Martha Mariki akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya Tsh. Trilioni 10.125 Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,173
1,028

MHE. Martha Mariki Akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya Tsh. Trilioni 10.125 Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

"Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyofanya kazi kubwa katika Taifa letu la Tanzania na katika Mkoa wa Katavi kwa kuleta fedha zaidi ya Shilingi Trilioni 1.2 ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassa." - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Wananchi wa Katavi tunazidi kumuombea kwa MUNGU aendelee kumpa afya njema Rais wetu kwani ameendelea kuboresha sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Katavi tumepata Vituo vya Afya zaidi ya 20, Zahanati zaidi ya 36. Sekta ya Afya imeboreshwa katika Mkoa wa Katavi" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nampongeza Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko kwa usimamizi mzuri wa fedha nyingi za miradi zilizoletwa katika Mkoa wa Katavi ndani ya Miaka mitatu ya uongozi wa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nakupongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Manaibu Mawaziri na watendaji wote wa TAMISEMI lakini wananchi wa Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Tanganyika katika Kata ya Ilangu ni Kata ya kimkakati na ina idadi kubwa ya watu ambao wameanza kujichanga fedha kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya. Mama zangu wanatembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Wananchi wa Kata ya Ilangu (Tanganyika) wameonyesha juhudi za kujenga Kituo cha Afya, Naiomba Wizara husika muweze kutenga fedha kwaajili ya kuwajengea wananchi kituo cha Afya ili waweze kuepukana kutembea umbali mrefu hususani wamama wanaokwenda kujifungua" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mambo mazuri yanafanyika TAMISEMI lakini bado kuna upungufu mkubwa wa watumishi katika vituo vya afya. Mkoa wa Katavi pekee tuna uhaba wa zaidi ya asilimia 57. Tuna watumishi asilimia 43, bado wananchi hawapati huduma iliyokusudiwa kutokana na uchache wa watumishi. Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Daktari ni mmoja" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mkoa wa Katavi kuna ukosefu mkubwa wa nyumba za watumishi. Halmashauri ya Nsimbo watumishi wa sekta ya Afya wanalazimika kuja maeneo ya Mjini kwaajili ya kupanga nyumba. Na Hospitali za Wilaya zilijengwa mbali na makazi ya wananchi. Watumishi wanalazimika kupanga nyumba maeneo ya Mijini. Wizara TAMISEMI liangalieni suala la nyumba za watumishi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ukaribu na kwa ufanisi" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Katavi tumepata fedha nyingi za miradi ya BOOST kuboresha sekta ya elimu lakini ziko changamoto za uchakavu mkubwa wa Shule kongwe zilizojengwa miaka ya 1970 lakini shule hizo mazingira hayaridhishi na kutokana na Mvua za Elinino kuta zinaweza kuwaangukia watoto. Wizara ya TAMISEMI tengeni fedha kuboresha" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Mtendaji Mkuu wa TARURA, Eng. Seif anafanya kazi nzuri. Tumesema wabunge TARURA iongezewe fedha lakini kule chini kuna changamoto kumekuwa na ujenzi wa Mitaro iliyo chini ya kiwango, wanatumia madini ujenzi hayana kiwango. Nini kinasababisha Mitaro inajengwa ila ikinyesha Mvua kidogo Mitaro yote inaharibika, hii haikutokea kwa Mvua za mwaka huu, hata miaka ya nyuma Mitaro imekuwa inajengwa chini ya kiwango" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nitumie fursa kutoa pole kwa maeneo yote nchini yaliyokumbwa na mafuriko ikiwemo eneo la Rufiji. Nawapa pole wananchi wenzangu wa Mkoa wa Katavi kutokana na mvua zilizonyesha, sasa hatuma mawasiliano kutoka Katavi kwenda Kigoma na Katavi kwenda Rukwa. Tunaamini Serikali ni sikivu, Wahandisi wa TARURA wapo pale kuhakikisha changamoto inatatuliwa" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-18 at 01.14.07.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-18 at 01.14.07.jpeg
    97.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom