamishwa kupisha uchunguzi"

Nani huyo atakayetuwekea mifumo ya nchi kujitegemea kiuendeshaji na sisi kuisimamia mifumo hiyo?
Tz yangu inuka ujitetee.
 
Kipimo cha "Kazi Iendelee" kitaonekana hapa! Kama ni Mwigulu ameliona hili akaona atoe habari basi wananchi tufahamishwe haraka tujue. La sivyo hii ina maanisha kwamba waajiriwa hewa wameshaanza kurudi serikalini. Hili linaogopesha, wahusika wafunguliwe mashtaka haraka iwezekanavyo.
 
Nadhani wengi hatufahamu. Kulipana kwa namna hiyo kumekuwepo hapo Wizara ya Fedha kwa muda mrefu sasa. Huo ni mwendelezo tuu. Haikuanza March mwaka huu. Hongera kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuona hili
 
Si mlisema mzunguko wa hela uraiani Mwendazake aliuubana.
Sasa tusubiri huku tutazipata wakati wa kuchimba misingi ya mahekalu yao, au baa.
Muhimu wazuie wasitoroshe nje ya nchi
 
RAIS WA TANZANIA 2025 kweli watu wanaiba yuko ofisini..anaumbuliwa na waziri mkuu ..yeye alikuwa wapi kuyajua haya ......
Mwigulu apunguze siasa ..na kuzungukwa na madalali , afanye kazi , kwa mwendo huu watamtumbua ..
Kwa mwendo huu? HeLa zishapigwa afu unasema "ata" asee wabongo mnawahi kusameh
 
Waibe wengine ajiuzulu waziri!. Dawa ni kufukuza kazi hao wezi na kuwafikisha mahakamani. Ajiuzulu waziri halafu wale wezi waendelee kudunda mtaani!!.

Hili sio suala lenye kufanana na Mwinyi alipojiuzulu mwaka 1975. Kipindi kile walikufa watu kwa ujinga wa waliokuwa chini ya waziri wa mambo ya ndani. Hili la Mwigulu hajafa mtu bali kuna wezi wa chini yake, fukuza kazi hao waheshimiwa kama ushahidi upo wenye kujitosheleza, ili wengine wajifunze kupitia adhabu wanayopewa.
Ajiuzulu na wezi wafukuzwe.
 
Kipimo cha "Kazi Iendelee" kitaonekana hapa! Kama ni Mwigulu ameliona hili akaona atoe habari basi wananchi tufahamishwe haraka tujue. La sivyo hii ina maanisha kwamba waajiriwa hewa wameshaanza kurudi serikalini. Hili linaogopesha, wahusika wafunguliwe mashtaka haraka iwezekanavyo.
Mnaanza kutengeneza mazingira
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom